Tetesi: Majasusi wamnyima Trump siri nyeti

Tetesi: Majasusi wamnyima Trump siri nyeti

Hawana ubavu wa kumnyima commander inchief habari
Wenzetu si kama hapa kwetu ambapo raid anaweza kufanya au kuongea chochote atakacho halafu idara au hata miimili yote ikakubaliana naye. Wenzetu kila sekta inafanya majukumu yake kwa weledi wake bila kuingiliwa. Angalia jinsi mahakama yao ilivyotengua mpango wa Rais wao juu ya suala la mataifa mengine kuingia Marekani jambo ambalo ingekuwa hapa Tanzania hakuna jaji yeyote ambaye atadhubutu kupingana na mipango au hata matamshi ya Rais hata kama yataonekana dhahiri kuwa na mapungufu ktk utekelezaji wake. Idara ya kijasusi ya Marekani haiwezi kuburutwa na yeyote badala yake kiongozi akikomaa kuchuana nayo chochote chaweza kumfika. Kwa mwanzo huu wa Trump kupishana nao sidhani kama iko siku tena watajampa uwazi was ujasusi wao hasa yanayohusiana na nchi zenye mahusiano na Urusi. Watakuwa wameshamwekea alama ya kuwa na wasiwasi naye kwani wao wanajali zaidi maslahi ya kiusalama wa Taifa zaidi na si maslahi ya chama au ya kiongozi yeyote bila kujali ukuu wake ndani ya nchi.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Mm hapo bado sijawaelewa elewa. kwamba trump hawata mpa taarifa za kijasusi za dunia nzima au za urusi tu?

Na kama hizo taarifa hawata mpa rais trump na je hizo taarifa watampa Nani harafu na rais asijue.
Wale taarifa zote muhimu wanaweza kukaa nazo wenyewe na zile ambazo zitakuwa zinahatarisha usalama wa nchi watazimega kwa jeshi ambalo nalo pia Rais hawezi kulikurupusha apendavyo.

Sent from my HUAWEI Y336-U02 using JamiiForums mobile app
 
Sijui mnapozungumzia jamii ya kijasusi mnazungumzia nini zipo zaidi ya Intelligence Agency 17 ndani ya US pia zipo zle zinajulikana kama "Big Five" (+1) kutokana na ukubwa wa majukumu yao na utendaji wao wa kazi kulinganisha na vyombo vingin ambazo ni FBI,CIA,Homeland Security,NSA na Secret Service lakini Intelligence Agency zote zikiwamo hizo
"Big Five" (+1) zote zinareport kwa Office of the Director of National Intelligence ambae office zake zipo Washington Fort Meade, Maryland , U.S. yalipo makao makuu ya NSA

Huyu DNI ( Director of National Intelligence) ndio mwenye security clearance kubwa na yeye ndio anakuwapo ktk kikao cha The President's Daily Brief (PDB) kinachofanyika kila siku saa 07:45 AM ambapo rais anapokea taarifa zote za kijasusi na mambo ya usalama na wanaohudhulia ktk kikao hicho ni Commander-in-chief, VP, Defense secretary na National security adviser so ni lazima Rais apate taarifa zote kila siku juu ya mambo ya ulinzi na Usalama

Kuna mdau hapa jabulani anasema CIA wanaweza kufanya kama walivyofanya kwa J.F Kennedy November 22, 1963
Dallas, Texas, U.S. mifumo ya sasa hivi ni ngumu sana narudia ni ngumu sana kwa Taasisi kufanya hvyo
Huyo DNI asipopewa taarifa zote atapeleka nini?
 
Majasusi wa kibongo bongo ndio hutoa ushirikiano kwa mkulululuu wa bongo
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida nchini Marekani. Jamii ya Kijasusi ya Marekani imeamua kumpa kwa vipimo ripoti za kijasusi Rais wa Marekani Donald Trump.

Habari zinasema kumekuwa na vita baridi kati ya Ikulu ya White house na jamii ya kijasusi ambayo Trump amekuwa akiilaumu hasa baada ya KUVUJA kwa maongezi ya Mteule wake na mshauri wake mkuu wa mambo ya usalama bwana Mike Flynn aliyelazimika kujiuzulu baada ya mazungumzo yake na balozi wa Urusi KUVUJWA hadharani.

Trump amekuwa akilaumu idara hizi kuwa ZINAVUNJA sheria kwa KUVUJISHA maksudi habari nyeti/classified za serikali kwa vyombo vya habari.

Pia jamii hii ya kijasusi imeanzisha uchunguzi dhidi ya baadhi ya wasaidizi wa Trump ambao nao huenda wamefanya ama wamekuwa wakifanya mawasiliano na maafisa wa Urusi.

Hili limemkasirisha Trump ni kama vile wanataka kumchafua ili aachie uongozi..

Nao maofisa wa kijasusi wanaogopa kumpa Trump SIRI ZOTE wakihofu tabia yake ya KUMSIFIA Vladimir Putin rais wa Urusi kama INAYOWAKERA.

Habari zinasema katika breafings ambazo hupewa rais kila siku WAMEZIPUNGUZA hasa zile zinazohusika na jasusi unaofanywa dhidi ya SERIKALI ZA KIGENI.

Kuna madai kuwa hawampi ushirikianao kama vile VYANZO ama NAMNA wanavyokusanya habari kutoka mataifa mbali mbali wanayoyafanyia ujasusi.

Moja ya wanabunge wa California aliyekatika kamati ya Bunge ya UJASUSI /Intelligence committee wa chama cha Democrat Adam Schiff amenakiliwa akisema kumekuwa na malalamiko ndani ya jamii hiyo.

Naye Trump amaeamua kwenda kwa wananchi ili awe karibu nao. Hivyo amaeamua kufanya mkutano wa hadhara katika mji wa Meliboun utakaohudhuriwa na watu walio na TIKETI maalum tu. Sijui kutoaminiana kati ya Trump na Jamii hiyo utafika wapi?
Chanzo: WALL STREET JOURNAL
kwahiyo kama itafikia hivyo kunaposibility kubwa ya kufanyiwa assassination?
 
Huyo DNI asipopewa taarifa zote atapeleka nini?
Mkuu walichofanikiwa wenzetu weupe ni kutengeneza mifumo na taasisi imara
(Strong institution & strong systems)
watu weusi sisi tuna Strong people si Strong institution & strong systems pia kila idara au taasisi inafanya kazi kwa kutimiza majukumu na wajibu wake ndo maana uwezi kusikia FBI wameingilia Kazi ya CIA pia uwezi kusikia Secret service wameingilia majukumu ya NSA leo hata mtu akiwa anafatiliwa na CIA akafanikiwa kuingia USA basi CIA watapeleka File kwa FBI na kuwaachia FBI waendelee pale walipoishia wao

Pia unatakiwa kujua Directors wote wa taasisi hzo 17 za ujasusi wanateuliwa na Rais wanakwenda kusibitiswa na US congress tu na mpaka leo ni watu 6 tu ndio walishawai kukataliwa na US congress ktk uteuzi wao toka utaratibu huu uanze so ni ngumu sana kwa DNI kunyiwa taarifa au kudanganywa na ikithibitika umemdanganya rais au umetoa taarifa za uongo na adhabu ni kufukuzwa so ukifukuzwa umekosa pensheni yako yote so hakuna mtu mjinga anayeweza kufanya hvyo pia unaweza kupelekwa mahakamani na kufungwa jela mpaka miaka 15
 
Back
Top Bottom