Majanga ya Asili: Tukafanye utafiti kwa Wahadzabe na wanaofanana nao ili tufahamu jinsi wanavyotambua majanga haya kabla hayajatokea?

Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na kwa Maslahi ya Taifa. Leo ni kuhusu Natural Disasters: Jee Tuwafanyie Research watu wa makabila ya Wabarbaig, Wahadzabe, Wataturu, Wasandawe na Watindinga, huwa wanajuaje kutatokea natural disasters na kukimbia eneo hilo kabla ya majanga hayajatokea?

Japo wazungu wanasemekana ni wataalamu sana wa sayansi lakini hawawezi ku detect tetemeko la ardhi kabla halijatokea, au mlipuko wa volcano, lakini wanyama wa porini wana uwezo wa kudetect na makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo!

Mlima Hanang uko kwenye safu ya milima ya volcanic mountains kama Oldonyo Lengai, usikute una volcano hai!. Enzi zile Oldonyo Lengai, ulipofuka moshi mzito, na majivu yale yaliwaathiri wanyama na mifugo, ya kufungwa ndio iliathirika kutokana na kufungiwa lakini wanyama wa porini wao walijua na walikimbia kabla.

Watu wa makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana natural seismology intelligence hivyo wana uwezo huo kwa kuwasikia wanyama pori, wakiwaona wanakimbia kukimbilia direction fulani, nao hukimbia, na baada ya kukimbia ndipo huku nyuma, hutokea la kutokea.

Tusiwategemee sana Wazungu na research zao, na vifaa vyao, tufanye utafiti wa haya makabila ya wawindaji wa asili wanatumia nini na viashiria gani kuyakimbia maeneo kabla majanga hayajatokea!.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wanasema walisikia mlipuko kama wa volcano usiku wa manane na hali kama ya tetemeko la ardhi, ndipo ikanyesha mvua kubwa mlima Katesh na kusababisha maporomoko ya udongo yaliyosombwa na mafuriko na kuzisomba nyumba za wakazi wa chini ya mlima ambapo watu zaidi ya 50 wamefariki dunia, mamia kujeruhiwa na mamia wengine hawana makazi wala mahali pa kuishi.

Mashuhuda hao wamesema mpaka kunakucha walikuwa wanaona mvuke ukipaa juu kutoka mlima Hanang.

Ikifanywa research ya waathirika wa janga hili la mafuriko ya Mlima Katesh unaweza kukuta, wale wanaioshi milimani na wanyama wa porini waliisha kimbia usiku usiku kabla ya janga hilo!

Na kufuatia imani za kiasili, (siiti za kishirikina), kuna watu wana nguvu na uwezo wa ajabu ama kusababisha majanga ama ku control majanga. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alikuwa akiwapiga maadui zake kwa mvua ya mawe na kumrarua kiongozi wao kwa kumpiga radi.

Kuna watu wanapaa usiku kwa ungo, kuna watu wanapanda fisi anapaa hewani, kuna watu wanatumia nyoka kulinda mashamba yao, kuna watu wanatumia mazindiko fulani, ukiingia kuiba, unamangamanga mpaka asubuhi unakutwa.

Hizi zote ni sayasi za kiasili za Kiafrika, zikifanyiwa research, zitalisaidia sana taifa letu. Mnaonaje kama tutafanya research kwenye hili?

Natoa tena pole kwa wahanga wa janga hili na nimemsikia Mama, amekatisha ziara ya Dubai kurejea nyumbani kuimarisha juhudi za uokozi na utengemano.

Enzi za JPM kulipotokea Tetemeko la ardhi Bukoba, JPM aliahirisha ziara ya Zambia tukitegemea angeibukia Bukoba lakini kilichotokea tukabaki kuulizana Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, "Sema Neno Moja Tuu, na Roho Zetu Zitapona!"

Mungu inusuru Hanang,
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Wale mliohatibiwa na makanisa na misikiti yenu mtasema ni wachawi

Nina Imani na African traditions kuliko hizo mambo zenu za Wazungu.
 
Wanasema ulisikika mlipuko mkubwa wakati wa usiku, mlipuko uliodhaniwa kuwa wa volcano, lakini mawe tunayoambiwa yaliporomoka kutoka mlimani yalisababishwa na maji ya mvua iliyonyesha.

Sasa hapo kuna connection ipi kati ya mvua na volcano ya usiku, au volcano pia inaweza kuleta mvua?

Naona hapa lazima wapatikane wanasayansi kututhibitishia hili, na sio hao wabarbaig na wenzao.

By the way sidhani kama kukimbia hatari ni suala linalohitaji kuhusishwa na makabila fulani, mimi au wewe tunapohisi hali ya hatari kwa sababu ya tukio lisilo la kawaida, kukimbia ni jambo la kawaida.

Tatizo naloliona hapo, inawezekana wajanja wa mjini hawakukimbia kwasababu tu ya ujanja wao, na hao jamaa zangu wakakimbia kwasababu tu ya ushamba wao, matokeo yake ushamba wao ukawaokoa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Serikali imetuma Wataalamu wa miamba kuchunguza Kwa sababu Kwa mujibu wa RC Sendiga Bado hawana uhakika ni nini hasa kilisababisha majanga.

Bado Nina Imani na Mila za kiasi za Afrika kuliko hizo dini na sayansi zenu za Wazungu
 
Wanyama hasa ng'ombe wana detect janga kwa haraka sana naturally mara umuonapo analia huku anakimbia katika utaratibu wake usio wakawaida take care!, ng'ombe iliwahi kuniokoa na janga la radi. Wenzetu wahindi wakaona isiwe tabu, wakamfanya ni Mungu.
Sio Mungu just alama ya kuelekea Kwa Mungu wao.

Mambo kama haya tunatakiwa kufundishana.
 
1. Kwa case ya wanyama: kama ambavyo Mungu (nature) ame(ime)mzawadia mwanadamu ubongo wenye uwezo mkubwa, basi ame(ime)wazawadia wanyama uwezo mkubwa katika Milango ya fahamu kuliko hata mwandamu hasa mlango wa fahamu wa kunusa na mlango wa fahamu wa kusikia.
Kabla janga lolote la asili kutokea, kunakuwa na ishara za chini chini ambazo mwanadamu hawezi Ku detect. Kunakuwa na mabadiliko ya harufu ya hewa ya eneo.
Mfano kwa tetemeko, kunakuwa na mitetemo ya chini sana ambayo ndege, wanyama jamii ya Paka(Panthera Leos) wanasikia.
Sasa wakikisikia, basi kuhama kunaanza na hivyo hata wanyama wengine huiga wanapoona wenzao wanachama.
Mvua kubwa ina harufu yake, upepo mkali una harufu na mitetemo yake, volcano ina harufu yake ya kabla na mitetemo yake ya kabla(pre-condition).
Tetemeko la ardhi lina mitetemo midogo midogo ya kabla. Lina harufu yake ya kabla.
2. Kwa case ya hayo makabila, wao kwa sehemu kubwa bado wanategemea uasili. Husoma tabia za wanyama, ndege na miti. Wakiona mabadiliko fulani ya kuhama kwa wanyama, sauti ya wanyama na ndege, miti na udongo, basi nao hu detect jambo zuri au baya.
Pia hutumia uzoefu wa miaka mingi ambayo hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Experience is the best teacher.
Kuna sehemu Huwa nikipita shambani Kuna kamsitu Huwa nikifika tuu nasikia mlio Fulani wa ndege.

Huwa sielewi huyo ndege ana wa alart wenzie au ana ni alart Mimi au ikoje na Huwa simuoni.
 
Dah, nipe details zaidi mkuu kuhusu hiyo radi na uokozi wa ng'ombe. Naziheshimu mno radi na juzi zimetoka kupifa mji wetu huu si za kawaida hadi watu na familia zao wakakimbilia chini ya kitanda.
Nilikuwa napita zangu na njia, katika njia hiyo huwa na mifugo hasa ng'ombe wengi huwa wanajilia majani, ilikuwa ni siku iliyokuwa na mawinga kiasi lakini mvua ilikuwa haijaanza kunyesha, wingu likazidi kutanda, ghafla nikaona wale ngombe wakaanza kulia huku wanakuwa kama wamechanganyikiwa, mwanawane nikashtuka nikakimbilia pahala palikuwa na kajibanda ka mabati, mkuu hazikupita dakika 5,lilishuka furushi moto ukachoma manyasi kikafuata kishindo cha ngurumo!, ajabu mpaka nyasi zile ambazo ngombe walikuwepo ziliungua na kuwa nyeusi mpaka mchanga wa lile eneo, hii kitu isikieni tu.
 
Tv zetu zote zinaendelea kurusha tu vipindi vya kawaida, business as usual kama vile hamna dharura ya kitaifa. Hili janga liwe ni fursa ya kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwepo na maeneo ya hifadhi. Sio kila mahali paruhusiwe kufanyika shughuli za kibinadamu. Athari za mabadiliko ya tabia nchi na athari za kimazingira zinasababishwa na sisi wenyewe kwa zaidi ya asilimia 90. Tusimsingizie Mungu.
Serikali haijatangaza Janga ,Huwa Kuna utaratibu
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na kwa Maslahi ya Taifa. Leo ni kuhusu Natural Disasters: Jee Tuwafanyie Research watu wa makabila ya Wabarbaig, Wahadzabe, Wataturu, Wasandawe na Watindinga, huwa wanajuaje kutatokea natural disasters na kukimbia eneo hilo kabla ya majanga hayajatokea?

Japo wazungu wanasemekana ni wataalamu sana wa sayansi lakini hawawezi ku detect tetemeko la ardhi kabla halijatokea, au mlipuko wa volcano, lakini wanyama wa porini wana uwezo wa kudetect na makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo!

Mlima Hanang uko kwenye safu ya milima ya volcanic mountains kama Oldonyo Lengai, usikute una volcano hai!. Enzi zile Oldonyo Lengai, ulipofuka moshi mzito, na majivu yale yaliwaathiri wanyama na mifugo, ya kufungwa ndio iliathirika kutokana na kufungiwa lakini wanyama wa porini wao walijua na walikimbia kabla.

Watu wa makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana natural seismology intelligence hivyo wana uwezo huo kwa kuwasikia wanyama pori, wakiwaona wanakimbia kukimbilia direction fulani, nao hukimbia, na baada ya kukimbia ndipo huku nyuma, hutokea la kutokea.

Tusiwategemee sana Wazungu na research zao, na vifaa vyao, tufanye utafiti wa haya makabila ya wawindaji wa asili wanatumia nini na viashiria gani kuyakimbia maeneo kabla majanga hayajatokea!.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wanasema walisikia mlipuko kama wa volcano usiku wa manane na hali kama ya tetemeko la ardhi, ndipo ikanyesha mvua kubwa mlima Katesh na kusababisha maporomoko ya udongo yaliyosombwa na mafuriko na kuzisomba nyumba za wakazi wa chini ya mlima ambapo watu zaidi ya 50 wamefariki dunia, mamia kujeruhiwa na mamia wengine hawana makazi wala mahali pa kuishi.

Mashuhuda hao wamesema mpaka kunakucha walikuwa wanaona mvuke ukipaa juu kutoka mlima Hanang.

Ikifanywa research ya waathirika wa janga hili la mafuriko ya Mlima Katesh unaweza kukuta, wale wanaioshi milimani na wanyama wa porini waliisha kimbia usiku usiku kabla ya janga hilo!

Na kufuatia imani za kiasili, (siiti za kishirikina), kuna watu wana nguvu na uwezo wa ajabu ama kusababisha majanga ama ku control majanga. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alikuwa akiwapiga maadui zake kwa mvua ya mawe na kumrarua kiongozi wao kwa kumpiga radi.

Kuna watu wanapaa usiku kwa ungo, kuna watu wanapanda fisi anapaa hewani, kuna watu wanatumia nyoka kulinda mashamba yao, kuna watu wanatumia mazindiko fulani, ukiingia kuiba, unamangamanga mpaka asubuhi unakutwa.

Hizi zote ni sayasi za kiasili za Kiafrika, zikifanyiwa research, zitalisaidia sana taifa letu. Mnaonaje kama tutafanya research kwenye hili?

Natoa tena pole kwa wahanga wa janga hili na nimemsikia Mama, amekatisha ziara ya Dubai kurejea nyumbani kuimarisha juhudi za uokozi na utengemano.

Enzi za JPM kulipotokea Tetemeko la ardhi Bukoba, JPM aliahirisha ziara ya Zambia tukitegemea angeibukia Bukoba lakini kilichotokea tukabaki kuulizana Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, "Sema Neno Moja Tuu, na Roho Zetu Zitapona!"

Mungu inusuru Hanang,
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Indigenous & local knowledge ni silaha muhimu sana kwenye maisha!
Sema watu wa maghorofani hawajui umuhimu wake!
Kifupi ukiwa mwenyeji wa eneo fulani kuna vitu utavijua kwa kujiconnect na nature kuliko wageni!
 
Nilikuwa napita zangu na njia, katika njia hiyo huwa na mifugo hasa ng'ombe wengi huwa wanajilia majani, ilikuwa ni siku iliyokuwa na mawinga kiasi lakini mvua ilikuwa haijaanza kunyesha, wingu likazidi kutanda, ghafla nikaona wale ngombe wakaanza kulia huku wanakuwa kama wamechanganyikiwa, mwanawane nikashtuka nikakimbilia pahala palikuwa na kajibanda ka mabati, mkuu hazikupita dakika 5,lilishuka furushi moto ukachoma manyasi kikafuata kishindo cha ngurumo!, ajabu mpaka nyasi zile ambazo ngombe walikuwepo ziliungua na kuwa nyeusi mpaka mchanga wa lile eneo, hii kitu isikieni tu.
Radi iliwahi nikosa wakati Niko mdogo shule ya msingi.Mvua ilikuwa inayesha na ngurumo za Radi kama kawaida.Nikawa natoka nakimbia kwenye mvua kwenda home pekupeku.

Ilipoga rasi mbele yangu yaani sehemu ilikuwa imejaa maji ya Kate ganishwa na pakawa pakavj hiyo niliona wakati nimeanguka nainuka,nashukuru Mungu niliponaje sijui ila ilikuwa noma sana.

Nyingine tukiwa bweni Songea huko Shule Ina miti mikubwa mirefu kama. Yote,jioni mvua inanyesha,ilipoga rasi na kuchana Bonge la mti huku kwenye mabweni watu walianguka kutoka kwenye vitand vya Juu ni noma sana.
 
Madhara ya kuharibu uoto wa asili!

Hajuna anayelinda na kuyatunza uoto wa asili

Ova
Sahihi viumbe vya asili vilikuwa waweza viangalia ukajua Nini ni Nini? Mfano ukiona baadhi ya ndege waliokuwa wakijaa kwenye pori Kwa wingi aina tofauti hawapo Tena wakati uoto upo unajua kabisa ukame unakuja iwekwe mikakati kama kutunza chakula kutouza hovyo nk lakini Sasa hivi uoto wa asili Haipo tumejaza miti ulaya na miti ya kigeni ambayo ndege pekee awezaye Jenga hata kipya sio ndege wa asili ni kunguru wa India waliozagaa Dar na Zanzibar

Turudishe uoto wa Asili ndege,wadudu wa asili,na wanyama wa asili watarudi

Huwezi panda mbuga miti ulaya ,Miti ya miashoki na miti ya miarobaini eti kampeni ya panda miti halafu utegemee ndege wa asili,wanyama wa asili na wadudu wa asili warudi ikiwemo mboga pori za asili na uyoga wa asili uoatao kwenye uoto wa asili nk urudi

Wataalamu wa vitalu vya miti waanzishe vitalu vya asili waachane na ujinga wa kutuunzia Miche ya miti isiyo ya asili eti tukapande

Serikali iwekeze kwenye kurudisha uoto wa asili Kila Kijiji Tanzania kama walivyo na miradi ya REA umeme vijijini wawekeze kwenye kurudisha uoto wa asili
 
Radi iliwahi nikosa wakati Niko mdogo shule ya msingi.Mvua ilikuwa inayesha na ngurumo za Radi kama kawaida.Nikawa natoka nakimbia kwenye mvua kwenda home pekupeku.

Ilipoga rasi mbele yangu yaani sehemu ilikuwa imejaa maji ya Kate ganishwa na pakawa pakavj hiyo niliona wakati nimeanguka nainuka,nashukuru Mungu niliponaje sijui ila ilikuwa noma sana.

Nyingine tukiwa bweni Songea huko Shule Ina miti mikubwa mirefu kama. Yote,jioni mvua inanyesha,ilipoga rasi na kuchana Bonge la mti huku kwenye mabweni watu walianguka kutoka kwenye vitand vya Juu ni noma sana.
Hatari sana radi isikie tu

Radi inachana mti mzima mzima

Zile voltage zake si masihara

Ova
 
PASCO Acha uhuni juzi umevuta ndege Kwa kamba bado hujajifunza?CCM wapo Kwa akili ya maslahi Yao sio raia
 
Pascal Mayalla
Wewe ni mwandishi mzuri sana, nakushauri uende uhazabeni ukafanye utafiti.
Ukitaka ufadhili useme mapema nitakuunga na wafadhili.
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na kwa Maslahi ya Taifa. Leo ni kuhusu Natural Disasters: Jee Tuwafanyie Research watu wa makabila ya Wabarbaig, Wahadzabe, Wataturu, Wasandawe na Watindinga, huwa wanajuaje kutatokea natural disasters na kukimbia eneo hilo kabla ya majanga hayajatokea?

Japo wazungu wanasemekana ni wataalamu sana wa sayansi lakini hawawezi ku detect tetemeko la ardhi kabla halijatokea, au mlipuko wa volcano, lakini wanyama wa porini wana uwezo wa kudetect na makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo!

Mlima Hanang uko kwenye safu ya milima ya volcanic mountains kama Oldonyo Lengai, usikute una volcano hai!. Enzi zile Oldonyo Lengai, ulipofuka moshi mzito, na majivu yale yaliwaathiri wanyama na mifugo, ya kufungwa ndio iliathirika kutokana na kufungiwa lakini wanyama wa porini wao walijua na walikimbia kabla.

Watu wa makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana natural seismology intelligence hivyo wana uwezo huo kwa kuwasikia wanyama pori, wakiwaona wanakimbia kukimbilia direction fulani, nao hukimbia, na baada ya kukimbia ndipo huku nyuma, hutokea la kutokea.

Tusiwategemee sana Wazungu na research zao, na vifaa vyao, tufanye utafiti wa haya makabila ya wawindaji wa asili wanatumia nini na viashiria gani kuyakimbia maeneo kabla majanga hayajatokea!.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wanasema walisikia mlipuko kama wa volcano usiku wa manane na hali kama ya tetemeko la ardhi, ndipo ikanyesha mvua kubwa mlima Katesh na kusababisha maporomoko ya udongo yaliyosombwa na mafuriko na kuzisomba nyumba za wakazi wa chini ya mlima ambapo watu zaidi ya 50 wamefariki dunia, mamia kujeruhiwa na mamia wengine hawana makazi wala mahali pa kuishi.

Mashuhuda hao wamesema mpaka kunakucha walikuwa wanaona mvuke ukipaa juu kutoka mlima Hanang.

Ikifanywa research ya waathirika wa janga hili la mafuriko ya Mlima Katesh unaweza kukuta, wale wanaioshi milimani na wanyama wa porini waliisha kimbia usiku usiku kabla ya janga hilo!

Na kufuatia imani za kiasili, (siiti za kishirikina), kuna watu wana nguvu na uwezo wa ajabu ama kusababisha majanga ama ku control majanga. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alikuwa akiwapiga maadui zake kwa mvua ya mawe na kumrarua kiongozi wao kwa kumpiga radi.

Kuna watu wanapaa usiku kwa ungo, kuna watu wanapanda fisi anapaa hewani, kuna watu wanatumia nyoka kulinda mashamba yao, kuna watu wanatumia mazindiko fulani, ukiingia kuiba, unamangamanga mpaka asubuhi unakutwa.

Hizi zote ni sayasi za kiasili za Kiafrika, zikifanyiwa research, zitalisaidia sana taifa letu. Mnaonaje kama tutafanya research kwenye hili?

Natoa tena pole kwa wahanga wa janga hili na nimemsikia Mama, amekatisha ziara ya Dubai kurejea nyumbani kuimarisha juhudi za uokozi na utengemano.

Enzi za JPM kulipotokea Tetemeko la ardhi Bukoba, JPM aliahirisha ziara ya Zambia tukitegemea angeibukia Bukoba lakini kilichotokea tukabaki kuulizana Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, "Sema Neno Moja Tuu, na Roho Zetu Zitapona!"

Mungu inusuru Hanang,
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Unajua Wakazi wa Katesh Ndio hpo Wataturu na Wabarabaig unawasifia na Ndio wamekufa!
 
Mi nadhani tuwahoji wachungaji na manabii wetu kwanini hili hawakuliona likija wala kuhisi dalili. Si wanatupanga mitaani kuwa na uwezo hadi wa kufufua mama zao wakifa! Au nao ni ma misheni town tu na wapiga hela kama hustlers wengine mtaani?
 
Katika makabila ulotaja wasandawe wana mfumo wao wa kutabiri hali ya mvua na ukame kabla ya msimu wa mva kuanza.wao hasa huangalia shape na position ya mwezi kuanzi mwezi wa pili na watatu kuna namna huongali ukubwa,shape bending ya mwezi wanajua msimu unaokuja hali ya mva itakuwaje wajiandae vp kuukabili hasa upande wa vyakula kwasababu kwa jiographia ya kule ni ngumu sana mafuriko kutoke labda miaka ijayo baada ya kukamilika bwawa la maji
Kila kabila hasa wakulima wana namna yao ya kuangalia nyita, mwezi na jua kwa ajili ya kutabiri hali ya majira ya mvua itakavyokuwa.

Kwa maeneo ya Singida na Manyara upande wa Katesh pia Mlima Hanang huwapa oahara na dalili ya mvua hasa radi zile za awali kabla mvua haziajaanza
 
Back
Top Bottom