Nasikitika hii taarifa nimechelewa kuipata, lkn naamini bado sipo nje sana ya uzi.
Hii habari haijakaa sawa kabisa, na kama ni kweli basi ni jambo la kusikitisha sana.
Hii ishu inanikumbusha skendo ya 'Pizza hut' ambapo majasusi 12 wa CIA walikamatwa na makachero wa Iran and Hezbollah wakiwa Pizza Hut, Beirut ambapo walikua wanadukua taarifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Kilichofuata CIA, POTUS, Waziri wa ulinzi na usalama, Ashton pamoja na waziri wa mambo ya nje John Kerry wote waliwakana hao majasusi wa CIA. Alichokifanya Iran ni kuwa Execute (kunyongwa), tena pasipo huruma.
Vyombo vya usalama vifuatilie kwa ukaribu swala hili, serikali isijitie 'Hapa Kazi Tu' tutawapoteza hao wenzetu. Cha msingi meza ivutwe, iwekwe mauwa ya urembo, korosho na maji, mazungumzo ya kidiplomasia yafuate. Tuna hazina nzuri kama Dr. J. M Kikwete, Waziri mkuu mstaafu E. Lowassa. Peter wa Mutharika si adui yetu, ni mtu safi sana, anaweza kutuelewa. Let's get a way to settle this down kabla hatujawapoteza.