- Thread starter
- #21
Jamaa hapo anafikiri ni sababu kama za akina DAWASCO.
Mito yetu inapokauka kutokana na ukame kukithiri umeme hukatika.
Na huko Texas pia hali ya hewa imesababisha kukatika kwa maji na umeme.
Yote haya ni mabadiliko ya tabia nchi.
Lakini huwa kuna uzembe pia, iwe hapa kwetu au huko mkoani Texas, Marekani.
Bwana Bill Gates, mwanaharakati wa kimazingira wa mabadiliko ya tabia, nchi amepinga vikali visingizio vya hali mbaya ya hewa mkoani Texas akidai kwamba mikoa kama Iowa mbapo kuna baridi zaidi na kwa muda mrefu umeme wala maji havikatiki.
Bwana Gates alihoji ni kwa nini miundombinu ya huduma hizo, kama vile mapangaboi ya kufua imeme, haigandi theluji mkoani Iowa.