Majasusi wabobezi 8 wa Kitanzania wakamatwa nchini Malawi

Majasusi wabobezi 8 wa Kitanzania wakamatwa nchini Malawi

malawi kuna watz wengi sana waliokaa kule miaka mingi. pia kuna wamalawi wengi mno mwambao mwa ziwa wenye mlengo wa kibongo kwasababu huwa wanaamini wanabaguliwa. jamaa wanaamini unaweza kuvamia kinu cha nukes mikono mitupu, bila vikinga athari, bila silaha, na mmeongozana kama bata..tena mchana..hahaha. tusidharau nchi yetu namna hiyo. hao malawi wametafuta tu kitu cha kuzusha ili kuiweka dunia ijue mgogoro uliopo. ni kweli malawi na mozambique kuna watz wengi sana wachimbaji wadogowadogo wa madini, si ajabu hao jamaa walikuwa wanaamini pale wataokota kitu, au hawa hawajakuwepo pale ila wamekamatwa kupelekwa pale kuambiwa wamekuwepo pale kimakosa ili kufanya sababu tu ya mzozo wa maneno(kwani wa vitendo malawi wanaiogopa tz mno). kwahiyo, ujumbe waliokuwa wameutarajia hadi sasa umeshasambaa, kazi yao imetimia. wamewaacha wabongo wanajadili tiss 8 kukamatwa mchana karibu na kinu cha nuke malawi...hahaha, hata mtu ambaye hajapitia tiss hawezi fanya uzembe wa aina hiyo.
Siku hizi technology jinsi ilivyo unaweza zoom ilo eneo hata ukiwa umbali wa km 50 ukapekua kila kitu unachokitaka na ukaonfoka.....

Kwanza wangekuwa wamewakamata watu wetu kweli taarifa isingetoka na kuvuja kirahisi hivyo maana na wao wanaogopa reaction yetu pia.....

Hata Mimi sizani kama TISS wanaweza Fanya uzembe kiasi hicho .....

Hii habari itakuwa imetengenezwa....
 
Kuna vita kubwa ya Kimaslahi na ambayo inahusisha Super Powers watatu na ndiyo chanzo cha haya yote Mkuu. Malawi wanapewa Kiburi na Jeuri na Marekani na Ujerumani huku wao wakichukizwa na Kitendo cha Tanzania kuwakumbatia sana Wachina katika Sekta mbalimbali hasa za Kiuchumi kitu ambacho kimewaudhi mno kwani hata Wao walitamani mno kupewa nafasi ya kutoa msaada wao wa kutuwezesha Watanzania kuitumia Uraniam yetu lakini walipogundua tu kuwa sisi Kipaumbele chetu ni kwa Wachina sasa wanapenyeza chuki zao dhidi yetu Tanzania indirectly kabisa kupitia Malawi na taasisi zake Nyeti.

Na usisahau juzi kati tena hapa nchi ya Urusi nayo ilionyesha nia ya kuitumia Uranium yetu iliyogundulika kitendo ambacho kinaweza kuwaweka Strategical Friends China na Urusi pamoja kitu ambacho kitawaathiri sana Marafiki wakuu wa Ulaya Marekani na Wajerumani hasa Kiuchumi.

Naomba niishie hapa na niwaachie wengine nao waweze kutiririka Mkuu.
Umemsahahu mwingereza na kaburu
 
ukifika mazingira kama hayo, ndipo utajiuliza kwanini vikundi vingine vinakuwa masikini lakini vinakuwa na silaha nzito kupigana na serikali, ni kwasababu kuna mkubwa mmoja mwenye maslahi anasupply. katika hili tz inabidi tuwe makini...tuboreshe tiss yetu na tuwe makini katika uchaguzi wa rafiki. lazima tuforesee. historia inaonyesha hakuna aliyewakumbatia russia na china akaishia pazuri. syria ni mfano tosha. ila kwa wote waliokuwa pro westerners mwisho wao huwa ni mzuri. mfano ni kenya na nchi zingine za kibepari africa. hivyo, kama ikiwezekana, tuwapige tu chini wachina na warusi tujiunge na waulaya magaribi, na kama urusi na china watang'ang'ania kutugana, basi welete dau la kueleweka litakalofuta machozi zote ya usumbufu na vita baridi. la sivyo, piga chini twenzetu kwa wamagaribi.
Tatizo siyo kuchagua upande. Tatizo ni VIGEZO NA MASHARTI ya kila upande.

Wapo watakaokutaka uhalalishe ushoga ......
 
Kwan Tanzania kuna majasus?Wa nn labda mm naona wazamiaj wapigwe Tu nchi haina mvua munaongelea ujasus!?aliyeturoga alikufa
 
Msiwe na shaka hawa wantabia ya kutuchokoza. Muda ukifika serikali itatoa taarifa. Hawa wajinga wa MALAWI wanapenda kusumbua utulivu wa akili ZETU.
TANZANIA TUPO MAKINI NA NAAMINI HAKUNA UPUMBAFU WANAWEZA KUTUFANYIA HAWA VIUMBE. KUWENI NA AMANI NA MUENDELEE KUCHAPA KAZI. JIONI NJEMA
 
Nasikitika hii taarifa nimechelewa kuipata, lkn naamini bado sipo nje sana ya uzi.

Hii habari haijakaa sawa kabisa, na kama ni kweli basi ni jambo la kusikitisha sana.

Hii ishu inanikumbusha skendo ya 'Pizza hut' ambapo majasusi 12 wa CIA walikamatwa na makachero wa Iran and Hezbollah wakiwa Pizza Hut, Beirut ambapo walikua wanadukua taarifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Kilichofuata CIA, POTUS, Waziri wa ulinzi na usalama, Ashton pamoja na waziri wa mambo ya nje John Kerry wote waliwakana hao majasusi wa CIA. Alichokifanya Iran ni kuwa Execute (kunyongwa), tena pasipo huruma.

Vyombo vya usalama vifuatilie kwa ukaribu swala hili, serikali isijitie 'Hapa Kazi Tu' tutawapoteza hao wenzetu. Cha msingi meza ivutwe, iwekwe mauwa ya urembo, korosho na maji, mazungumzo ya kidiplomasia yafuate. Tuna hazina nzuri kama Dr. J. M Kikwete, Waziri mkuu mstaafu E. Lowassa. Peter wa Mutharika si adui yetu, ni mtu safi sana, anaweza kutuelewa. Let's get a way to settle this down kabla hatujawapoteza.
 
Majasusi kama nyumbu au kondoo wote wanakaa au kutembea pamoja au hata kuonekana tu wakizoeana? Kama ni wa kitanzania itabidi serikali ipitie upya uaandaaji wa hawa wasalama wake. Ni kushindwa kwa hali ya juu sana katika jicho la kiusalama. Revisit revisit revisit.....
Ukiwa hujuwi jambo kaa kimya usipende kujiandikia tu. Jaribu kushirikisha ubongo tafadhali. Usiandike upuuzi wa ivo. Unafikiri wewe unawaza zaidi ya watanzania wengine.? Jaribu kujadili kwa umakini mtanzania mwenzangu
 
Mimi naomba katika uzi huu niwe tu mtazamaji Wakuu zangu.
we mnyarwanda kiongozi shukuru hata unaishi kwa amani hapa,mambo ya tz hayakuhusu unaona kuna mapungufu rudi kwenu,hayo mambo yatashughulikiwa kidiplomasia na si lazima ujue wala ujulishwe hayakuhusu
 
Sio rahisi hivyo makomambo kukamatwa kijinga ivo especially watanzania,hizo ni propaganda za Malawi,kanchi kenyewe kama Dar es salaam Kwa ukubwa
 
Kazi imeanza haya wenye Kazi zenu hizi za Kijasusi ambao najua mpo wengi mno humu JF na mmejazana hebu tupeni ukweli wa hii taarifa ya Serikali ya nchini Malawi kuwa imewakamata Majasusi wanane ( 8 ) wa Kitanzania wakiwa wanafanya Ujasusi wao.
View attachment 450785
Source: Gazeti la The Citizen la leo tarehe 27, December 2016 tena ipo front page kabisa.

Je tunaweza pia kuwajua hao Watanzania Majasusi waliokamatwa kwani yawezekana kuna wengine ni Wategemezi wetu wa Kimaisha.

Nawasilisha.
Nani Atakupa Ukweli Wewe?? Naona Akili Yako Haifikiri Sawa Sawa. Unadhani Kuna Mwehu Ambaye atakuja hapa na kukupa ukweli? Mambo mengine yaache kama yalivyo. Angalia yako
 
Back
Top Bottom