GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #161
Malawi wanaitamani Tanzania wanapewa kichwa sana sijui na nani! Chokochoko tangu mdaaa
Kuna vita kubwa ya Kimaslahi na ambayo inahusisha Super Powers watatu na ndiyo chanzo cha haya yote Mkuu. Malawi wanapewa Kiburi na Jeuri na Marekani na Ujerumani huku wao wakichukizwa na Kitendo cha Tanzania kuwakumbatia sana Wachina katika Sekta mbalimbali hasa za Kiuchumi kitu ambacho kimewaudhi mno kwani hata Wao walitamani mno kupewa nafasi ya kutoa msaada wao wa kutuwezesha Watanzania kuitumia Uraniam yetu lakini walipogundua tu kuwa sisi Kipaumbele chetu ni kwa Wachina sasa wanapenyeza chuki zao dhidi yetu Tanzania indirectly kabisa kupitia Malawi na taasisi zake Nyeti.
Na usisahau juzi kati tena hapa nchi ya Urusi nayo ilionyesha nia ya kuitumia Uranium yetu iliyogundulika kitendo ambacho kinaweza kuwaweka Strategical Friends China na Urusi pamoja kitu ambacho kitawaathiri sana Marafiki wakuu wa Ulaya Marekani na Wajerumani hasa Kiuchumi.
Naomba niishie hapa na niwaachie wengine nao waweze kutiririka Mkuu.