Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa huja na kwa Maslahi ya Taifa. Leo ni kuhusu Natural Disasters: Jee Tuwafanyie Research watu wa makabila ya Wabarbaig, Wahadzabe, Wataturu, Wasandawe na Watindinga, huwa wanajuaje kutatokea natural disasters na kukimbia eneo hilo kabla ya majanga hayajatokea?
Japo wazungu wanasemekana ni wataalamu sana wa sayansi lakini hawawezi ku detect tetemeko la ardhi kabla halijatokea, au mlipuko wa volcano, lakini wanyama wa porini wana uwezo wa kudetect na makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo!
Mlima Katesh unasemekana una volcano hai, ulipofuka moshi mzito, na majivu yale yaliwaathiri wanyama na mifugo, ya kufungwa ndio iliathirika kutokana na kufungiwa lakini wanyama wa porini wao walijua na walikimbia kabla.
Watu wa makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo kwa kuwasikia wanyama pori, wakiwaona wanakimbia kukimbilia direction fulani, nao hukimbia, na baada ya kukimbia ndipo huku nyuma, hutokea la kutokea.
Tusiwategemee sana Wazungu na research zao, na vifaa vyao, tufanye utafiti wa haya makabila ya wawindaji wa asili wanatumia nini na viashiria gani kuyakimbia maeneo kabla majanga hayajatokea!.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wanasema walisikia mlipuko kama wa volcano usiku wa manane na hali kama ya tetemeko la ardhi, ndipo ikanyesha mvua kubwa mlima Katesh na kusababisha maporomoko ya udongo yaliyosombwa na mafuriko na kuzisomba nyumba za wakazi wa chini ya mlima ambapo watu zaidi ya 50 wamefariki dunia, mamia kujeruhiwa na mamia wengine hawana makazi wala mahali pa kuishi.
Mashuhuda hao wamesema mpaka kunakucha walikuwa wanaona mvuke ukipaa juu kutoka mlima Katesh.
Ikifanywa research ya waathirika wa janga hili la mafuriko ya Mlima Katesh unaweza kukuta, wale wanaioshi milimani na wanyama wa porini waliisha kimbia usiku usiku kabla ya janga hilo!
Na kufuatia imani za kiasili, (siiti za kishirikina), kuna watu wana nguvu na uwezo wa ajabu ama kusababisha majanga ama ku control majanga. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alikuwa akiwapiga maadui zake kwa mvua ya mawe na kumrarua kiongozi wao kwa kumpiga radi.
Kuna watu wanapaa usiku kwa ungo, kuna watu wanapanda fisi anapaa hewani, kuna watu wanatumia nyoka kulinda mashamba yao, kuna watu wanatumia mazindiko fulani, ukiingia kuiba, unamangamanga mpaka asubuhi unakutwa.
Hizi zote ni sayasi za kiasili za Kiafrika, zikifanyiwa research, zitalisaidia sana taifa letu. Mnaonaje kama tutafanya research kwenye hili?
Natoa tena pole kwa wahanga wa janga hili na nimemsikia Mama, amekatisha ziara ya Dubai kurejea nyumbani kuimarisha juhudi za uokozi na utengemano.
Enzi za JPM kulipotokea Tetemeko la ardhi Bukoba, aliahirisha ziara ya Zambia tukitegemea angeibukia Bukoba lakini kilichotokea tukabaki kuulizana.
Mungu inusuru Katesh, Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.