Tetesi: Majasusi wamnyima Trump siri nyeti

Hawana ubavu wa kumnyima commander inchief habari
Wenzetu si kama hapa kwetu ambapo raid anaweza kufanya au kuongea chochote atakacho halafu idara au hata miimili yote ikakubaliana naye. Wenzetu kila sekta inafanya majukumu yake kwa weledi wake bila kuingiliwa. Angalia jinsi mahakama yao ilivyotengua mpango wa Rais wao juu ya suala la mataifa mengine kuingia Marekani jambo ambalo ingekuwa hapa Tanzania hakuna jaji yeyote ambaye atadhubutu kupingana na mipango au hata matamshi ya Rais hata kama yataonekana dhahiri kuwa na mapungufu ktk utekelezaji wake. Idara ya kijasusi ya Marekani haiwezi kuburutwa na yeyote badala yake kiongozi akikomaa kuchuana nayo chochote chaweza kumfika. Kwa mwanzo huu wa Trump kupishana nao sidhani kama iko siku tena watajampa uwazi was ujasusi wao hasa yanayohusiana na nchi zenye mahusiano na Urusi. Watakuwa wameshamwekea alama ya kuwa na wasiwasi naye kwani wao wanajali zaidi maslahi ya kiusalama wa Taifa zaidi na si maslahi ya chama au ya kiongozi yeyote bila kujali ukuu wake ndani ya nchi.
 
Reactions: kui
Mm hapo bado sijawaelewa elewa. kwamba trump hawata mpa taarifa za kijasusi za dunia nzima au za urusi tu?

Na kama hizo taarifa hawata mpa rais trump na je hizo taarifa watampa Nani harafu na rais asijue.
Wale taarifa zote muhimu wanaweza kukaa nazo wenyewe na zile ambazo zitakuwa zinahatarisha usalama wa nchi watazimega kwa jeshi ambalo nalo pia Rais hawezi kulikurupusha apendavyo.

Sent from my HUAWEI Y336-U02 using JamiiForums mobile app
 
Huyo DNI asipopewa taarifa zote atapeleka nini?
 
Majasusi wa kibongo bongo ndio hutoa ushirikiano kwa mkulululuu wa bongo
 
kwahiyo kama itafikia hivyo kunaposibility kubwa ya kufanyiwa assassination?
 
Huyo DNI asipopewa taarifa zote atapeleka nini?
Mkuu walichofanikiwa wenzetu weupe ni kutengeneza mifumo na taasisi imara
(Strong institution & strong systems)
watu weusi sisi tuna Strong people si Strong institution & strong systems pia kila idara au taasisi inafanya kazi kwa kutimiza majukumu na wajibu wake ndo maana uwezi kusikia FBI wameingilia Kazi ya CIA pia uwezi kusikia Secret service wameingilia majukumu ya NSA leo hata mtu akiwa anafatiliwa na CIA akafanikiwa kuingia USA basi CIA watapeleka File kwa FBI na kuwaachia FBI waendelee pale walipoishia wao

Pia unatakiwa kujua Directors wote wa taasisi hzo 17 za ujasusi wanateuliwa na Rais wanakwenda kusibitiswa na US congress tu na mpaka leo ni watu 6 tu ndio walishawai kukataliwa na US congress ktk uteuzi wao toka utaratibu huu uanze so ni ngumu sana kwa DNI kunyiwa taarifa au kudanganywa na ikithibitika umemdanganya rais au umetoa taarifa za uongo na adhabu ni kufukuzwa so ukifukuzwa umekosa pensheni yako yote so hakuna mtu mjinga anayeweza kufanya hvyo pia unaweza kupelekwa mahakamani na kufungwa jela mpaka miaka 15
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…