Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Status
Not open for further replies.
I mean with all due respect kwa mwanzishaji, lakini kama hakuna ushaidi au dataz zaidi ya tulizozisikia tayari basi hiii haifikii standard zetu hapa Jf kuwepo hapa,

Labda kina Mods, vipi hii nayo ikifuata mkondo wa kwenda inakostahili?
 
Msee ES,
kichwa cha habari cha hii mada kinaweza kuwa ni cha kizushi, lakini kwa mawazo yangu nadhani tumepata debate nzuri tu na kujifunza mengi juu ya Comoro, historia yake, ushiriki wa AU na jeshi letu ktk sakata hili. Hivyo basi, sidhani kama ni sahihi hii mada kuamishwa au kufanyiwa lolote zaidi ya kichwa cha habari kubadilishwa ili kiendane na ukweli wa mambo na contents zilizomo tayari ktk thread!!.
asante.
 
I mean with all due respect kwa mwanzishaji, lakini kama hakuna ushaidi au dataz zaidi ya tulizozisikia tayari basi hiii haifikii standard zetu hapa Jf kuwepo hapa,

Labda kina Mods, vipi hii nayo ikifuata mkondo wa kwenda inakostahili?

interesting....
 
Mkuu YRMN,

Basi kama ulivyoshauri, kichwa cha mada kibadilishwe maana hakiendani na context za mjadala, na kama ulivyosema ni kweli, ni very educative in some ways.

Ubadilishwe kichwa cha mada ikiwezekana.
 
Ni uongo mtupu. Kungekuwa na uthibitisho tungekuwa tumewekewa. Mpaka leo tulichopata ni opinions za watu binafsi. Jamani tunaomba muweke uthibitisho wa mada hii please.

NA NANI SERIKALI AU? MBONA HAMULIZI NI KIASI GANI KINATUMIKA PER DAY HUKO COMORO? NA TUSIDANGANYANE ETI AU WANATOA FUNDS NI OUNGO MTUPU KAMA WAMESHINDWA KUKODISHA HELICOPTER KULE DARFUR WHAT MAKES YOU THINK WATAKUWA NA PESA ZA KUONGOZA OPERATION KAMA ILE KULE COMORO?

AFRICAN UNION KILA UNAPOFIKA WAKATI WA HIYO PAN AFRICAN PARLIAMENT HUWA HAWANA PESA SASA LEO PESA ZA VITA ZIMEPATIKANA?

Quick question: Hivi ni kweli kuna wanajeshi wetu wamerudi maiti huko Comoro? au?

Hakuna taarifa yoyote inayoonyesha hilo, si kwenye local media si mitaani. Hata kama serikali ingeficha, baada ya muda wote huo kupita toka thread hii ianze, tungefahamu tu na kuona kama kweli kuna maiti zimerudi. High degrees of uzushi.
 
Mkuu GT,

Wewe umeshauliza ni kiasi gani kinatumika per day huko Comoro? let's share it then!
 
Quick question: Hivi ni kweli kuna wanajeshi wetu wamerudi maiti huko Comoro? au?

kuna wanajeshi wawili wamekufa week ago....nadhani inawezekana hawakufa kwa moto wa adui ndio maana kimya.....kuna some logistics zinaendelea na hadi sasa helicopter ya ufaransa pia imeanguka...kwa hali iliyo sasa na waandishi wameshapelekwa ..habari yoyote itakuwa rahisi kupatikana!
 
Jamani bado mnalivalia njuga hili swala?..
Nimeshasema kuwa Comoro ni sehemu ya Tanzania kwa kizazi..Tuna Watanzania kibao ndani ya serikali ya Comoro na wengine ni raia hapa kwetu tena naweza sema asilimia kubwa ya wananchi wazawa na wakazi wa Unguja ni Wakomoro.

hapana mkuu Comoro ni Comoro na Tanzania ni Tanzania, ni nchi mbili tofauti, masilahi ya comoro ni masilahi ya wanacomoro, na masilahi ya tanzania ni masilahi ya tanzania, kama tunasaidia basi tunasaidia kwa minajili ya kusaidia lakini si kwa sababu zozote zile zaidi ya nchi moja kuisaidia nyingine. kama kuna uhusiano wa damu uhusiano huo hauna tofauti na uhusiano wa watu wenyeji wa kagera na waganda, au wamakonde na watu wa msumbiji au wangoni na watu wa sauzi afrika. tunaunganishwa zaidi na uafrika wetu, lakini masilahi ya hizi nchi ni tofauti

Tulishawahi kuvunja mapinduzi kama hayo Komoro miaka ya Nyerere na leo hii ni marudio tu hawa jamaa kina Kanali Mohamed Bacar hawawezi kuingizwa ktk daraja la insurguency kwani sii wananchi wenyewe wanaotaka mapinduzi hayo ila kundi la wanajeshi mbuzi waliolewa madaraka kama Mugabe. Acheni vijana wapate mazoezi kidogo, miaka mingi imepita toka Uganda hatujaribu uwezo wa jeshi letu.

Ndugu Mkandara vita siyo lelemama, huwezi kuwatuma vijana bila sababu na dharura muhimu eti wakapate mazoezi, dhamana iliyo mikononi mwa Amiri jeshi mkuu ni dhamana nzito, maisha ya Askari ni muhimu sana kiasi kwamba si vyema kumtuma askari msitari wa mbele katika vita katili ili akafanye mazoezi tu bila ya sababu nzito ambayo hamna alternative tena isipokuwa kupigana tu. mtu kuwa askari ni pamoja na kujitolea maisha lakini huku ukitegemea maisha yako unayatoa kwa sababu iliyo ya muhimu sana.

Sii rahisi kuziona interest za Tanzania Komoro ikiwa huwezi kuona madhara mengi yatakayotokana na familia zilizopo hapa nchini kwetu. Komoro ni sawa na Israel kwa Marekani...kizuri chake kwa mlalahoi kama mimi siwezi kukiona
.
Hapana mkuu Comoro kwetu siyo sawa na Israel kwa Marekani,Comoro wana internal conflict wakati israel ina hostilities na mataifa ya kiarabu.jinsi ya kudeal na hizi conflicts ni tofauti

sababu nyingine ni kwamba Marekani asiposimama upande wa israel ujue mataifa ya Kiarabu yatawafanya kitu mbaya israel, human catastrophy itakuwa mbaya mno.

kitu kingine Israel sympathizers wa marekani ni nguvu kuu kuinfluence siasa za marekani, wanamiliki media, wanamiliki industries kibao zenye influence, kuna issue ya christianity in sympathy with israel. kwa hiyo mkuu sisi kama tunasaidia tusaidie tu lakini kusema tuna direct interest na comoro nadhani hakuna kitu cha namna hiyo

Trust me hadi leo sielewi kwa nini Marekani wanawalinda Israel kwa billions of dollar pamoja na silaha. Yawezekana mimi sii mwanasiasa kuweza kuona ndani.

je sisi tunayo mabilioni ya kufinance vita?.
je tungewapa serikali ya comoro vifaa vya vita kama vile vifaru,mabomu, bunduki tungekuwa hatujasaidia?. kwa nini tupeleke vijana wetu huko?,
je tungeendesha majadiliano ya kidiplomasia bila kuchoka tusingefaniukiwa au tulichoka kuwa na subira?. mimi ninadhani kama bacar angewekewa vikwazo juu ya vikwazo ingeweza kumleta katika makubaliano muhimu je tumechagua vita badala ya diplomasia?.
 
Mara ya mwisho Tanzani kwenda vitani ilikuwa 1979 na Uganda wengi wa wanajeshi wamestaafu!Acha hao waende Comoro angalau wakapate ujuzi wa vita!siyo siku mmoja tunavamiwa hapa wanajeshi wetu wanaanza kubabaika vitani!siku hiyo hakuna gamba la nyoka wala mamba watakuwepo!
 
kuna wanajeshi wawili wamekufa week ago....nadhani inawezekana hawakufa kwa moto wa adui ndio maana kimya.....kuna some logistics zinaendelea na hadi sasa helicopter ya ufaransa pia imeanguka...kwa hali iliyo sasa na waandishi wameshapelekwa ..habari yoyote itakuwa rahisi kupatikana!

hii helicopter ilicrash land Anjouan tarehe 19, wanajeshi wetu wameanza kuingia Fomboni tarehe 20, hawajaanza kwenda Anjouan.

610x.jpg

An Anjouan soldier loyal to rebel leader Col. Mohamed Bacar stands near part of the salvaged wreckage of a French helicopter that crash landed on the coast of Anjouan, Comoros, Wednesday March 19, 2008. Anjouan officials are investigating the crash, in which three occupants escaped with minor injuries. Bacar seized control of the island after disputed elections in July.
 
Be serious, Salim. hatutafuti vita kwa ajili ya mazoezi. Jaribu kuchambua possible reasons plz!
 
Mara ya mwisho Tanzani kwenda vitani ilikuwa 1979 na Uganda wengi wa wanajeshi wamestaafu!Acha hao waende Comoro angalau wakapate ujuzi wa vita!siyo siku mmoja tunavamiwa hapa wanajeshi wetu wanaanza kubabaika vitani!siku hiyo hakuna gamba la nyoka wala mamba watakuwepo!

Wow if we start using this as a reason to go to war we might as well support bush's war in Iraq and Afganistan...Watanzania tuache kulopoka lopoka..wengi hatujaona vita na hatutaki kuiona!!!..ngoja terrorists kutoka Comoro waaanze kujilipua Dar city centre hapo kama hatujaanza kulia..we should never involve ourselves in the affairs of others unless it affects our national interest..Kikwete amejimix anafikiri kuwa kiongozi AU maana yake Tanzania ndo leaders of Africa..(Je ghana imepeleka soldies Darfur NO! Kenya No! SoMALia No!..Kikwete dont save face with the west at Our Expense..Wazungu wanajua how corrupt ur govt is..wewe cheka cheka tuu kila kukicha..when they are done with you,,they will forget about you (Pray that Obama doesnt become the president of the US, Lazma akutupe he will see right through u!!) nchi kama South Africa zenye uwezo kijeshi na experience ya many wars wametulia and they chose diplomacy ndo sisi tunajifanya saviors?? Only time will tell..Once again Pole Kikwete...Get new advisors ASAP!!!!
 
Interest ya Tanzania Comoro ni nini? Je, hizo interest ni za mtu binafsi au kikundi cha watu?
Kama ni interest ya nchi kwa nini rais aliyepewa dhamana na kula kiapo kama amiri jeshi mkuu kwa nini hakuja yeye mwenyewe binafsi na kuwaambia Watanzania ambao ndio walipa kodi? Hiki kiburi cha kuwadharau walipa kodi kwa muda wote huu kinatoka wapi?

Je, ni sahihi waziri wa ulinzi na huyo wa foreign affairs kutangaza vita?

Jamani bado mnalivalia njuga hili swala?..
Nimeshasema kuwa Comoro ni sehemu ya Tanzania kwa kizazi..Tuna Watanzania kibao ndani ya serikali ya Comoro na wengine ni raia hapa kwetu tena naweza sema asilimia kubwa ya wananchi wazawa na wakazi wa Unguja ni Wakomoro.

Tulishawahi kuvunja mapinduzi kama hayo Komoro miaka ya Nyerere na leo hii ni marudio tu hawa jamaa kina Kanali Mohamed Bacar hawawezi kuingizwa ktk daraja la insurguency kwani sii wananchi wenyewe wanaotaka mapinduzi hayo ila kundi la wanajeshi mbuzi waliolewa madaraka kama Mugabe. Acheni vijana wapate mazoezi kidogo, miaka mingi imepita toka Uganda hatujaribu uwezo wa jeshi letu.

Sii rahisi kuziona interest za Tanzania Komoro ikiwa huwezi kuona madhara mengi yatakayotokana na familia zilizopo hapa nchini kwetu. Komoro ni sawa na Israel kwa Marekani...kizuri chake kwa mlalahoi kama mimi siwezi kukiona..
Trust me hadi leo sielewi kwa nini Marekani wanawalinda Israel kwa billions of dollar pamoja na silaha. Yawezekana mimi sii mwanasiasa kuweza kuona ndani.

Sasa rais yuko wapi aje atueleze hizo sababu nzuri kama peremende na sisi tuanze kulamba kabla ya kutatua matatizo kama haya hapa chini?

2943.jpg
 
Mojawapo ya mapungufu ya Katiba yetu katika vipengele nilivyoonesha ni kuwa hakuna jinsi ya moja kwa moja ya Bunge kusimamia deployment ya jeshi kwa kuhoji au kupinga maamuzi ya Rais.

Hatari yake ni kuwa Rais anaweza kuamuru Jeshi kwenda mahali popote alimradi si vitani na kufanya lolote lile bila kusimamiwa sana na Bunge. Binafsi naamini angalau Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge iwe consulted na wao waweze kushauriana na Rais kuhusu mikakati ya kutokea vinginevyo, tunaweza kujikuta yaliyowakuta Ethiopia kule Somalia, mambo ya Marekani Iraq na AFghanistan.
 
Mwanakijiji,

I couldn't agree with you more; you are right on the money . Wanabodi we must push for constitution amendment as soon as possible . Jamani hii constitution imempa Rais madaraka makubwa sana kwa hiyo ni lazima tuyapunguze .

Ni jambo la kushangaza kuona huyu Rais akideploy majeshi yetu kwenda Comoro bila hata ya kuwajulisha wananchi achilia mbali kuomba idhini ya bunge. Lakini wakati huo huo ajavunja katiba. Maswali yanayoniumiza kichwa ni nini haswa sisi wadanganyika tutabenefit tokana hii vita and how much have we spent so far ? Are we going to be reimbursed ?

Tatizo la viongzi wetu wanadhani wana uwezo mkubwa sana kuwafikiri na mara nyingi wana ignore mawazo ya wazalendo . Hivi watu wanajua kitu chochote kuhusu historia ? Wanajua jinsi vita vya Uganda vilivyotugharimu . Nakubalina na yule aliyesema ya kuwa JK anafikiri kuchaguliwa kwenye AU basi ndio ticket ya kutumia majeshi yetu afrika nzima . Na hawa viongozi wa afrika wana akili kweli ni vigezo gani wanatumia kuchagua Mwenyekiti wa AU? Utamchaguaje mtu ambaye 60% ya nchi yake hiko gizani aina umeme , what will he bring to the table?

Mr. President with all due respect I would like to remind you that charity begins at home . We have a lot of problems in our country that need serious attention to circumvent them ; I am urging you to redeploy our troops as soon as possible .
 
nchi kama South Africa zenye uwezo kijeshi na experience ya many wars wametulia and they chose diplomacy ndo sisi tunajifanya saviors?? Only time will tell..Once again Pole Kikwete...Get new advisors ASAP!!!!

The AU contact group consists of Libya, Senegal, South Africa, Sudan and Tanzania.

Hakuna taarifa yoyote inayoonyesha hilo, si kwenye local media si mitaani. Hata kama serikali ingeficha, baada ya muda wote huo kupita toka thread hii ianze, tungefahamu tu na kuona kama kweli kuna maiti zimerudi. High degrees of uzushi.

Nadhani tumeshasahau kuwa tuna wanajeshi wetu Lebanon, na hakuna anyehoji hali zao za usalama.
Hizo maiti zinaweza zikawa za wanajeshi wetu walioko popote duniani kwenye training sio lazima kutoka Comoro.
Operation yenyewe bado haijaanza, wamekufa kwa friendly fire au natural cause?

Binafsi naamini angalau Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge iwe consulted na wao waweze kushauriana na Rais kuhusu mikakati ya kutokea vinginevyo, tunaweza kujikuta yaliyowakuta Ethiopia kule Somalia, mambo ya Marekani Iraq na AFghanistan.

Maafikiano ya kutumia nguvu za kijeshi yalifikiwa February 20th kama sikosei, nataka kuamini kuwa toka siku hiyo mpaka siku ambayo majeshi yetu yameanza kwenda Comoro,wataku waliconsult na kamati ya Bunge. Lakini knowing how our Bunge functions mmmmh!!!
 
Wanajeshi wetu wakiwa kwenye Training, Fomboni March 22
610x.jpg

610x.jpg

610x.jpg

610x.jpg

610x.jpg

Wakisherekea baada ya mazoezi
610x.jpg

610x.jpg

610x.jpg
 
NA NANI SERIKALI AU? MBONA HAMULIZI NI KIASI GANI KINATUMIKA PER DAY HUKO COMORO? NA TUSIDANGANYANE ETI AU WANATOA FUNDS NI OUNGO MTUPU KAMA WAMESHINDWA KUKODISHA HELICOPTER KULE DARFUR WHAT MAKES YOU THINK WATAKUWA NA PESA ZA KUONGOZA OPERATION KAMA ILE KULE COMORO?

AFRICAN UNION KILA UNAPOFIKA WAKATI WA HIYO PAN AFRICAN PARLIAMENT HUWA HAWANA PESA SASA LEO PESA ZA VITA ZIMEPATIKANA?

GT, ndio maana nilianzisha thread ya Mercenaries kule (ikasogezwa sogezwa). Maana ukweli ni kwamba huyu jamaa anaweza kuondolewa at a lower cost.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom