Maji nayo yakatika mkoani Texas, Marekani, wananchi Wachota barafu kwa matumizi

Tatizo la Tanganyika ni genge mbogamboga
..Malaysia walipata uhuru 1963.

..Singapore walipata uhuru 1965 baada ya kujitenga na Malaysia.

..Nchi hizo zimepata maendeleo makubwa kuliko Tanganyika iliyopata uhuru 1961.
 
Texas siyo mkoa ni Nchi Kama ilivyo Tanganyika sawa dogo acha kuharibu kwa kuifananisha Texas na mkoa
Nchi ni USA Texas ni jimbo ambalo kwa Kwetu ni kama mkoa tu kwa hadhi achana na swala la ukubwa
 
Huwa mnamchagua mkuu wenu wa mkoa? Mkuu wenu wa mkoa anaweza kuteua majaji? Anaweza kutoa amri ya lockdown au kutangaza hali ya hatari bila idhini ya Rais?
Mkuu wenu wa mkoa anaweza kusamehe wafungwa?
Kwenu kuna mikoa yenye mamlaka ya kutunga sheria zake za kodi na kujikusanyia kodi zake yenyewe?
Mikoa yenu ina majeshi yake yake ya kimkoa?
Mikoa yenu inaweza kujitungia sheria zake za uchaguzi tofauti na mkoa mwingine?
Nchi ni USA Texas ni jimbo ambalo kwa Kwetu ni kama mkoa tu kwa hadhi achana na swala la ukubwa
 
Kajifunze kwanza maana ya STATE halafu uelewe maana ya United STATES of America kama hujaja kufuta huu upupu wako hapa.
Nchi ni USA Texas ni jimbo ambalo kwa Kwetu ni kama mkoa tu kwa hadhi achana na swala la ukubwa
 
Beberu ni mtu mzuri tu,ila haya maviongozi yetu ndo yana shida..
Yaani kama chance ipo,hii afrika si sehemu salama kuishi
 
Ingekuwa Afrika ingewekwa front na media za kimataifa na kila dakika breaking news
 
Kumbe shida yenu ni aina ya beberu. Chanjo za ndui, polio tetekuwanga na kifua kikuu ni kutoka kwa beberu la kizungu, tena mama yako hakutoa hata senti tano. Sema asante kubwa zaidi kwa beberu la kizungu maana bila hilo kama hata ungefanikiwa kuvuka miaka mitano huenda vidole vingekuwa haviwezi kuingia JF kutapika unayaandika sasa.
Ya beberu la kichina mkuu sio la Marekani apa nina sema asante mchina
 
Media za kimataifa ni zipi kwako au unafikiri hiyo taarifa imekufikia kupitia wasafi TV?
Ingekuwa Afrika ingewekwa front na media za kimataifa na kila dakika breaking news
 
Media za kimataifa ni zipi kwako au unafikiri hiyo taarifa imekufikia kupitia wasafi TV?
Hoja yangu Afrika wanaangazia zaidi matatizo yetu, umaskini, picha zisizo na matumaini, njaa, Magonjwa, mafuriko...mbona BBC , CNN hawaripoti tukio hili, karibia wiki Texas hali ni hiyo
 
Usikaririshwe mambo kama mbumbumbu. Kwa hiyo ukiingia YouTube sasa hivi huwezi kuikuta kumbukumbu ya hii taarifa kutoka BBC na CNN?
Kuna tukio limekua na coverage kubwa zaidi katika vyombo vikubwa vya Marekani na dunia nzima kwa wiki hii zaidi ya hilo janga la theluji Texas?
Halafu kwa nini unataka kufananisha umaskini, njaa, magonjwa na mafuriko ambayo ni mambo yanajirudia kila mara na binadamu wanaojielewa wanawaza kuweka mipango ya kuzuia dhidi ya Tukio kama la Texas ambalo ni janga lisilotarajiwa?
Hoja yangu Afrika wanaangazia zaidi matatizo yetu, umaskini, picha zisizo na matumaini, njaa, Magonjwa, mafuriko...mbona BBC , CNN hawaripoti tukio hili, karibia wiki Texas hali ni hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…