The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 22,278
- 65,817
Kwahiyo nyie wanaume wa mjini mnaogopa majeneza kuuzwa sehemu sahihi? Jeneza haliepukiki,hata kama majeneza yatakua yanauzwa Kariakoo shimoni.Nyie wa vijijini kaeni kwa kutulia ya mjini hayawahusu
sadly 2090 humu patakua na comments, reply na avatar za marehemu kibao
dah hakuna kitu kibaya kama kifo nachukia sana kifo mimi
Hata bugando mwanza unapoanza tu kupandisha kilima kwenda hospital kushoto na kulia ni majeneza tu.Habari wanaJamiiForums. Kwanza nimshukuru Mungu kwa uzima tulionao. Pili nishukuru kwa jukwaa hili ambalo linatupa fursa ya kutema nyongo zetu kwa usalama.
Kwa yeyote kati yetu ambaye ameshawahi kufika hospitali ya Mkoa wa Dar es Salaam (Hospitali ya Rufaa) atakubaliana na mimi kwamba kuna majeneza yanauzwa getini pale. Yaani kabla hujaingia hospitalini unakaribishwa na majeneza yakiuzwa kushoto na kulia mwa barabara. Jambo hili linaleta ukakasi kwelikweli kwa wagonjwa. Yaani linamnyong'onyesha mgonjwa anayeenda kupambania afya yake, kwamba asipotoboa jeneza linamhusu.
Mimi nadhani wauza majeneza wangetafuta sehemu nyingine angalau iliyojificha na siyo pale. Siamini kama ndio utaratibu wa hospitali kubwa za serikali. Kwa muono wangu mimi siyo sawa, na ninaomba mamlaka husika zichukue hatua haraka kurekebisha hili.
Jambo la pili tunaomba Serikali inunue jenereta kubackup umeme unapokatika kwenye hospitali kubwa. Amana kwa mfano, umeme ukikatika na huduma zote zinasimama mpaka urudi. Si sawa kwa hospitali ya Rufaa kukosa jenereta.
NB: Nimetumia Hospitali ya Amana kama kielelezo hai. Kama kuna Hospitali zingine zenye mazingira kama haya na zenyewe ziangaliwe.
Ahsante.
Umezungumza jambo la maana sanaHabari wanaJamiiForums. Kwanza nimshukuru Mungu kwa uzima tulionao. Pili nishukuru kwa jukwaa hili ambalo linatupa fursa ya kutema nyongo zetu kwa usalama.
Kwa yeyote kati yetu ambaye ameshawahi kufika hospitali ya Mkoa wa Dar es Salaam (Hospitali ya Rufaa) atakubaliana na mimi kwamba kuna majeneza yanauzwa getini pale. Yaani kabla hujaingia hospitalini unakaribishwa na majeneza yakiuzwa kushoto na kulia mwa barabara. Jambo hili linaleta ukakasi kwelikweli kwa wagonjwa. Yaani linamnyong'onyesha mgonjwa anayeenda kupambania afya yake, kwamba asipotoboa jeneza linamhusu.
Mimi nadhani wauza majeneza wangetafuta sehemu nyingine angalau iliyojificha na siyo pale. Siamini kama ndio utaratibu wa hospitali kubwa za serikali. Kwa muono wangu mimi siyo sawa, na ninaomba mamlaka husika zichukue hatua haraka kurekebisha hili.
Jambo la pili tunaomba Serikali inunue jenereta kubackup umeme unapokatika kwenye hospitali kubwa. Amana kwa mfano, umeme ukikatika na huduma zote zinasimama mpaka urudi. Si sawa kwa hospitali ya Rufaa kukosa jenereta.
NB: Nimetumia Hospitali ya Amana kama kielelezo hai. Kama kuna Hospitali zingine zenye mazingira kama haya na zenyewe ziangaliwe.
Ahsante.
Hongera kumbe mpaka kariakoo shimoni unakufahamu?Kwahiyo nyie wanaume wa mjini mnaogopa majeneza kuuzwa sehemu sahihi? Jeneza haliepukiki,hata kama majeneza yatakua yanauzwa Kariakoo shimoni.
Good customer careWauza majeneza wameona waweke huduma karibu na wateja wao wakuu
Usichukulie comments za JF too serious.Hongera kumbe mpaka kariakoo shimoni unakufahamu?
Unataka picha ya dar? Mada inahusu majeneza labda tukupe picha ya majeneza tu.Weka picha mkuu ili na sisi wa huku vijijini tuione Daslam japo kwa picha
Mada inahusu majeneza yanayouzwa nje ya geti la Hospitali iliyopo Dar.Unataka picha ya dar? Mada inahusu majeneza labda tukupe picha ya majeneza tu.
Weee ngependekeza biashara gani iwekwe hapo? Guest au bar?Hata bugando mwanza unapoanza tu kupandisha kilima kwenda hospital kushoto na kulia ni majeneza tu.
Use unashirikisha akili kabla ya kutoa maoni humu GTWeee ngependekeza biashara gani iwekwe hapo? Guest au bar?
Biashara yoyote inalenga potential customers hiyo ndo sehemu sahihi ya hiyo display ya biashara, huwezi kupeleka biashara ya vipuri vya magari karibu na hospitali sio mahara pake au upeleke jeneza jaribu na bar au guest house.Use unashirikisha akili kabla ya kutoa maoni humu GT
1.Nani kakwambia guest na bar ndio biashara mbadala?
2. Kwani hoja hapa ni hayo maeneo kuwekwa biashara? Au hoja biashara ya majeneza kufanywa eneo LA wazi kama sehemu yakuingilia hospital?
N.B huko shuleni ulienda somea ujinga?!!
Hata usipokuwa na wasiwasi, mavumbini panatungoja tu.Mkuu uko sahihi!
Yaani mgonjwa akiyaona anakuwa na wasi wasi kwamba huenda anaenda kukata roho!
Wayaweke mbali kabisa.
Hata ww unaweza kuwa mteja wao saa yyteWauza majeneza wameona waweke huduma karibu na wateja wao wakuu