Majasusi wabobezi 8 wa Kitanzania wakamatwa nchini Malawi

Majasusi wabobezi 8 wa Kitanzania wakamatwa nchini Malawi

[QUOTE="isukare, post: 19048323, member: 390958"[/QUOTE]

I put you as a grist to the mill.
 
Mkuu nimependa huu mchango wako hadi natamani nikufahamu tu nikupe Zawadi. Laiti baadhi yetu humu JF tungekuwa na IQ hii nzuri na iliyotukuka ya huyu Jamaa wengine wala tusingepata taabu kuwafundisha Watu jinsi ya kufikiri na kujenga hoja. Mkuu nimekukubali mno na nakubalina na ulichokiandika kwa 100%. Tunaoijua nchi ilipotoka, ilipokuwa na inapoenda tumekuelewa mno na akhsante kwa kufunguka Kiume kabisa huku ukisema ukweli ambao naamini utakuwa mchungu kwa wahusika. Kula like yangu tafadhali!
Asante mkuu uchungu wakuzaliwa kwenye hii nchi tumebakia nao watanzania wachache sana nakupongeza pia kwa ujasiri wa kuleta hii mada hapa jukwaani,tuukatae unafiki wa wacache wanao taka kuhodhi hii nchi kwa kutugawa katika kila nyanja,msimamo wa baba wataifa na mapungufu yake yote tunge ukubali na kuacha kumuenzi kinafiki tungekuwa mbali sana kimaendeleo kama wenzetu wa uchina lakini tumekataa ukweli na kufata uongo tunaoupenda!! Tuko pamoja mkuu
 
Mawazo yameheshimiwa Mkuu, ila kuna kitu lazima ujifunze mambo Haya kiundani sana, weakness yako kubwa ni Ku JUDGE haraka bila kuwa na ushahidi wa kina.

Tafuta kuna Uzi uko humu toka jana angalau aliyeuleta alileta habari yote ilivyoandikwa.

Wewe unachokifanya hapa ni kuleta Propaganda dhidi ya TISS ilhali kipaumbele hapa ni utaifa kwanza.

Huwezi kuthibitisha kuwa waliokamatwa ni Majajusi wakati hata kule Malawi hawajathibitisha kupitia vyombo rasmi ila wewe hapa ushathibitsha na kuanza kutoa hukumu.

Halafu kwa Elimu ndogo tu ni kuwa mara nyingi Agents wanapokamatwa huwa hawatoi habari hovyo hovyo,

Mfano Leo Tanzania ikamate Agents wa Malawi halafu OCD wa Tunduma ndio atoe taarifa kwa umma.

You must be an Intelligent in this things
Mkuu upo vizuri sana. Big up [emoji1]
 
Kazi imeanza haya wenye Kazi zenu hizi za Kijasusi ambao najua mpo wengi mno humu JF na mmejazana hebu tupeni ukweli wa hii taarifa ya Serikali ya nchini Malawi kuwa imewakamata Majasusi wanane ( 8 ) wa Kitanzania wakiwa wanafanya Ujasusi wao.
View attachment 450785
Source: Gazeti la The Citizen la leo tarehe 27, December 2016 tena ipo front page kabisa.

Je tunaweza pia kuwajua hao Watanzania Majasusi waliokamatwa kwani yawezekana kuna wengine ni Wategemezi wetu wa Kimaisha.

Nawasilisha.
Jamani acheni hizi porojo kwa kweli; mtu akitaka kufanya ujasuri maeneo kama hayo haiwezekani kufanya hivi. Kama ni kweli ni majasusi wanahitaji kufukuzwa!
 
Niulize tu, tukijua wanatengeneza tunafanyaje? Au na sisi tutatengeneza au kuwashitaki??
Nimejiuliza sana hili swali, but till now nahang tuu bila jibu, emb kina nanihiii mtusaidie hapa
 
Usisumbuke nao Mkuu unaweza ukadhani hao ni Watu tofauti tofauti wanatiririka na hicho Kifaransa chao ila nikuhakikishie tu kuwa huyo ni Mtu mmoja. JF ni zaidi ya uijuavyo Mkuu!
Au ndo wameanza course wako wanapractise ,waache wanafunzi hawa!!!
 
Sio rahisi hivyo makomambo kukamatwa kijinga ivo especially watanzania,hizo ni propaganda za Malawi,kanchi kenyewe kama Dar es salaam Kwa ukubwa
Israel inaukubwa gani??mbona inawatesa waarabu wote wa asia
 
Israel inaukubwa gani??mbona inawatesa waarabu wote wa asia

Mkuu hao ndiyo Wasomi wa Tanzania ambao kuna Professor mmoja aliwahi kusema usomi wao wala hauna tija na sana sana tu unaongeza tu idadi ya Wapumbavu duniani. Umemjibu vizuri mno na kumdhalilisha kwa kuonyesha ni jinsi gani asivyojua kufikiri. Nani aliyewaambieni kuwa ukubwa wa nchi ndiyo uhalali wake kushinda vita? Rwanda kwa mfano ni nchi ndogo sana lakini ilitupelekesha hadi ikabidi sasa Mkemia wa Kale alipoingia tu Magogoni aombe suluhu nayo Kidiplomasia ndiyo itashindwa Malawi kutuchapa? Rudini tena darasani mkajifunze upya mbinu za Medani za Kivita.

Mkuu nimekukubali sana na sina shaka na IQ yako kwani inaonyesha kuwa imetukuka kisawasawa. Kula tena like yangu tafadhali.
 
Back
Top Bottom