KERO Maji machafu Stendi ya Mabasi Nyegezi - Mwanza yanahatarisha Afya za wasafiri

KERO Maji machafu Stendi ya Mabasi Nyegezi - Mwanza yanahatarisha Afya za wasafiri

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
289
Reaction score
415
NImeshangaa kusema ukweli, nilikua natoka kwenye pilikapilika zangu Mikoani, wakati nashuka Stendi kuu ya Mabasi ya Nyegezi nikakutana na harufu kali ambayo kimsingi haivumiliki.
kugeuka kushoto kulika nikakuta maji machafu yatokanayo na kinyesi yanatitirika bila wasiwasi ndani ya stendi hiyo kuu ya Mwanza ambayo ilitumia mabilioni ya fedha kukamilika.

Miundombinu ile kusema ukweli ni jambo la aibu kuona Stendi hata miaka mitano haina ila imeanza kuharibika, sikuishia hapo nikaanza kutembea nje kuona hali, kumbe, hata vyoo vya nje navyo vimeanza kutiririsha maji machafu kwahivyo ni Aibu maji machafu ya Chooni kutitirika Stendi ya Mabasi ya Nyegezi wahusika wachukue hatua kabla ya Kipindupindu hakijawamaliza watu na wasafiri.

Maana ukiangalia mule ndani kuna vyakula vinauzwa, hapo Kipindupindu kinaepukwaje? Kuna Maduka mbalimbali, hapo watu wakianza kuhara itakuwaje?
20250420_145003.jpg

20250420_145022.jpg

20250420_145009.jpg

20250420_145043.jpg
 
Back
Top Bottom