Majanga ya Asili: Tukafanye utafiti kwa Wahadzabe na wanaofanana nao ili tufahamu jinsi wanavyotambua majanga haya kabla hayajatokea?

Majanga ya Asili: Tukafanye utafiti kwa Wahadzabe na wanaofanana nao ili tufahamu jinsi wanavyotambua majanga haya kabla hayajatokea?

Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na kwa Maslahi ya Taifa. Leo ni kuhusu Natural Disasters: Jee Tuwafanyie Research watu wa makabila ya Wabarbaig, Wahadzabe, Wataturu, Wasandawe na Watindinga, huwa wanajuaje kutatokea natural disasters na kukimbia eneo hilo kabla ya majanga hayajatokea?

Japo wazungu wanasemekana ni wataalamu sana wa sayansi lakini hawawezi ku detect tetemeko la ardhi kabla halijatokea, au mlipuko wa volcano, lakini wanyama wa porini wana uwezo wa kudetect na makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo!

Mlima Katesh unasemekana una volcano hai, ulipofuka moshi mzito, na majivu yale yaliwaathiri wanyama na mifugo, ya kufungwa ndio iliathirika kutokana na kufungiwa lakini wanyama wa porini wao walijua na walikimbia kabla.

Watu wa makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo kwa kuwasikia wanyama pori, wakiwaona wanakimbia kukimbilia direction fulani, nao hukimbia, na baada ya kukimbia ndipo huku nyuma, hutokea la kutokea.

Tusiwategemee sana Wazungu na research zao, na vifaa vyao, tufanye utafiti wa haya makabila ya wawindaji wa asili wanatumia nini na viashiria gani kuyakimbia maeneo kabla majanga hayajatokea!.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wanasema walisikia mlipuko kama wa volcano usiku wa manane na hali kama ya tetemeko la ardhi, ndipo ikanyesha mvua kubwa mlima Katesh na kusababisha maporomoko ya udongo yaliyosombwa na mafuriko na kuzisomba nyumba za wakazi wa chini ya mlima ambapo watu zaidi ya 50 wamefariki dunia, mamia kujeruhiwa na mamia wengine hawana makazi wala mahali pa kuishi.

Mashuhuda hao wamesema mpaka kunakucha walikuwa wanaona mvuke ukipaa juu kutoka mlima Katesh.

Ikifanywa research ya waathirika wa janga hili la mafuriko ya Mlima Katesh unaweza kukuta, wale wanaioshi milimani na wanyama wa porini waliisha kimbia usiku usiku kabla ya janga hilo!

Na kufuatia imani za kiasili, (siiti za kishirikina), kuna watu wana nguvu na uwezo wa ajabu ama kusababisha majanga ama ku control majanga. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alikuwa akiwapiga maadui zake kwa mvua ya mawe na kumrarua kiongozi wao kwa kumpiga radi.

Kuna watu wanapaa usiku kwa ungo, kuna watu wanapanda fisi anapaa hewani, kuna watu wanatumia nyoka kulinda mashamba yao, kuna watu wanatumia mazindiko fulani, ukiingia kuiba, unamangamanga mpaka asubuhi unakutwa.

Hizi zote ni sayasi za kiasili za Kiafrika, zikifanyiwa research, zitalisaidia sana taifa letu. Mnaonaje kama tutafanya research kwenye hili?

Natoa tena pole kwa wahanga wa janga hili na nimemsikia Mama, amekatisha ziara ya Dubai kurejea nyumbani kuimarisha juhudi za uokozi na utengemano.

Enzi za JPM kulipotokea Tetemeko la ardhi Bukoba, aliahirisha ziara ya Zambia tukitegemea angeibukia Bukoba lakini kilichotokea tukabaki kuulizana.

Mungu inusuru Katesh, Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Ha ha ha!

Ukweli ni kwamba hakuna kitu cha Kiasili ambacho hakijawekwa Scientifically siku hizi!

Kila kitu kiko Studied na kuwa Scientific approved!

Of course-Kuna Primitive Science ambayo Economically Hailipi!

Kama kupanda fisi in liu to Human Blood...haina maana...bora fossil fuel.

Halafu siyo kweli kwamba Wazungu hawawezi kutabiri Earthquakes na Majanga mengineyo..

Hurricane Catrina waliweza kuiona few Hours kabla ya kutokea na America na Ujerumani waliokoa watu wake wengi sana!

Kwa vivo Lets go for Science na hapa ndo maana unaona Mataifa Makubwa yanarusha Satellite nyingi huko Angani.

Kila Satellite ina kazi yake...!
 
Kilimanjaro,monduli, meru,usambara,pare,udzungwa
Milima yote hii ni dormant
Kilichotoea hanang inaweza tokea
Pia kwa milima hii
Sasa sijui wataalam wetu wajipangaje
Kwa huko ya mbeleni?

Ova
 
Tatizo nyie wanadam mnajifanya wajuaji sana ,mnataka kupingana na nature

Ova
Halafu kuna watu 'wataalamu wa mipango ya makazi' wanazurura na vitembea kazi vya dude linaloitwa serikali, wanaruhusu na kufumbia macho uibukaji wa makazi ya kiholela kwenye sehemu zisizofaa ... iwe milimani au mabondeni ambapo mafuriko na landslides hupendelea sana kuibukia! Tahadhari ni gharama nafuu kuliko tiba kamili. Nchi yetu hiyo! 😡
 
1. Kwa case ya wanyama: kama ambavyo Mungu (nature) ame(ime)mzawadia mwanadamu ubongo wenye uwezo mkubwa, basi ame(ime)wazawadia wanyama uwezo mkubwa katika Milango ya fahamu kuliko hata mwandamu hasa mlango wa fahamu wa kunusa na mlango wa fahamu wa kusikia.
Kabla janga lolote la asili kutokea, kunakuwa na ishara za chini chini ambazo mwanadamu hawezi Ku detect. Kunakuwa na mabadiliko ya harufu ya hewa ya eneo.
Mfano kwa tetemeko, kunakuwa na mitetemo ya chini sana ambayo ndege, wanyama jamii ya Paka(Panthera Leos) wanasikia.
Sasa wakikisikia, basi kuhama kunaanza na hivyo hata wanyama wengine huiga wanapoona wenzao wanachama.
Mvua kubwa ina harufu yake, upepo mkali una harufu na mitetemo yake, volcano ina harufu yake ya kabla na mitetemo yake ya kabla(pre-condition).
Tetemeko la ardhi lina mitetemo midogo midogo ya kabla. Lina harufu yake ya kabla.
2. Kwa case ya hayo makabila, wao kwa sehemu kubwa bado wanategemea uasili. Husoma tabia za wanyama, ndege na miti. Wakiona mabadiliko fulani ya kuhama kwa wanyama, sauti ya wanyama na ndege, miti na udongo, basi nao hu detect jambo zuri au baya.
Pia hutumia uzoefu wa miaka mingi ambayo hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Experience is the best teacher.
Hata kijijini kwetu:
1. Kuna ndege wakionekana tunajua kabisa mwaka huu masika yatakuwa mwake mwake, murua, bam bam!
2. Kuna mimea(nyasi na majani) ikionekana tunajua kabisa mvua za kutosha zitakuwepo.
3. Kuna wanyama pori tukiona wakikatiza tunajua mwaka huu ukame utatukomesha. Mfano unashangaa tu nyumbu au swala au pundamilia wanapita kijijini wakihama, hofu yake ni balaa. Inakatisha tamaa.
4. Kuna wadudu kama vile vipepeo, kumbi kumbi, panzi, nzige wanakuwa na jumbe mbali mbali wanapokuwepo kwa wingi kijijini kwetu.
5. Madume kuacha Kupanda ng'ombe hata kama wanashiba vizuri, kuna ujumbe hasa wa baa la ukame, kuchelewa kwa mvua, magonjwa ya mlipuko kwa ng'ombe.
6. Afya ya mifugo kugoma, hata uwape nini, uchome sindano gani, ujue hapo hali ya hewa imegoma na imebadilika juu kwa juu.
 
Utakuwa Muikolojia....

Wasalimie huko TANAPA na National Herbarium TPRI
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na kwa Maslahi ya Taifa. Leo ni kuhusu Natural Disasters: Jee Tuwafanyie Research watu wa makabila ya Wabarbaig, Wahadzabe, Wataturu, Wasandawe na Watindinga, huwa wanajuaje kutatokea natural disasters na kukimbia eneo hilo kabla ya majanga hayajatokea?

Japo wazungu wanasemekana ni wataalamu sana wa sayansi lakini hawawezi ku detect tetemeko la ardhi kabla halijatokea, au mlipuko wa volcano, lakini wanyama wa porini wana uwezo wa kudetect na makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo!

Mlima Hanang uko kwenye safu ya milima ya volcanic mountains kama Oldonyo Lengai, usikute una volcano hai!. Enzi zile Oldonyo Lengai, ulipofuka moshi mzito, na majivu yale yaliwaathiri wanyama na mifugo, ya kufungwa ndio iliathirika kutokana na kufungiwa lakini wanyama wa porini wao walijua na walikimbia kabla.

Watu wa makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana natural seismology intelligence hivyo wana uwezo huo kwa kuwasikia wanyama pori, wakiwaona wanakimbia kukimbilia direction fulani, nao hukimbia, na baada ya kukimbia ndipo huku nyuma, hutokea la kutokea.

Tusiwategemee sana Wazungu na research zao, na vifaa vyao, tufanye utafiti wa haya makabila ya wawindaji wa asili wanatumia nini na viashiria gani kuyakimbia maeneo kabla majanga hayajatokea!.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wanasema walisikia mlipuko kama wa volcano usiku wa manane na hali kama ya tetemeko la ardhi, ndipo ikanyesha mvua kubwa mlima Katesh na kusababisha maporomoko ya udongo yaliyosombwa na mafuriko na kuzisomba nyumba za wakazi wa chini ya mlima ambapo watu zaidi ya 50 wamefariki dunia, mamia kujeruhiwa na mamia wengine hawana makazi wala mahali pa kuishi.

Mashuhuda hao wamesema mpaka kunakucha walikuwa wanaona mvuke ukipaa juu kutoka mlima Hanang.

Ikifanywa research ya waathirika wa janga hili la mafuriko ya Mlima Katesh unaweza kukuta, wale wanaioshi milimani na wanyama wa porini waliisha kimbia usiku usiku kabla ya janga hilo!

Na kufuatia imani za kiasili, (siiti za kishirikina), kuna watu wana nguvu na uwezo wa ajabu ama kusababisha majanga ama ku control majanga. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alikuwa akiwapiga maadui zake kwa mvua ya mawe na kumrarua kiongozi wao kwa kumpiga radi.

Kuna watu wanapaa usiku kwa ungo, kuna watu wanapanda fisi anapaa hewani, kuna watu wanatumia nyoka kulinda mashamba yao, kuna watu wanatumia mazindiko fulani, ukiingia kuiba, unamangamanga mpaka asubuhi unakutwa.

Hizi zote ni sayasi za kiasili za Kiafrika, zikifanyiwa research, zitalisaidia sana taifa letu. Mnaonaje kama tutafanya research kwenye hili?

Natoa tena pole kwa wahanga wa janga hili na nimemsikia Mama, amekatisha ziara ya Dubai kurejea nyumbani kuimarisha juhudi za uokozi na utengemano.

Enzi za JPM kulipotokea Tetemeko la ardhi Bukoba, JPM aliahirisha ziara ya Zambia tukitegemea angeibukia Bukoba lakini kilichotokea tukabaki kuulizana Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, "Sema Neno Moja Tuu, na Roho Zetu Zitapona!"

Mungu inusuru Hanang,
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Wabarbaig wepi unawazungumzia, Pale Hanang ndio kwao na ndio hao wamekufa na kaya zaidi ya 28 hazijulikani zilipo, bila shaka wamefukiwa na matope. Hali ya Hanang ni mbaya kuliko viongozi wanavyoeleza. Vitongozi vitatu vimefukiwa. Nenda kaangalie kwenye ripoti ya sensa ya mwaka jana 2022, kaangalie kijiji cha Gendabi ina watu wangapi. Watu ambao wamefukiwa ni wengi sana.
 
Usambara nayo inasemekana
Ni dormant....
Huko nimepanda sana miti nikiwa na jamaa wa friends of usamabara
(Member)
Huo mlima nimeuzunguka karibia sehemu kubwa

Ova
Mlima Usambara ni upi?? hakuna Mlima Usambara. KUna Usambara ranges of Miuntains. Kuanzia Same hadi Korogwe to Mkinga (Maramba) yote ni Usambara. Kuna Usambara magharibi ambayo ni Milima ya Upande wa Same na Usambara Mashariki ambayo ni Lushoto, Korogwe, Muheza (Amani) hadi Mkinga, Tanga. Ni safu za Milima kama ilivyo milima ya Himala. Maarufu milima Mikunjo.
 
Back
Top Bottom