Jamani bado mnalivalia njuga hili swala?..
Nimeshasema kuwa Comoro ni sehemu ya Tanzania kwa kizazi..Tuna Watanzania kibao ndani ya serikali ya Comoro na wengine ni raia hapa kwetu tena naweza sema asilimia kubwa ya wananchi wazawa na wakazi wa Unguja ni Wakomoro.
hapana mkuu Comoro ni Comoro na Tanzania ni Tanzania, ni nchi mbili tofauti, masilahi ya comoro ni masilahi ya wanacomoro, na masilahi ya tanzania ni masilahi ya tanzania, kama tunasaidia basi tunasaidia kwa minajili ya kusaidia lakini si kwa sababu zozote zile zaidi ya nchi moja kuisaidia nyingine. kama kuna uhusiano wa damu uhusiano huo hauna tofauti na uhusiano wa watu wenyeji wa kagera na waganda, au wamakonde na watu wa msumbiji au wangoni na watu wa sauzi afrika. tunaunganishwa zaidi na uafrika wetu, lakini masilahi ya hizi nchi ni tofauti
Tulishawahi kuvunja mapinduzi kama hayo Komoro miaka ya Nyerere na leo hii ni marudio tu hawa jamaa kina Kanali Mohamed Bacar hawawezi kuingizwa ktk daraja la insurguency kwani sii wananchi wenyewe wanaotaka mapinduzi hayo ila kundi la wanajeshi mbuzi waliolewa madaraka kama Mugabe. Acheni vijana wapate mazoezi kidogo, miaka mingi imepita toka Uganda hatujaribu uwezo wa jeshi letu.
Ndugu Mkandara vita siyo lelemama, huwezi kuwatuma vijana bila sababu na dharura muhimu eti wakapate mazoezi, dhamana iliyo mikononi mwa Amiri jeshi mkuu ni dhamana nzito, maisha ya Askari ni muhimu sana kiasi kwamba si vyema kumtuma askari msitari wa mbele katika vita katili ili akafanye mazoezi tu bila ya sababu nzito ambayo hamna alternative tena isipokuwa kupigana tu. mtu kuwa askari ni pamoja na kujitolea maisha lakini huku ukitegemea maisha yako unayatoa kwa sababu iliyo ya muhimu sana.
Sii rahisi kuziona interest za Tanzania Komoro ikiwa huwezi kuona madhara mengi yatakayotokana na familia zilizopo hapa nchini kwetu. Komoro ni sawa na Israel kwa Marekani...kizuri chake kwa mlalahoi kama mimi siwezi kukiona
.
Hapana mkuu Comoro kwetu siyo sawa na Israel kwa Marekani,Comoro wana internal conflict wakati israel ina hostilities na mataifa ya kiarabu.jinsi ya kudeal na hizi conflicts ni tofauti
sababu nyingine ni kwamba Marekani asiposimama upande wa israel ujue mataifa ya Kiarabu yatawafanya kitu mbaya israel, human catastrophy itakuwa mbaya mno.
kitu kingine Israel sympathizers wa marekani ni nguvu kuu kuinfluence siasa za marekani, wanamiliki media, wanamiliki industries kibao zenye influence, kuna issue ya christianity in sympathy with israel. kwa hiyo mkuu sisi kama tunasaidia tusaidie tu lakini kusema tuna direct interest na comoro nadhani hakuna kitu cha namna hiyo
Trust me hadi leo sielewi kwa nini Marekani wanawalinda Israel kwa billions of dollar pamoja na silaha. Yawezekana mimi sii mwanasiasa kuweza kuona ndani.
je sisi tunayo mabilioni ya kufinance vita?.
je tungewapa serikali ya comoro vifaa vya vita kama vile vifaru,mabomu, bunduki tungekuwa hatujasaidia?. kwa nini tupeleke vijana wetu huko?,
je tungeendesha majadiliano ya kidiplomasia bila kuchoka tusingefaniukiwa au tulichoka kuwa na subira?. mimi ninadhani kama bacar angewekewa vikwazo juu ya vikwazo ingeweza kumleta katika makubaliano muhimu je tumechagua vita badala ya diplomasia?.