Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Status
Not open for further replies.
i get you ether..pia nakuunga mkono lunyungu....mnajua tumepigana sana afrika hii lakini hatujui kutumia influence yetu kiuchumi..mimi ninaposafiri kwenye baadhi ya hizo nchi ie southafrica ..roho huniuma sana kuona wadogo na watoto zetu..wanakebehiwa kama ombaomba...masikini..wanauliwa hovyo na kutukanwa tena afadhali wazungu kidogo wanawastahi ..watu weusi ndio wanaongoza kuwanyanyasa wadogo zetu....bora wangekuwa wanawarudisha kwa amani....

ukijaribu kuwaambia mbona sisi tuliwasaidia mlipokuwa mnakimbia hovyo...mbona tulichangishwa shule damu na pesa kwa ajili ya ukombozi...mbona tuliwasomesha wapigania uhuru kuanzia nursery na wengi tumekuwa nao university ,jeshini ,na hata kuwafunza ujasusi....hawakumbuki....bado uganda na kwingineko....

hatujapata kufaidika na harakati zetu...mwaka 1994 tulipeleka majeshi liberia kwa ahadi ya kulipwa ..na UN ...hatukulipwa ..labda kama pesa ililiwa....vijana walikufa hakuna tulilopata....

kimsingi kutokana na historia yetu naona kuwa hii vita comoro inatugharimu wakati ambapo ..tuna hali ngumu ya uchumi..barabara hazijengeki...na tayari majeshi yapo huko ...nahisi kuwa hatutaweza kujiondoa tena hukom itabidi tuendelee kugharamika.....

jamani kama ni kujitolea nchi hii tumeshajitolea sana ...kama UN au AU wanataka jeshi letu wagharamie kila kitu ...kila kitu.......HATUTAKI PESA ZA KODI ZETU ZITUMIKE TENA KUPIGANIA NJE!!!
Nchi nyingi zimepata uhuru afrika sasa ni zamu yao kusaidia ..sijasikia NAMIBIA..MSUMBIJI..AFRIKA KUSINI...Ets wakisaidia majeshi ya amani kwa kiwango ambacho walistahili....na sisi tupumzike....
 
Na Saed Kubenea
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepeleka majeshi nchini Comoro ili “kumng’oa” Kanali Mohamed Bacar ambaye anadaiwa kung’ang’ania kwenye madaraka katika kisiwa cha Anjouan baada ya muda wake wa utawala kumalizika.

Askari 650 wa Tanzania tayari wamewasili nchini humo, tokea 11 Machi, 2008 kushiriki kumg’oa Kanali Bacar ambaye kipindi chake cha uongozi kimemalizika tangu Aprili 2007.

Uamuzi wa serikali kupeleka majeshi Anjouan, ulitangazwa na mawaziri Dk. Hussein Mwinyi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Bernard Membe (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), katika mkutano wao na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Tanzania, nchi nyingine zilizopepeleka majeshi ni Sudan, Senegal na Libya. Majeshi hayo yamepewa jukumu la kumng’oa Kanali Bacar, kumkamata na kumfikisha mahakamani.

Muungano wa serikali ya Comoro unajumuisha serikali za visiwa vya Ngazija, Moheli na Anjouan katika muundo uliotokana na mkataba wa Fomboni wa 17 Februari 2001.

Membe anasema majeshi yanakwenda Comoro “kurejesha utawala wa kisheria na demokrasia” kisiwani Anjouan.

Kwanza lazima tuangalie uhalali wa Kanali Bacar kuwapo madarakani. Kwa mujibu wa Katiba ya Comoro, kutokana na kutokuwapo ukomo wa uongozi, mwanajeshi huyo alikuwa na haki ya kuendelea kugombea urais wa kisiwa hicho.

Hivyo hakufanya makosa zaidi ya kukiuka taratibu. Ni dhahiri jambo hili linaweza kurekebishwa bila kutumia nguvu za kijeshi. Mara nyingi sana nguvu za kijeshi husababisha madhara makubwa.

Aidha, katika uchaguzi aliouitisha, ambao nchi washirika katika vita hiyo wanaupinga, Kanali Bacar alishinda kwa zaidi ya asilimia 85. Je, AU inapingana na matakwa ya wananchi wa Anjouan?

Tujifunze Irak. Marekani ilivamia nchi hiyo mwaka 2003. Rais George Bush alijitapa kwamba vita hivyo vingechukua wiki chache sana, kutokana na alichosema “wananchi wa Irak wanaunga mkono kampeni za kumuondoa Saddam Hussein.” Vita inaendelea hadi leo.

Je, akina Membe wana uhakika gani iwapo hilo halitatokea kwa majeshi ya Tanzania, kama wanavyodai, ili kupunguza vifo na uharibifu wa nchi?

Mgogoro wa Comoro ulianza mara tu baada ya visiwa hivyo kujitawala kutoka Ufaransa mwaka 1975 na tayari serikali imepinduliwa mara 19 tangu hapo.

Hata hivyo, kuna kisiwa cha Mayotte kilichoasi tangu wakati wa uhuru baada ya kutaka kuendelea kuwa chini ya himaya ya Ufaransa, jambo ambalo hadi leo hii, mabingwa wa vita wameshindwa kulitafutia ufumbuzi.

Je, kwa nini AU haukupeleka majeshi yake hapo kukikomboa kisiwa hicho kutoka mikononi mwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa?

Ni jambo gani linaloisukuma Tanzania na washirika wake kuivamia Anjoaun wakati wananchi wa kisiwa hicho hawajalalamika kudhulumiwa, kuteswa na kunyanyaswa na Kanali Bacar?

Kwa nini AU haijapeleka vikosi Zimbabwe kuwakomboa wananchi wanaoteseka chini ya mkono wa chuma wa Robert Mugabe?

Kwa nini Tanzania haijapeleka majeshi kuyakomboa maeneo yanayokaliwa na waasi wa Kongo (DRC) wanaoongozwa na Jenerali Laurent Nkunda?

Membe na Mwinyi wanasema kwamba watahakikisha vifo vya raia na majeshi vinakuwa vichache. Hawajasema wamepanga kuua watu wangapi katika hicho wanachokiita “kuua watu wachache.”

Lakini pia kuna hili la uhalali wa serikali kupeleka majeshi nje ya nchi kwa dhamira ya kuondoa utawala ambao haujalalamikiwa na wananchi wenyewe.

Hili si suala la kupeleka majeshi kulinda amani, kama tulivyowahi kupeleka nchini Liberia na Lebanon.

Kwa kuwa suala ni uvamizi wa kijeshi, basi angalau serikali ingepata ridhaa ya wananchi kupitia Bunge lao. Nchi haipaswi kuingizwa vitani bila ridhaa ya chombo cha wawakilishi, hata kama hilo lilishawahi kutokea huko nyuma.

Hata Marekani ilipotaka kuvamia Irak, Bunge lake la Congress lilijulishwa na baadaye likaidhinisha kwa kupiga kura.

Hata Serikali ya Japan ilifanya hivyo mwaka 2004 ilipotaka kupeleka wanajeshi wake nchini Irak kwa ajili ya kulinda amani.

Watawala wa Japan walikuwa wamefuta kabisa uwezekano wa wanajeshi wao kutumika popote nje ya nchi yao baada ya shambulio la bomu la nyuklia lililofanywa na Marekani katika mji wa Hiroshima mwaka 1945.

Pamoja na kwamba Bunge la Japan lilikubali serikali ipeleke wanajeshi nchini Irak, bado lilitaka wanajeshi hao wasishiriki katika mapambano, bali wabaki tu kuwa wahudumiaji wa shughuli za dharura za kibinadamu.

Wataalamu wa sheria Tanzania wanasema wazi kwamba hata sheria zetu na katiba yetu, haziruhusu wanajeshi kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kufanya uvamizi.

Lakini hilo halikufanyika, badala yake, Membe na Mwinyi wanasema, “tayari rais amelijulisha Bunge, Baraza la Mawaziri na vikao vya juu vya chama chake - Chama Cha Mapinduzi (CCM). Haifahamiki Bunge limeshiriki vipi katika uamuzi huu.

Je, kama hivyo ndivyo, ni wapi ambako Rais Jakaya Kikwete amepata madaraka na mamlaka ya kuipeleka nchi vitani?

Ni dhahiri kama serikali ingepeleka maombi yake bungeni na Bunge likaridhia uamuzi huo, angalau tungeweza kusema kwamba wananchi wameshirikishwa na wameridhika nchi iende vitani.

Hakika katika suala la nchi kwenda vitani, hakupaswi kuwepo ushirikishaji mtu mmoja au kamati moja ya bunge, bali kupata maoni mapana na ruhusa kamili ya bunge zima hasa inapokuwa kwamba Comoro haijaivamia Tanzania.

AU haikupaswa kukubali ombi la Rais Sambi la kupewa majeshi ili kumg’oa Bacar. Ingemshauri rais kuweka shinikizo kwa Kanali Bacar, kukubali kuitisha uchaguzi mwingine utakaosimamiwa na Jumuiya za Kimataifa. Na hili Kanali Bacar alilikubali.

Kwa kujua hilo, Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, amepingana na wenzake katika utumiaji nguvu za kijeshi. Anaamini kwamba mgogoro huo unaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo.

Inawezekana kabisa kwamba Kanal Bacar, ni mnafiki, katili na mzandiki wa kutupwa kama anavyodai Membe, lakini ukweli unabaki palepale kuwa bado anaungwa mkono na wananchi wake tena walio wengi.

Kama si hivyo, kwa nini rais Sambi ameshindwa kuingia Anjouan? Je, ameogopa nini? Hilo ndilo tunastahili kujengea mashaka.
 
Interest ya Tanzania Comoro ni nini? Je, hizo interest ni za mtu binafsi au kikundi cha watu?

Kama ni interest ya nchi kwa nini rais aliyepewa dhamana na kula kiapo kama amiri jeshi mkuu kwa nini hakuja yeye mwenyewe binafsi na kuwaambia Watanzania ambao ndio walipa kodi? Hiki kiburi cha kuwadharau walipa kodi kwa muda wote huu kinatoka wapi?

Je, ni sahihi waziri wa ulinzi na huyo wa foreign affairs kutangaza vita?
 
Jamani bado mnalivalia njuga hili swala?..
Nimeshasema kuwa Comoro ni sehemu ya Tanzania kwa kizazi..Tuna Watanzania kibao ndani ya serikali ya Comoro na wengine ni raia hapa kwetu tena naweza sema asilimia kubwa ya wananchi wazawa na wakazi wa Unguja ni Wakomoro.
Tulishawahi kuvunja mapinduzi kama hayo Komoro miaka ya Nyerere na leo hii ni marudio tu hawa jamaa kina Kanali Mohamed Bacar hawawezi kuingizwa ktk daraja la insurguency kwani sii wananchi wenyewe wanaotaka mapinduzi hayo ila kundi la wanajeshi mbuzi waliolewa madaraka kama Mugabe. Acheni vijana wapate mazoezi kidogo, miaka mingi imepita toka Uganda hatujaribu uwezo wa jeshi letu.
Sii rahisi kuziona interest za Tanzania Komoro ikiwa huwezi kuona madhara mengi yatakayotokana na familia zilizopo hapa nchini kwetu. Komoro ni sawa na Israel kwa Marekani...kizuri chake kwa mlalahoi kama mimi siwezi kukiona..
Trust me hadi leo sielewi kwa nini Marekani wanawalinda Israel kwa billions of dollar pamoja na silaha. Yawezekana mimi sii mwanasiasa kuweza kuona ndani.
 
Hii story ya Kubenea imeegemea upande mmoja, kwa nini asingeelezea mwanzo wa tukio zima mpaka juzi kwenye kikao cha AU ambacho kiliafikia nguvu za kijeshi zitumike?
 
Kubenea naona kama anabweteka na popularity anayoip[ata sasa, kiasi kwamba hafanyi homework yake kabla hajaandika. Hii topic tumejadilia hapa kwa kirefu sana, na baadhi ya majibu yamepatikana. Hata hivyo, baadhi ya hoja zinamajibu kwenye mtiririko mzima wa issues leading to Anjouan troops build up. Kama angekuwa na nia ya kutupa uhondo ni kutafuta majibu ya maswali magumu yanayojitokeza kwenye issue, na si kurudia rudia yenye majibu tayari. Mfano:

1. Hivyo hakufanya makosa zaidi ya kukiuka taratibu. Ni dhahiri jambo hili linaweza kurekebishwa bila kutumia nguvu za kijeshi. Mara nyingi sana nguvu za kijeshi husababisha madhara makubwa.

Hajui kama hawa jamaa wamejaribu kuzungumza kwa zaidi ya miezi nane bila mafanikio?

2. Aidha, katika uchaguzi aliouitisha, ambao nchi washirika katika vita hiyo wanaupinga, Kanali Bacar alishinda kwa zaidi ya asilimia 85. Je, AU inapingana na matakwa ya wananchi wa Anjouan?

Uchaguzi ukifanywa Anjuan peke yake ni kuvunja muungano,unasahau kuwa Kisiwa hiki na vingine 2 ndiyo nchi ya Comoro? Seriali iliyopo madarakani Comoro ndiyo inapinga, na ndiyo imeomba msaada AU kama mwanachama hai wa jumuia.

3. Tujifunze Irak. Marekani ilivamia nchi hiyo mwaka 2003. Rais George Bush alijitapa kwamba vita hivyo vingechukua wiki chache sana, kutokana na alichosema "wananchi wa Irak wanaunga mkono kampeni za kumuondoa Saddam Hussein." Vita inaendelea hadi leo.

Kubenea, Comoro initiator wa vita ni serikali yao wenyewe, walichofanya ni kuomba msaada AU. Irak initiator wa vita ni foreigners...huoni kuna tofauti kubwa? Comoro wakiomba msaada AU, tusiwasaidie kwa kuogopa mfano wa USA na Iraq?

4. Je, kwa nini AU haukupeleka majeshi yake hapo kukikomboa kisiwa hicho kutoka mikononi mwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa?

Good, Je, unaweza kutueleza kama Serikali ya Comoro wakati huo iliomba msaada AU na ilikataliwa?

5. Ni jambo gani linaloisukuma Tanzania na washirika wake kuivamia Anjoaun wakati wananchi wa kisiwa hicho hawajalalamika kudhulumiwa, kuteswa na kunyanyaswa na Kanali Bacar?

Nani akawasemee wananchi hao kama wananyanyaswa, na wapi? after all, nchi imemegwa, what do you expect?

6. Kwa nini AU haijapeleka vikosi Zimbabwe kuwakomboa wananchi wanaoteseka chini ya mkono wa chuma wa Robert Mugabe?

hapa Unataka kusema legality ya Anjuan action itathibitishwa kuwa sahihi endapo tu AU itapeleka majeshi kwanza Zimbabwe? Duh wewe kiboko. Kama mwandishi, kwa nini usitoe mawazo mbadala unapoona mambo hayaendi sawa? Umespecialize criticism tu? SADC Ina tume ya Mbeki juu ya mzozo wa Zimbabwe, ingekuwa bora ungegusia failures za tume hii, badala ya proposal hii ya ajabu.

7. AU haikupaswa kukubali ombi la Rais Sambi la kupewa majeshi ili kumg'oa Bacar. Ingemshauri rais kuweka shinikizo kwa Kanali Bacar, kukubali kuitisha uchaguzi mwingine utakaosimamiwa na Jumuiya za Kimataifa. Na hili Kanali Bacar alilikubali.

Unajua kuwa amekubali last week baada ya kuona majeshi yanaenda, after 8 months of ignoring peace dialogue?

8. Kwa kujua hilo, Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, amepingana na wenzake katika utumiaji nguvu za kijeshi. Anaamini kwamba mgogoro huo unaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo.

Na kwa hiyo na wewe unaona kila anachofiri na kuamua Mbeki basi ni sahihi? Mbeki alihusika na peace dialogue muda wote huo na alikuwepo kwenye decision ya kutumia nguvu hadi last two weeks alipoandikiwa barua na Bacar kuomba asitolewe kinguvu. Yeye hapendi nguvu itumike, lakini maamuzi ya AU si lazima yafuate Mbeki anaema nini, kwa kuwa wanachama si Mbeki peke yake.

Pengine uchambue maamuzi ya AU kuivamia Comoro yamefikaje, badala ya kusema tu eti Mbeki alikataa.

Tunategemea MwanaHalisi liwe linaleta hoja nzito kama mfano wa mageuzi ya vyombo vya habari, hivyo kaza buti kaka.
 
Hii story ya Kubenea imeegemea upande mmoja, kwa nini asingeelezea mwanzo wa tukio zima mpaka juzi kwenye kikao cha AU ambacho kiliafikia nguvu za kijeshi zitumike?

Ndugu Icadon,

Hata mimi nimeshangaa sana kama Kubenea anaweza kufanya analysis ya namna hii kweli. Hajatutendea haki wasomaji wake.
 
Jamani wadau wa sheria naomba ufafanuzi
Je majeshi yetu kule Comoro yameenda kulinda amani au Kuvamia kijeshi??
Katiba inasemaje kuhusu kuvamia na kulinda amani??/
 
Kubenea analaumiwa na kuambiwa amevimba kichwa kwa umaarufu nikidhani ninyi mtakuja namaneno ya maana.

Utetezi huo hapo juu hauna chochote cha maana.

You are just hitting around the bush.

AU imeingilia mambo ya ndani ya Comoro kwa sababu Comoro ni nchi ndogo.

Sasa endapo Comoro itaomba msaada cuba au Venezuela na kukubaliwa na wa Cuba au Waven kujaa hapo tele hao wanajeshi wenu wa AU si watafyekwa kama nyasi?

Kwanza Wasouth tu wakitua na midege yao tu hpo hao AU soldier watafyata mikia yao kama vile vijibwa vya Mexico Chihuahua mbele ya dume la mbwa aina ya Grayhound.

Kuna sehemu kibao za kwenda kuingilia kati migogora barani Afrika lakini Comoro ndo imeonekana ni namba moja.

AU ni very weak inachagua Soft Target, kama AU ni Wanafyale wa Shoka waende wakamtie Jambajamba Mugabe kule Zimbabwe.

Hao wanajeshi wa AU uwepo wao Comoro ni sawa na majeshi ya kukodiwa MAMLUKI.
 
Ha ha that post is hilarious.....

Quick question serikali ya Zanzibar inatambulika AU?
 
Jamani wadau wa sheria naomba ufafanuzi
Je majeshi yetu kule Comoro yameenda kulinda amani au Kuvamia kijeshi??
Katiba inasemaje kuhusu kuvamia na kulinda amani??/

Msanii, mwanzo wa thread hii au ile nyingine inayofanana nayo (nani karuhusu jeshi kwenda Comoro) tumejadili sana hayo. Na vimeletwa vifungu vya katiba hapa kujibu maswali yako hayo. tafuta tu hiyo info.
 
Ha ha that post is hilarious.....

Quick question serikali ya Zanzibar inatambulika AU?

tatizo la post ya Madela kubwa, kwanza ni scenarios zake zote HAZIWEZEKANI!! pili, huwezi kufananisha tatizo la Zimbabwe na Comoro, hata Darfur hakuna anayesema kwamba iwe nchi huru.
leo tumeona Cyprus inazogea zaidi kuwa nchi moja....tumeona kilichotokea Kosovo pale ilipojitangazia uhuru wake. hata Tibet hakuna nayesema iwe nchi, ingawa kuna matatizo ya kijamaa yanayosababishwa na China ndani ya Tibet.
hapa kinachofanyika ni ku-discourage tabia ya kujitenga na kuanzisha vinchi visivyokuwa na mbele wala nyuma..........kwani utitiri wa vinchi hasa ktk Afrika ndio mwanzo wa economic and political stabilities zinazo likabiri bara letu.
mie sio shabiki wa mambo ya kijeshi kama haya, na pia siungi mkono kwa asilimia mia TZ kuwa Comoro...lakini nadhani mission hii ni halali kwa AU kushiriki!!.
 
Ha ha that post is hilarious.....

Quick question serikali ya Zanzibar inatambulika AU?

Ndugu, Icadon,

Zanzibar, kama ilivyo kwenye EAC, inangia kwenye AU as part of URT.

Nadhani unataka kulinganisha na Comnoro, bila shaka, ili Anjouan itambulike na AU lazima hatua nyingi za kisheria zifanywe katika kuuvunja muungano ule na Anjouan ibaki huru.
 
leo ni good friday, miaka kumi ilopita peace accord ilisainiwa Northern Ireland kubaki moja!!
Kanali Bacar, kapewa multiple chances za kumaliza hili suala mezani, lakini yeye kaleta kiburi kama cha Saddam. tena nadhani baada ya hili sakata wamtingishe kortini mjini Moroni au The Hague, na kama alishaga wahi kuawa watu basi kitanzi ni halali yeke........hatupo kwenye karne ya 14, hizi ni modern dayz na rule of international laws lazima zifuatwe!!! hii ni good advert kwamba AU ipo na ina meno!!
Vipi na itakuwaje siku kaka Sule(maada ya mafia) atakapojitangazia uhuru wa Mafia?? LOL
 
Ndugu, Icadon,

Zanzibar, kama ilivyo kwenye EAC, inangia kwenye AU as part of URT.

Nadhani unataka kulinganisha na Comnoro, bila shaka, ili Anjouan itambulike na AU lazima hatua nyingi za kisheria zifanywe katika kuuvunja muungano ule na Anjouan ibaki huru.

Ahsante kwa kujibu swali.. though ilikuwa ni rhetorical question

Kwa kifupi haya mambo ya kusema kwa nini AU haiendi Zimbabwe au mbona hatukwenda Kenya...ni baseless.

issue ya Nziwani ni very interesting walipojitenga mwaka 1997(kama sikosei) walitaka warudi kuwa chini ya Ufaransa kama ilivyo Mayotte, jamaa wakawachomolea..wakaamua kurudi kwenye shirikisho sasa naona jamaa kaamua kufanya madudu tena.
 
Quick question: Hivi ni kweli kuna wanajeshi wetu wamerudi maiti huko Comoro? au?

Ni uongo mtupu. Kungekuwa na uthibitisho tungekuwa tumewekewa. Mpaka leo tulichopata ni opinions za watu binafsi. Jamani tunaomba muweke uthibitisho wa mada hii please.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom