Majeshi yangu bora ya Afrika 2024

Majeshi yangu bora ya Afrika 2024

kwa mara ya kwanza naona ndani ya thread yako umesifu zana za mrusi
big up braza
Kwanini huwa mnadai naziponda silaha za Urusi, huwa nafanya fair comparison. Iwe naipinga silaha yao au naikubali dhidi ya nyingine ya Western bado nafanya fair sipindishi.
Mfano hapo nimetaja Yak-130 trainer kuwa ni bora kutoka Urusi, sio bora dunia nzima. Ila kwenye list ya trainers bora duniani ipo, ingawa haiwezi kuwa ya kwanza ushindani ni mkali. Nyinyi mnataka niseme Russia ni wazuri kila kitu au wabovu kila kitu wakati sio.
 
5. Nigeria
Hakuna nchi ya kukaa nafasi ya tano kama si Nigeria. Wana tatizo la ugaidi ila ni ideology vigumu kupambana nayo. Pia wana shida ya ufisadi jeshini, na morali ndogo sana. Wanajeshi wa Nigeria huliowa kidogo na maofisa wao hujilimbikizia mali.

Idadi ya wanajeshi: 200,000+ ila nina wasiwasi kuna wanajeshi hewa kiasi.

Idadi ya ndege: Rais Buhari alikuza sana military spending na alifanya sana procurement. Nigeria wana Chinese & Pakistani JF-17 4th generation fighter jet cache sana, wana Chengdu F-7 kama Tanzania ila za kwao zinapata sana ajari. Wana ground attack Embraer EMB 314 Super Tucano imependwa kwenye mashambulizi yake dhidi ya Boko Haram. Wana Alpha jets kutoka Ufaransa. Airforce yao ni average kwa nchi masikini ila wana idadi ndogo ya ndege.

Melivita: Wana frigate moja tu na makumi ya meli ndogo ndogo.

Vifaru: Wana VT-4 MBT kutoka China idadi 30 walichukua, T-72 kutoka Urusi walichukua miaka ya hivi karibuni. T-54 ya zamani na Vickers kutoka Uingereza, kutokana na historia yao ya utunzaji mbovu itakuwa Vickers vina hali mbaya maana hata spare parts ni shida kupata.
Pia wana IFV na APC na vehicles nyinginezo kwa idadi nzuri.

Uchumi: $ 1.1 trillion

Population: More than 200 million

Baadhi ya silaha zao View attachment 2893145View attachment 2893148

MWISHO
Mkuu Umesahau Tanzania ni ya 6 Duniani..
Alisema yule msemaji wetu
 
Tangu ulipotuamisha kuhusu IDF kuwa jeshi bora sana duniani, ukasifia vifaru vyao vya Mercava, ukawananga warusi kuwa ni jeshi bovu na wame underperform huko Ukraine; napata mashaka na uchambuzi wako, hasa ukizingatia performance ya IDF huko gaza.
 
Mkuu Umesahau Tanzania ni ya 6 Duniani..
Alisema yule msemaji wetu
Tanzania hatuwezi kuwa kinara wa lolote jema duniani. Wachungaji wetu wezi wa sadaka na matapeli, watumishi wa Mungu wahuni mara wanabaka mara wanalawiti, wanasiasa mafisadi, wanandoa sio waaminifu, wakandarasi wakifanya miradi wanalipua, maaskari waonevu, wahudumu wa afya hawajitumi.

Kwenye jamii ya watu wahuni kama hao hamuwezi kuwa na jeshi imara duniani, jeshi ni product ya jamii na ndio kielelezo cha haraka cha jamii iliyostaarabika. Haiwezekani kila sekta na taasisi hata za kidini ziwe mbovu alafu eti jeshi tu ndio liwe sawa.
 
Tanzania hatuwezi kuwa kinara wa lolote jema duniani. Wachungaji wetu wezi wa sadaka na matapeli, watumishi wa Mungu wahuni mara wanabaka mara wanalawiti, wanasiasa mafisadi, wanandoa sio waaminifu, wakandarasi wakifanya miradi wanalipua, maaskari waonevu, wahudumu wa afya hawajitumi.

Kwenye jamii ya watu wahuni kama hao hamuwezi kuwa na jeshi imara duniani, jeshi ni product ya jamii na ndio kielelezo cha haraka cha jamii iliyostaarabika. Haiwezekani kila sekta na taasisi hata za kidini ziwe mbovu alafu eti jeshi tu ndio liwe sawa.
Ni kwasababu watu wanatengenezwa na ugumu wa Maisha
 
2. Algeria
Algeria huwa inakaa #2 mara nyingi. Walianza fujo wakati wanatafuta uhuru kutoka Ufaransa wakapigana. Baada ya kuwa huru wakapigana muda mrefu kubishana kati ya kuwa secular au non- secular state. Walikuwa na makundi mengi ya kidini ila miaka ya 1990s wakatengamaa. Wamekaa kwa wasiwasi ndani yao, harakati za nchi za Kiarabu pamoja na chuki kubwa sana waliyonayo dhidi ya Morocco majirani zao.
Kuna miaka Algeria walinunua 45% ya silaha zote zilizonunuliwa Afrika.

Idadi ya wanajeshi: est. 320,000
Idadi ya ndege: Helicopters kama Mi-24 Hind, Mi-28 Havoc, Mi-17, Ka-27 za majini. Fighter jets kama Mig-29, Su-30 ambayo ni front line fighter na Su-24 for attack. Wana trainers za kisasa kama Yakovlev Yak-130 trainer bora zaidi ya Urusi, L-39 kutoka Ulaya hii inapendwa sana na nyinginezo. Wana transport aircrafts kama C-130 na Ilyushin Il-76

Melivita: Algeria wako vizuri kwenye Navy, naval assets zaidi ya 200. Kuna muda walikuwa na submarines 14 ila nyingine za zamani na nyingine nina imani ziko retired au mothballed.

Vifaru: Ina vifaru zaidi ya 1,400 vikiwemo vya zamani kama T-55. Wana T-90A zaidi ya 500 na version moja ya T-72 vifaru zaidi ya 300.

Uchumi: $516 billion in PPP.

Population: Milioni 47 hivi. Hawa wanalazimisha kuwa na wanajeshi wengi kinyume na population yao.

Bila kusahau Algeria wana missile arsenal & rocketry nzuri sana. Hata Iskander missiles wanazoView attachment 2893075
Islander missile hazijawahi kuuzwa popote
 
Islander missile hazijawahi kuuzwa popote
Screenshot_20240723-094320~2.png

Russia, Algeria na Armenia
 
Ni kazi kubwa sana kupima uwezo wa kijeshi wa nchi, kuna vigezo vingi hutumika na pengine kwa malengo tofauti. Kuna vyanzo ranking huzingatia namba kwamba idadi ya zana na wanajeshi, hii ni rahisi kufanya na hutumiwa pale mtu asipotaka mambo mengi ila sio sahihi. Hakuna ranking inayoweza kutoa majibu 100% kwa usahihi ila ranking nzuri inatoa makadirio yanayoendana na ukweli.

Kwanza kabisa ranking yangu haihusishi majeshi dhidi ya makundi ya waasi, magaidi au makundi ya kiitikadi yanayotaka kujitenga. Hii ni kulinganisha jeshi la nchi endapo lingepigana na jeshi la nchi nyingine.
Nimekwepa mtego huo sababu una mkanganyiko hata kwingineko duniani. Uturuki ina jeshi kubwa, ila ina waasi wa kundi la PKK wanaisumbua. Huwezi sema basi Uturuki haina nguvu sababu PKK hawaiwezi, ile ni ideology sio silaha. Au huwezi sema nchi ya Sao Tome and Principe yenye population ndogo kuliko idadi ya wanajeshi wa Misri, eti ina jeshi bora zaidi ya Misri sababu Sao Tome and Principe wenye wanajeshi less than 1,000 hakuna kundi la kigaidi na Misri kule Sinai kuna magaidi.

Imagine uiambie JWTZ ipigane na Wanyakyusa wakorofi iwaache watulivu. Sasa itajuaje kirahisi huyu Mwaikimba aliyepo Kigoma ni mkorofi, na huyu Mwamakula aliyepo Tanga ni msafi wakati wote wana act ni wasafi. Na Wanyakyusa wakorofi hawana kambi wala ofisi, wala hutakiwi kuua wote sheria za kimataifa zinakataa, na huwezi bomoa nyumba zote za Wanyakyusa utaathiri na wasio na hatia, na ukienda kuwatembelea hata ukihutubia wote wasafi na wakorofi wanakuona, wanajichanganya na wewe na wanakujua sababu umevaa sare unajulikana mwanajeshi wakati wao wamevaa fulana ya klabu au chama cha kisiasa wakati ni wakorofi.

Pia ukiachana na idadi ya silaha & zana na wanajeshi. Nimezingatia;

Ukubwa wa uchumi na rasilimali: Nchi yenye uchumi mkubwa inaweza piga nchi yenye uchumi mdogo. Inaweza kununua silaha bora na nyingi, inaweza chukua mkopo mkubwa wa silaha kama uchumi unaruhusu kulipa, ni suala la kutazama debt to GDP ratio na mambo mengine ya kiuchumi. Hapo usitarajie Rwanda kununua silaha sawa na DR Congo wakati wa shida.
Pia nchi yenye rasilimali nyingi kwa Afrika inaweza ziweka rehani ikakopa au ikaungwa mkono kwa misaada, silaha na kuungwa mkono kidiplomasia kama ambavyo Nigeria ilifanya kwenye vita ya Biafra. Waingereza wakapewa ahadi ya mafuta na USSR wakapewa ahadi ya iron ore, Wamarekani sijui walipewa nini. Kwa pamoja zikaiunga mkono Nigerian Federal government wakati kwa kawaida huwa hazikai pamoja kwenye migogoro na mwanzoni kila mmoja alikuwa upande wake (mojawapo ya sababu Kanali Ojukwu alikuwa na confidence, alijua anaungwa mkono).

Population: Nchi yenye watu wengi inaweza unda jeshi kwa muda wa dharula, ikapata reserves wa kutosha na kuendesha fronts nyingi. Inaweza sustain human loss kwenye vita, POWs, KIA, MIA, deserters.

Jiografia: 'Kiafrika' kuwa na bahari ni faida kijeshi, imports & exports sio rahisi kuzuiliwa na adui. Hapa Uganda ina disadvantage kubwa sababu iko landlocked inategemea Tanzania na Kenya. Ethiopia naona ina hasara kubwa ya kuwa landlocked kuliko nchi zote Afrika.
Pia nchi yenye majirani wengi kama Tanzania sio faida kiusalama kama nchi yenye jirani wachache.

Utawala wa nchi: Serikali za kidikteta hulizingatia sana jeshi hivyo zina majeshi makubwa, imara, yenye bajeti kubwa na utayari zaidi ya serikali za kiraia. Hata hivyo nchi za kiraia hupata support kubwa sana ya wananchi. Hapa Museveni au Kagame wako standby na majeshi ila kuna wananchi wengi sana wanaoamini jeshi ni la watawala wala haliwahusu raia. Kinachotokea mara nyingi kwenye vita na hizi nchi ni ushindi wa muda mfupi wa battles za mwanzoni, kisha nchi ya kiraia iki-gain momentum mobilization ya public inawapa nguvu kufanya counterattack. Yaleyale ya vita ya Kagera.

Pia nchi yenye rushwa, upendeleo wa matabaka, utawala mbovu, uongo na ufisadi iko more likely kuwa disorganized kwenye majeshi. Maofisa wa kamlete hawajawahi kuwa na uwezo mbele ya maofisa wanaojua waliopata kwa kustahili, wanajeshi walioingia ili waibe hela au wapate ajira ni hasara vita ikitokea. Iddi Amin alikuwa na Chief of Staff mpumbavu kwenye vita hadi maofisa waandamizi walipanga wamuue alikwamisha jeshi. Imagine Museveni ana mwanae Muhoozi ni Jenerali, hata akili zake na busara zake haziko sawasawa eti huyo aongoze jeshi.

Bajeti ya jeshi: Bajeti ina mchango wake ingawa exactly ni siri ila makadirio sahihi yapo na kwa sababu. Bajeti ya jeshi hupimwa kwa ratio ya GDP. Unakuta nchi inatumia 9% ya GDP yake kwenye ulinzi, wastani nchi nyingi duniani hazivuki 2%. Nchi Y inaweza kuwa ina $16 billion kama bajeti ya nchi nzima ila ikatumia 4% of GDP kwenye jeshi. Wakati X yenye uchumi mdogo wa $12 GDP inatumia 9% of GDP hivyo X ina bajeti kubwa ya jeshi.
Mazoea ya kuwa na bajeti ndogo kila mwaka husababisha kuwa na poor equipped military, unakuwa na zana za kizee na hazina maintenance nzuri (maintenance ya silaha ni gharama sana). Unakuwa na jeshi ilimradi, kupigia gwaride na kufanyia maonyesho. Hasara kubwa zaidi unakuwa huna uzoefu na silaha, mastering of arms ni suala la mazoea na makosa ya muda mrefu. Sio kama bodaboda unanunua tu kuendesha utajua mbele ya safari, silaha zina logistics zake, compatibility mfano umenunua fighter jets vipi kuhusu air to air missiles na spare parts, order yake ina muda wa kusubiri huendi yard China au Ufaransa ukafunga maboksi kama zana za kilimo, kuna geopolitics nyingi sana mara huyu anaona uko desperate na vita analazimisha ufanye kitu fulani ndio akuuzie silaha kwa bei ghali. Bado silaha zije uanze mafunzo na muda huo vita inaendelea, utapata matokeo mabovu sana ya matumizi. Silaha sio pikipiki kwamba kisa najua kuendesha Boxer basi hata TVS nitajua, yani rubani mzoefu wa Su-30 kwa miaka 7 ukimpa J-17 na mafunzo ya wiki ukamwambia kapigane unampa tiketi ya kifo.

Naishia hapa uzi usijefutika nikaanza upya...... Inaendelea
GDP hazina uhasilia
 
Inaonekana vita inahamia kwenye drones. Tuwekeze kwenye kufundisha watu masuala ya drones. SA waliwekewaga vikwazo vya silaha wakati wa ukaburu, wakaaanza kuunda wenyewe. Waliunda mzinga mmoja bora sana hadi nchi zingine zikaanza kununua. Wakaja hawa wakina Zuma wanawaza ngono na kula, yaani hata starehe zao ni basic kabisa!!
 
Kwa mfano umeandika GDP ya Egypt ni zaidi ya 1 tr usd! Hamna nchi ya Africa iliyofika hapo
Ungesoma hapo niliandika kabisa kwamba ni in terms of PPP si ndio. Sasa wewe unakariri nominal. Egypt hata kufika $2 trillion GDP in PPP haitokuwa ajabu.
 
Back
Top Bottom