Majeneza getini mwa Hospitali ya Amana hayaleti taswira nzuri kwa Wagonjwa.

Nyie wa vijijini kaeni kwa kutulia ya mjini hayawahusu
Kwahiyo nyie wanaume wa mjini mnaogopa majeneza kuuzwa sehemu sahihi? Jeneza haliepukiki,hata kama majeneza yatakua yanauzwa Kariakoo shimoni.
 
Habari wanaJamiiForums. Kwanza nimshukuru Mungu kwa uzima tulionao. Pili nishukuru kwa jukwaa hili ambalo linatupa fursa ya kutema nyongo zetu kwa usalama.

Kwa yeyote kati yetu ambaye ameshawahi kufika hospitali ya Mkoa wa Dar es Salaam (Hospitali ya Rufaa) atakubaliana na mimi kwamba kuna majeneza yanauzwa getini pale. Yaani kabla hujaingia hospitalini unakaribishwa na majeneza yakiuzwa kushoto na kulia mwa barabara. Jambo hili linaleta ukakasi kwelikweli kwa wagonjwa. Yaani linamnyong'onyesha mgonjwa anayeenda kupambania afya yake, kwamba asipotoboa jeneza linamhusu.

Mimi nadhani wauza majeneza wangetafuta sehemu nyingine angalau iliyojificha na siyo pale. Siamini kama ndio utaratibu wa hospitali kubwa za serikali. Kwa muono wangu mimi siyo sawa, na ninaomba mamlaka husika zichukue hatua haraka kurekebisha hili.

Jambo la pili tunaomba Serikali inunue jenereta kubackup umeme unapokatika kwenye hospitali kubwa. Amana kwa mfano, umeme ukikatika na huduma zote zinasimama mpaka urudi. Si sawa kwa hospitali ya Rufaa kukosa jenereta.

NB: Nimetumia Hospitali ya Amana kama kielelezo hai. Kama kuna Hospitali zingine zenye mazingira kama haya na zenyewe ziangaliwe.

Ahsante.
Hata bugando mwanza unapoanza tu kupandisha kilima kwenda hospital kushoto na kulia ni majeneza tu.
 
Umezungumza jambo la maana sana
 
Ambao hatujaona hayo masanduku hapo amana tuna comment wapi
 
Hilo la backup ya umeme wa jenereta ndio la Msingi mnoo,,Naagiza wizara husika ilifanyie kazi kwa ufanisi na Haraka,,Wamo humu watapata ujumbe
 
Yote tisa kumi kama huo ni mradi wa Dr flani humo ndani mie siongei chochote
 
Weee ngependekeza biashara gani iwekwe hapo? Guest au bar?
Use unashirikisha akili kabla ya kutoa maoni humu GT

1.Nani kakwambia guest na bar ndio biashara mbadala?
2. Kwani hoja hapa ni hayo maeneo kuwekwa biashara? Au hoja biashara ya majeneza kufanywa eneo LA wazi kama sehemu yakuingilia hospital?

N.B huko shuleni ulienda somea ujinga?!!
 
Biashara yoyote inalenga potential customers hiyo ndo sehemu sahihi ya hiyo display ya biashara, huwezi kupeleka biashara ya vipuri vya magari karibu na hospitali sio mahara pake au upeleke jeneza jaribu na bar au guest house.
 
Wewe KCMC bado hujafika nadhani. Pale unaweza ukagoma hata kuendelea na safari ya hospitali
 
Back
Top Bottom