Majeshi ya nchi nyingine za kizalendo yaungane na JWTZ kuzuia vibaraka wa Wazungu M23 wasiuteke Mji wa Goma

Hana alijulo huyo. Si unajua chawa tena😆😃😀
Kwa nini wasitumie hizo rasilimali zao kulipa wanajeshi wao wenyewe badala ya kuzipa nchi nyingine?
JEshi sio kucheza playstation kwamba una hela unaenda sehemu unalipa unakua na jeshi, it needs lot of things kuliandaa, Binafsi naunga Mkono Tanzania kuingilia huo mgogoro, tunahitaji Congo salama kwenye interest zetu, wakimalizana na Congo ujue hata sisi hatutakua salama.
 
Nchi za EAC zimeikemee Rwanda iache kuivuruga Drc maana pia ni mwanachama wa EAC.
 
Kwa miaka 60 Congo imeshindwa kuliandaa jeshi lake kudhibiti nchi, hiyo ina maana hiyo nchi ni kubwa kuliko uwezo wao wa kuitawala. Hapo suluhisho ni mmoja tu, waigawe nchi kama ilivyofanyika Sudan.
 
Tunahitaji Congo Salama kwa Interests zetu zipi? Congo ikigawanywa kuwa nchi mbili au tatu ni faida kubwa zaidi kwa Tanzania.
 
Kwa miaka 60 Congo imeshindwa kuliandaa jeshi lake kudhibiti nchi, hiyo ina maana hiyo nchi ni kubwa kuliko uwezo wao wa kuitawala. Hapo suluhisho ni mmoja tu, waigawe nchi kama ilivyofanyika Sudan.
Wampe nani Rwanda?
 
Tunahitaji Congo Salama kwa Interests zetu zipi? Congo ikigawanywa kuwa nchi mbili au tatu ni faida kubwa zaidi kwa Tanzania.
Congo wana import hadi 500M+ usd kwa Mwaka toka Tanzania, tunawauzia vitu kibao mpaka Dagaa, wafanyabiashara wao wanafunga Shia vitu huku most of time, hapo bado Mizigo ya Transit, na Congo wanatumia USD hivyo inasaidia reserve za Hela za kigeni kwetu.

Ikigawanywa kwa Nchi ambazo sio rafiki kwa Tanzania Wataumia Bandari nyengine ama wata trade na nchi nyengine, ila tukiwasaidia sisi ni rahisi kuwekeana mikataba ambayo ni favourable kwetu.
 
Kwani Sudan Kusini alipewa nani??
Pakistan alipewa nani alipojiondoa kutoka India?
Bangladesh alipewa nani ilipojiondoa kutoka Pakistan?
Hizo nchi zilikuwa na watu wa ndani, waliotaka Kujitenga ila Congo ni interference za mataifa ya nje so situation ni tofauti.
 
Bandari gani zaidi ya Dar Es Salaam inayoweza kuwa mbadala kwa unafuu kwa eneo lolote la DRC? Kama ipo hiyo bandari basi ujue kinachoizuia DRC kuitumia hiyo bandari sasa hivi ni vita au utawala mbovu na siku DRC ikitulia ndio tutaipoteza kabisa kama mteja wa bandari ya Dar.
 
EAC ni hii inayoandaa CHAN hizo nchi nyingine ni kuwaridhisha wakubwa huko Ulaya.
 
Ukienda kumsaidia mjinga basi nawe mjinga pia, kwa tarifa yako Goma tayali iko mikononi mwa M23. Now usalama ndio umepatikana mauwaji ya kiholela kwisha.
 

Attachments

  • C5vHebI6xHwFBK7t.mp4
    1.4 MB
  • 20250126_192342.jpg
    124.2 KB · Views: 1
  • 20250126_194209.jpg
    140.7 KB · Views: 1
  • 20250126_194206.jpg
    153.9 KB · Views: 1
  • 20250126_194515.jpg
    47.1 KB · Views: 1
  • 20250126_194513.jpg
    47 KB · Views: 2
  • 20250126_194203.jpg
    151.1 KB · Views: 1
Tanzania ina maslahi makubwa Congo, ili tupate faida ya bandari yetu inabidi tupambane Congo iwe mahali salama na biashara zao ziende
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…