Maji ni huduma ambayo Serikali inafeli vibaya mno, uhaba na mgao karibu kila mkoa japo mabilioni yanatumika. Rais Samia anashindwa wapi?

Nadhani kuna tozo pia ikiwa unavuna maji ya mvua utafikiri yametoka serikalini 🀣🀣🀣🀣
Hawa wangekuwepo kwenye ile vita ya Maji Maji wangewatoza Wazee wetu kwa kutumia jina la Maji tu.πŸ˜†πŸ˜‚
 
Hawa wangekuwepo kwenye ile vita ya Maji Maji wangewatoza Wazee wetu kwa kutumia jina la Maji tu.πŸ˜†πŸ˜‚
Aaah, machifu wetu hawakuwa na V-8, kwa hiyo enzi hizo ukiwapa kuku mmoja ni tozo tosha kabisa!
 
Pale wao Idara za Maji zinaposhindwa jukumu lao sisi ndio tufe kwa kiu? au tusioge tuwe kama Wachawi?

Kuna kipindi nilikuwa naishi Mkoa fulani Maji yalikuwa hayatoki kabisa na bili wanakuletea tumenyanyasika sana kwenye Nchi yetu.
 
Tena Bora na Rais Samia kafanya uwekezaji mkubwa kiasi kwenye hii sekta maana waliopita walipuuza kabisa sekta ya Maji na kilimo..

Mwaka ukiopita mvua ilikuwa kidogo ni automatically maji itakuwa tatizo maana hata visima vyetu vya majumbani maji yamekauka au kupungua Sana..

Mwisho tatizo la maji haliwezi kutatuliwa overnight bali kwa uwekezaji ambao utachukua mda fulani..

Kwa sasa Nina matumaini maana naona serikali inajaribu kuchukua hatua za kuwa na suluhisho la kudumu na kusema ukweli miradi ya maji Kwa sasa ni countless si Vijijini si mjini..

Kwa ishu ya Maji nadhani Rais Samia ataimaliza kwa sababu ni moja ya kipaombele chake na anatakiwa asifanye mchezo maana huko ndiko kuna wanawake wenzie ambao wanaweza mhakikishia Kura kama akiwatua ndio kichwani..
 
Samia hajawahi kuweza sababu anarembua rembua tu badala ya kuwajibisha watu...
 
Sisi upinzani tunasema.
UKIONA ADUI YAKO ANAFANYA MAKOSA YA KIJINGA.
USIMSTUE
 
KWANI RIPOTI YA KIKOSI KAZI HAIJATOA MAPENDEKEZO JUU YA MAJI?
 
Oyaaa, tupeni maji, hatujaoga wiki mbili sasa na tunafanya kazi maji machafu! Kula urefu wa kamba yako sio kwa watu wa maji machafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…