Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Majeshi yetu Comoro: Who is responsible?

Status
Not open for further replies.
Hizi ni double standards za ajabu kabisa! Huko Zimbabwe Jongwe anafanza uchaguzi wa kiinimacho (ambao majeshi yanatangaza KABLA ya uchaguzi kuwa hayatakubali rais mwingine zaidi ya Jongwe), hakuna anayepeleka majeshi! Somalia, kwa miaka zaidi ya 15 hakuna serikali, ni mabwana wa vita (warlords) wanapokezana mji mkuu wa Mogadishu na hata nchi nzima imegawanyika kiwango kisichotawalika, OAU iliwaachia Marekani (ambao waliumbuliwa vibaya), na sasa uwepo wa majeshi ya AU hauonekani wala haieleweki kama nayo ni ajenda ya AU au la! Kule Togo kulikuwa na jamaa akiitwa Gnassingbe Eyadema, alipindua nchi akiwa na umri wa miaka 31, na akatawala kwa mkono wa chuma hadi alipojifia mwenyewe akiwa na umri wa miaka 69 baada ya kutawala miaka 38. Jeshi la nchi likamteua mwanawe Faure, kinyume kabisa na katiba na taratibu za utawala, kurithi urais wa baba yake. Hakuna AU iliyosema chochote! Nao pia wakafanya uchaguzi wa "danganya toto" (sawa tu na huo aliofanya Col Mohamed Bacar huko Anjuan, Comoro), lakini hakuna AU iliyoinua pua kusema kuna chochote kilichotokea, au kumtaka aachie ngazi! Na huyo Col Mohamed Bacar huko Comoro wala hajapindua serikali ya Comoro, amechukua madaraka na kuitisha uchaguzi katika kisiwa kimojawapo kinachounda shirikisho la Comoro (ambalo lina marais watatu kama sikosei, yeye ni mmojawapo kati ya hao watatu, tatizo ni kuwa serikali kuu haikubaliani na jinsi alivyopata madaraka). Sasa inaelekea "tunakaonea" haka ka-kisiwa, kiasi tunajua wapiganaji 1,800 (kama batallions 2 tu) wanatosha kuwafyatisha mkia. Bob Denard alikuwa anatumia wapiganaji 150 tu (hazifiki kombania 2) kusambaratisha visiwa vyote hivyo! Au kuna dili fulani jama hatuambiwi? Nani katoa dau hilo Col Bacar apigwe? Kinachonishangaza ni kuwa hata AU walipoamua kuwa inapaswa kupeleka jeshi Darfur, nchi nyingi zilizojitolea kupeleka majeshi zilikuwa zinasuasua kupeleka askari wao, wakidai wanasubiri kuhakikishiwa financing (hela haikuwepo!) Uganda walianza kujitolea kwa hela yao kabla hata fungu halijaingia kwa sababu zao za kiusalama na Sudan, wakatanguliza ndege moja na askari. Hizi hela za "fastafasta" za kuwahisha majeshi Comoro zimetoka wapi?
 
mna habari pia kama majeshi ya TZ yapo na Lebanon yanaweka amani? na huko pia wamekwenda kama UN peace keepers.
sasa hizo maiti aloziona PM uwanja wa ndege wa jeshi zaweza kuwa zinatoka huko pia.
 
mna habari pia kama majeshi ya TZ yapo na Lebanon yanaweka amani? na huko pia wamekwenda kama UN peace keepers.
sasa hizo maiti aloziona PM uwanja wa ndege wa jeshi zaweza kuwa zinatoka huko pia.

na kinyume chake
 
Hivi Comoro hakuna watanzania waliowekeza? Mbona watu wamekimbilia kupeleka majeshi haraka na kutoa kauli zenye nguvu na za kutisha?
 
comorro uwekeze nini? labda kwenye mashamba ya vanilla (joke)
 
..Askari waliotangulia Comoro walikwenda huko kulinda amani.

..Hawa wa sasa hivi wamekwenda kupigana vita kumuondoa Col.Bocar.

..Kwa mtizamo wangu Tanzania ni masikini mno kujishughulisha na masuala ya kivita. Haya majukumu ya kivita na kurejesha amani tuwaachie wenye uwezo.
 
Hivi Comoro hakuna watanzania waliowekeza? Mbona watu wamekimbilia kupeleka majeshi haraka na kutoa kauli zenye nguvu na za kutisha?

Mtanzania ninaemjua mimi aliyeekeza ni rais mstaafu wa Zanzibar "Comandoo" ana hoteli kubwa sana ya kitalii pengine kuliko Ngurdoto
 
Mtanzania ninaemjua mimi aliyeekeza ni rais mstaafu wa Zanzibar "Comandoo" ana hoteli kubwa sana ya kitalii pengine kuliko Ngurdoto

Niko Comoro naomba jina la Hotel ni visit nijionee tafadhali
 
..Askari waliotangulia Comoro walikwenda huko kulinda amani.

..Hawa wa sasa hivi wamekwenda kupigana vita kumuondoa Col.Bocar.

..Kwa mtizamo wangu Tanzania ni masikini mno kujishughulisha na masuala ya kivita. Haya majukumu ya kivita na kurejesha amani tuwaachie wenye uwezo.

Wenye uwezo akina nani?
Tumeambiwa France watasaidia Transportation na Logistics AU watatoa funds, uwezo gani unaouzungumzia kusafirisha wanajeshi kutoka kwenye kambi zao kwenda airport au kuwatengenezea combat mpya?
 
I am not a supporter of CCM and its government BECAUSE OF CORRUPTION AND MISMANAGEMENT. But credibility should be accorded where it is due. I fully support this mission huko Comoro. Hivi wananchi wenzangu mnaposema African problems for African solutions, mna maana gani? who are the Africans? au ulitegemea wazungu waje kufa huko eti wanapigania waafrica? Hii mission ina baraka zote za AU, TZ na wenzake hawajavamia illigally. So I think Membe is very right in what is doing as our foreign policy chief!

Mkuu Masanja,

Very strong argument, ingawa binafsi ninahitaji more facts kuhusu hii mission kwa ujumla, maana viongozi wetu wametufikisha mahali pagumu sana kuhusina n trust ya wanachokisema.
 
Labda kwanza tuwekane sawa, Tanzania haiko vitani, na naamini itakuwa vizuri kama Ofisi ya Rais au Membe, au mtu mmoja anayekumbuka wajibu wake kuwaambia wananchi kuwa hatuko vitani. Ili kutangaza vita Rais anaongozwa na Kifungu cha 44:1 cha katiba yetu kinachosema:

44.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali
ya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.
(2) Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala ya
tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya
kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani
ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha
mkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiria
kupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita
lililotolewa na Rais.
 
Labda kwanza tuwekane sawa, Tanzania haiko vitani,

Heshima mbele mkuu MMJ, kwanza hatuko vitani as a nation,

halafu iwapo tungekuwa vitani rais wa jamhuri angekuwa amekiuka hiki kifungu cha sheria, very simple and clear.
 
Heshima mbele mkuu MMJ, kwanza hatuko vitani as a nation,

halafu iwapo tungekuwa vitani rais wa jamhuri angekuwa amekiuka hiki kifungu cha sheria, very simple and clear.

exactly, sasa wengine wanaweza kuuliza sasa majeshi yetu yameenda kule kwa uwezo gani au amri ya nani hata kama ni ya AU kwani JWTZ haliko chini ya AU. Well, Jibu liko hapa kwenye Katiba:

148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
 
Now wait a minute, kama this is true then what is the fuss kwenye hii thread?

1. Kwanza ninataka kuamini kuwa majeshi yetu yameenda huko kama inavyosemwa hapa.

2. Ni kweli kuwa kuna wanajeshi wetu tayari wameanza kufa huko,

Mwisho mkuu wangu ninakushukuru kwa kuukata mzizi wa fitina, I mean kalas, ndio maana ninaipenda hii forums maana this is good stuff, yaani pure facts!
 
Mkjj ahsante kwa vifungu vya katiba,

So where is the beef?

kuna few scenarios ambazo zinaweza kumfanya JK apeleke majeshi kule,
-Kuhofia vita kutambaa kwenye visiwa vingine vinavyomake Comoro, by intervening and acting now itasaidia kuepukana na wimbi la wakimbizi pindi hali ikiwa mbaya.

-Aliombwa na Rais wa Comoro, ukiangalia historia inaonekana tunawasaidia sana hawa pindi kunapokuwa na machafuko.

-Kulinda interests za Tanzania kule(sizijui ni zipi na kama zipo).

-Ameact na kulead by example kama mwenyekiti wa AU.
 
Wakati mkitafuna kwanini Comoro, labda tusome wamarekani wanasema nini kuhusu Comoro.

Comor CIA Factbook

Nchi hii imepata coups kibao katika historia yake fupi.

Jinsi wanavyoelezea ni kwamba ni nchi moja masikini sana (ingawa mimi siamini). South Africa wanapinga mavamizi (why?). Basically, the jury is out kuhusu Comoro kunani. Kuna mtu hapo juu kaelezea kuhusu mchizi Denard aliyetaka kupindua nchi, huyu jamaa kafanya ushenzi wake hadi Benin.
 
comoros.gif

africa_small_map.jpg

Distance ni 692 kilometers, 430 miles na 373 nautical miles.

Ila ukisoma sana issue za Anjuoan ni ngumu maana mwaka 1997 walivyojitenga walitaka warudi kwenye utawala wa wafaransa kama ilivyo Mayotte lakini wafaransa wakawachomolea, mwaka 2002 wakarudi tena kwenye Union. US walifunga ubalozi wao Comoro tangu 1993 sijui kwa nini though.
 
Watanzania kwanza punguzeni woga! sasa hao maaskari wengine wa nchi zingine wanaokufa ktk mapambano je sii watu?

Ushupavu ktk jeshi ni kipimo cha uzalendo wetu!

Aluta Continua!

Kwa ushujaa huo wa kuto ogopa kufa unaonaje tukiivamia Kenya na kuongeza ukubwa wa mikoa ya Arusha Mara kilimanjaro na Tanga?
 
Kumbe Hauna source ya habari yako bana, sasa nishaelewa kwamba unadadisi habari kama ulivyosema ! keep it up !

Nimekuuliza source tu wewe unakuja na kashfa zako !

Haya mambo ya kuuliza Source ya kila kitu yanachekesha kweli.

Kwa udadisi huu mtu hata ukitwishwa matusi ya nguo na maneno mengi ya aibu utaendelea kuuliza source ya matusi.

Hapa JF kuna watu wasio hitaji source.

Pilot wa ndege ya Jeshi akitoa taarifa hapa kwamba maiti zimeanza kurudi yeye binafsi ni source.

Ukiendelea kung'ang'ania source atakupa namba ya simu ya mkononi ya Mkoloni Rostamu Azizi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom