Majeshi yetu yana Maoni gani kwenye Sakata la Bandari?

Jeshi la Wananchi wa Tanzania..

Wanaangalia maslahi mapana ya watanzania na kuyalinda,kuyatekeleza..Wana viapo thabiti na uzalendo uliotukuka

JPM alitumia zaidi wanajeshi sababu ya nidhamu iliotukuka..
 
kama JPM ali kuwa makini wakati wa kujenga ikulu yetu ya Chamwino kwa kutumia jeshi kwa nini umakini uleule usitumike kwenye suala la bandari
Sasa jpm yupo muheshimiwa?. Jamaa alikuwa na mapungufu kweli yawezekana, lakini kwenye masuala kama haya alijitahidi sana. Naangalia jinsi alivyopambana na akina Barick, je wangelikuwa Hawa wangeweza kweli? Mkataba haujapelekwa bungeni lakini ushasainiwa na mkurugenzi wa bandari anajiumauma TU, maelezo yake hata hayaeleweki. Mara kilichosainiwa sio mkataba, mara bunge lisipouridhia hautakuwa mkataba. Yaani wananchi wote wametaharuki na hakuna kiongozi anayejaribu kuondoa sintofahamu hii.
 
Wameapa kuilinda katiba na kumtii Rais na Amiri Jeshi Mkuu ambaye ndiye Rais wa JMT. Uamuzi atakaotoa watautii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…