Majeshi ya nchi nyingine za kizalendo yaungane na JWTZ kuzuia vibaraka wa Wazungu M23 wasiuteke Mji wa Goma

Majeshi ya nchi nyingine za kizalendo yaungane na JWTZ kuzuia vibaraka wa Wazungu M23 wasiuteke Mji wa Goma

Hana alijulo huyo. Si unajua chawa tena😆😃😀
Kwa nini wasitumie hizo rasilimali zao kulipa wanajeshi wao wenyewe badala ya kuzipa nchi nyingine?
JEshi sio kucheza playstation kwamba una hela unaenda sehemu unalipa unakua na jeshi, it needs lot of things kuliandaa, Binafsi naunga Mkono Tanzania kuingilia huo mgogoro, tunahitaji Congo salama kwenye interest zetu, wakimalizana na Congo ujue hata sisi hatutakua salama.
 
Inakera sana kuona Baadhi ya Nchi za Kiafrika zimejikausha na kuisusa DRC Kwa kuiacha inagukie kwenye mikono ya Jeshi la Vibaraka wa Wazungu M23 Kupitia Rwanda.

Ni kama Wameisusia Tanzania peke yake kiasi kwamba inaweza ikawa ngumu Kwa JWTZ Kuzuia hao Vibaka kuuteka Mji wa Goma ikizingatiwa kwamba watakuwa wanapewa vifaa vya Kisasa ,kusaidia inteligensia nk na Mabeberu. Soma JWTZ yatoa sababu 200 zilizoifanya Tanzania ipambane na waasi wa M23

Wananchi wa DRC wa Imani na JWTZ lakini Sina hakika kama wao yao wataweza kuwazuia M23 ikizingatiwa kwamba JWTZ Iko huko kulinda amnani na sio mstari wa mbele wa Vita,wanatakiwa kuwa mstari wa mbele NJ Jeshi la DRC lakini ndio Hilo limezidiwa.Inatia sana hasira.👇👇

View: https://youtu.be/Fs7jEBnCRJU?feature=shared

My Take
Nchi zingine za Kizalendo Ziungane kuzuia huu uhuni wa Rwanda.

Ikumbukwe Rwanda Kwa Sasa imepunguza sana biashara na Tanzania na bidhaa zao nyingi wanapitishia Bandari ya Mombasa.

View: https://youtu.be/yi8VlUZYe84?feature=shared

Nchi za EAC zimeikemee Rwanda iache kuivuruga Drc maana pia ni mwanachama wa EAC.
 
JEshi sio kucheza playstation kwamba una hela unaenda sehemu unalipa unakua na jeshi, it needs lot of things kuliandaa, Binafsi naunga Mkono Tanzania kuingilia huo mgogoro, tunahitaji Congo salama kwenye interest zetu, wakimalizana na Congo ujue hata sisi hatutakua salama.
Kwa miaka 60 Congo imeshindwa kuliandaa jeshi lake kudhibiti nchi, hiyo ina maana hiyo nchi ni kubwa kuliko uwezo wao wa kuitawala. Hapo suluhisho ni mmoja tu, waigawe nchi kama ilivyofanyika Sudan.
 
Tunahitaji Congo Salama kwa Interests zetu zipi? Congo ikigawanywa kuwa nchi mbili au tatu ni faida kubwa zaidi kwa Tanzania.
 
Kwa miaka 60 Congo imeshindwa kuliandaa jeshi lake kudhibiti nchi, hiyo ina maana hiyo nchi ni kubwa kuliko uwezo wao wa kuitawala. Hapo suluhisho ni mmoja tu, waigawe nchi kama ilivyofanyika Sudan.
Wampe nani Rwanda?
 
Tunahitaji Congo Salama kwa Interests zetu zipi? Congo ikigawanywa kuwa nchi mbili au tatu ni faida kubwa zaidi kwa Tanzania.
Congo wana import hadi 500M+ usd kwa Mwaka toka Tanzania, tunawauzia vitu kibao mpaka Dagaa, wafanyabiashara wao wanafunga Shia vitu huku most of time, hapo bado Mizigo ya Transit, na Congo wanatumia USD hivyo inasaidia reserve za Hela za kigeni kwetu.

Ikigawanywa kwa Nchi ambazo sio rafiki kwa Tanzania Wataumia Bandari nyengine ama wata trade na nchi nyengine, ila tukiwasaidia sisi ni rahisi kuwekeana mikataba ambayo ni favourable kwetu.
 
Kwani Sudan Kusini alipewa nani??
Pakistan alipewa nani alipojiondoa kutoka India?
Bangladesh alipewa nani ilipojiondoa kutoka Pakistan?
Hizo nchi zilikuwa na watu wa ndani, waliotaka Kujitenga ila Congo ni interference za mataifa ya nje so situation ni tofauti.
 
Congo wana import hadi 500M+ usd kwa Mwaka toka Tanzania, tunawauzia vitu kibao mpaka Dagaa, wafanyabiashara wao wanafunga Shia vitu huku most of time, hapo bado Mizigo ya Transit, na Congo wanatumia USD hivyo inasaidia reserve za Hela za kigeni kwetu.

Ikigawanywa kwa Nchi ambazo sio rafiki kwa Tanzania Wataumia Bandari nyengine ama wata trade na nchi nyengine, ila tukiwasaidia sisi ni rahisi kuwekeana mikataba ambayo ni favourable kwetu.
Bandari gani zaidi ya Dar Es Salaam inayoweza kuwa mbadala kwa unafuu kwa eneo lolote la DRC? Kama ipo hiyo bandari basi ujue kinachoizuia DRC kuitumia hiyo bandari sasa hivi ni vita au utawala mbovu na siku DRC ikitulia ndio tutaipoteza kabisa kama mteja wa bandari ya Dar.
 
Kwa kweli inashangaza ,haya maumojanyasiyo.na maana Bora Kujitoa tuu.

Yaani EAC Wameshindwa kuwakanywa Rwanda ,kwanza Inaelekea Tanzania pekee ndio Wazalendo wengine wote waliotuzunguka ni mawakala wa Mabeberu kina Rwanda,Uganda,Kenya nk.

Bila Tanzania hata Burundi ingeshaanguka Kwa vibaraka.
EAC ni hii inayoandaa CHAN hizo nchi nyingine ni kuwaridhisha wakubwa huko Ulaya.
 
Ukienda kumsaidia mjinga basi nawe mjinga pia, kwa tarifa yako Goma tayali iko mikononi mwa M23. Now usalama ndio umepatikana mauwaji ya kiholela kwisha.
 
Attachments

  • C5vHebI6xHwFBK7t.mp4
    1.4 MB
  • 20250126_192342.jpg
    20250126_192342.jpg
    124.2 KB · Views: 1
  • 20250126_194209.jpg
    20250126_194209.jpg
    140.7 KB · Views: 1
  • 20250126_194206.jpg
    20250126_194206.jpg
    153.9 KB · Views: 1
  • 20250126_194515.jpg
    20250126_194515.jpg
    47.1 KB · Views: 1
  • 20250126_194513.jpg
    20250126_194513.jpg
    47 KB · Views: 2
  • 20250126_194203.jpg
    20250126_194203.jpg
    151.1 KB · Views: 1
Tanzania ina maslahi makubwa Congo, ili tupate faida ya bandari yetu inabidi tupambane Congo iwe mahali salama na biashara zao ziende
 
Back
Top Bottom