Majeshi yetu yana Maoni gani kwenye Sakata la Bandari?

Majeshi yetu yana Maoni gani kwenye Sakata la Bandari?

Jeshi la Wananchi wa Tanzania..

Wanaangalia maslahi mapana ya watanzania na kuyalinda,kuyatekeleza..Wana viapo thabiti na uzalendo uliotukuka

JPM alitumia zaidi wanajeshi sababu ya nidhamu iliotukuka..
 
kama JPM ali kuwa makini wakati wa kujenga ikulu yetu ya Chamwino kwa kutumia jeshi kwa nini umakini uleule usitumike kwenye suala la bandari
Sasa jpm yupo muheshimiwa?. Jamaa alikuwa na mapungufu kweli yawezekana, lakini kwenye masuala kama haya alijitahidi sana. Naangalia jinsi alivyopambana na akina Barick, je wangelikuwa Hawa wangeweza kweli? Mkataba haujapelekwa bungeni lakini ushasainiwa na mkurugenzi wa bandari anajiumauma TU, maelezo yake hata hayaeleweki. Mara kilichosainiwa sio mkataba, mara bunge lisipouridhia hautakuwa mkataba. Yaani wananchi wote wametaharuki na hakuna kiongozi anayejaribu kuondoa sintofahamu hii.
 
Tupo katika kipindi ambacho ugaidi unakua na kusambaa na kushika taswira ya janga la kidunia.

Ni dhahiri kuwa ubinafsishwaji wa bandari unaweza kuwa na athari za Kiulinzi na za kiusalama kwa nchi yetu kwani itapunguza mamlaka za bandari hivyo hata uwezo wa ukaguzi wa shehena huwenda utapunguwa na baadaye inaweza kuwa mwiba mbavuni mwa majeshi yetu.

Je, maoni ya jeshi au majeshi ya nchi yetu ni yapi?!
Wameapa kuilinda katiba na kumtii Rais na Amiri Jeshi Mkuu ambaye ndiye Rais wa JMT. Uamuzi atakaotoa watautii!
 
Back
Top Bottom