Majanga yanayoikumba Dunia, chanzo adhabu Toka Kwa Mungu, tugeuke na kutubu

Vita zinazoendelea duniani na maelfu wanakufa, hiyo neema Iko wapi inayoongezeka?

Wakristo walioko Kongo, Israeli Kila siku wananusurika kuripuka na mabomu, hao wako nyakati zipi?

Nyakati tulizopo ndizo hizo zimeandikwa Mt 24 na Ufunuo,

Usilolijua, MUHURI wa nne umefunguliwa, Malaika aliyepanda farasi wa kijivu ndiye ameruhusiwa kuua theluthi ya watu duniani.
 
Mlima wa maombi hauporomoki, Si mlima halisi kama unavyoshani, ni something spiritual.
Ok. Najua hilo mwalimu wa neno kwa watoto.
Ila nikushauri tu kama mtu ulieona nuru ya kristo. Jaa upendo. Usihukumu, nazani unakumbuka tulipopishana ukanishushia hukumu.
 
Wewe huijui Injili hivi unazijua vita wewe?
Yaani hayo maigizo ya kisiasa unaita vita?
Hivi Kati ya Dunia ya kale na leo wapi kumepiganwa vita zaidi?
Kingine hakuna Malaika aliyetumwa kuua watu katika Agano jipya kiufupi huo Ufunuo wa Yohana ulishatimizwa miaka zaidi ya 2000 iliyopita kijana!
 
Ni mwalimu wa watoto bado hajakomaa kuchambua neno.
Si unajua wagoto hula chakula gani? Maziwa.
 
Wakristo wa kongo wanakufa kwa sababu ya ujinga wao na kutotambua nafasi zao,
Hata Wakristo wa bongo wanaburuzwa na CCM sababu ya kutojitambua kama wewe hapo,
Kumbuka ukiwa Mkristo ni Kristo anaishi ndani yako na utaishi maisha ya miujiza ila kwa sababu ya ujinga na kutojitambua utaendelea kuburuzwa na Ibilisi kwa kutojitambua hivi Mkristo unaongozwa na Roho Mtakatifu nani atakua juu yako?
Wewe jamaa hujui Injili ni nini!
 
Nyie nao hamna akili, mamikaa mnayoyakata na kuchoma kila siku na mashamba mnayoyasafisha ili mlime mnategemea nini kama sio tabia za nchi kuwa na changes..??
Dhambi sio sababu ya changes ya hali ya hewa.
 
Kwamba wakristo wa Kongo wanakufa Kwa Ujinga wao?

Nani aliyekusimamia ukuaji wako kiimani na kimafundisho?
 
Weka namba za simu tutoe sadaka
 
Ni mwalimu wa watoto bado hajakomaa kuchambua neno.
Si unajua wagoto hula chakula gani? Maziwa.
True bado mtoto mdogo!
(In TID voices)

Hailewi maana ya ufalme wa Mungu ni nini
Yaani mtu unaomba ile sala ya Baba yetu uliye Mbinguni Jina lako litukuzwe,ufalme wako uje,Mapenzi yako yatimizwe hapa Duniani kama huko Mbinguni'

Hii sala inajieleza kwamba ufalme wa Mungu uje na Dunia ifananie Mbinguni yaani Mungu afanye mambo yale yale ya Mbinguni hapa hapa Duniani just imagine Taifa la Marekani litupe bajeti kama yao kama msaada kila Mwaka ili tulingane nao si tutakua Marekani ya Africa?
Ndio maana ya hio Sara
God kingdom in Earth!
 
Reactions: 511
Kumbe na Ulimwengu ulioandikwa utachomwa moto, ni hapo Israel pekee?
BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Mwa 8:21‭-‬22 SUV

Mkuu hakikisha unasoma bible yako vizuri, hiyo dunia itakayochomwa moto ni ipi
 
Huyu jamaa na mwingine anajiita "Yesu anarudi" niliwachallenge kwa thread zao tofauti. Wakashindwa kunijibu hoja wakaniita shetani, eti wanashuhudiwa kabisa kuwa wanaongea na mtu asie na Mungu.

Sasa mtu asie na Mungu anakuletea andiko wewe mwenye Mungu unashindwa kulifafanua. Nani hapo anakuwa hana Mungu.

Nilichogundua walokole wengi hawajui neno. Wao wanajua tu kushika verses za bible lakini sio kuchambua neno. Wanatumia ule msemo "there are only two rules: one, the boss is always right and two if the boss is wrong look rule one"

Mtu kama huyo ukimuuliza unabii aliotoa Yakobo kwa mwanae Gadi ulitimia wapi mwenye bible ataleta siasa, but ulitimia baada ya miaka mingi tu.
 
Mbona Kama unawawekea watu hofu kuwa utakufa kwani wewe utaishi milele. Yaani mnaishi kwa kuwapa watu uwoga , haya Mungu aliyajua kabla hata hajaumba ulimwengu. Na alisema hakika mtakufa.
Ongea kawaida kuwa inabidi tumche na tumnyenyekee na kumuomba Mola wetu bila ya kuweka vitisho.
Unakifanya unayajua ya kesho ama yaliyotokea. Unatumia hindsight bias analysis yaani kitu kimeshatokea ndio unajaribu kuweka mawazo yako ili yaendane m na tukioa lililotokea.
Mbona hukuyaongea kabla hayajatokea.

Kufa kupo Kama kuzaliwa kulivyo.

Huwezi jua mipango ya aliyeiumba dunia na mawazo yake sio Kama ya kwako
 
Kwamba wakristo wa Kongo wanakufa Kwa Ujinga wao?

Nani aliyekusimamia ukuaji wako kiimani na kimafundisho?
Wakristo wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa sababu wanaacha kusimamia Neno linasema wanatoka Neno ndio lifananie na wanachotaka,

Kingine sina anayenisimamia zaidi ya Neno na Roho Mtakatifu,
Nasema kile Neno limesema na nafanya kile Roho Mtakatifu amenipa kufanya nothing more
Kama wewe una mtu anakusimamia nakupa pole sana maana umapatwa na tabu ya namna yote hiyo kufuata mafundisho manyonge yawafaayo watoto wadogo ila kama unataka maisha yako yamfananie Kristo huna budi kuanza kuchukua hatua as a personal na utapata matokeo ya kiungu karibu kwa ufafanuzi zaidi ndugu Rabbon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…