Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
Ndugu wanajamii, kuna utofauti upi wa kiimani Kati ya maji ya "baraka " na maji "ya upako"?

Je, tofauti pekee ni, yale mengine kuuzwa? Au kuna tofauti zingine za ziada?

Je, mkate wa Bwana na keki ya upako Vina tofauti gani?

Nashawishika kuamini kuwa bulldozer ana"copy" vitu upande wa "kanisa katoliki" na kuvi"modifai".

Je kuna uhusiano upi hapo juu?

Nawakaribisha wajuzi wa mambo watudadavulie!
 
Kikubwa imani yako tu ... hata maji ya kawaida wewe mwenyewe waweza yabariki na kuyatumia
Kuhusu mkate na mafuta.

Utofauti upo mkubwa sana (Utaratibu mzima wa ibada husika na mamlaka alonayo padre katika kuendesha ibada)
 
Kuna utofauti mkubwa sana Bwaaa shekhe.

1. Maji ya Baraka hayauzwi ili hali yale ya upako yanauzwa.

2. Maji ya Baraka sio mali ya mtu, ili hali yale ya upako ni mali ya Mwamposa.

3. Maji ya Baraka yana nguvu ya Mungu, ili hali yale ya Upako hayana nguvu ya Mungu bali binadamu na ndio Maana yanauzwa.

Kuhusu Sakramenti na vimikate vingine.

1. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni mwili kweli na damu kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo, ili hali Mikate hiyo mingine ni Mikate tu kama Mikate.

2. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu inatupa Uzima wa Milele, Wakati Mikate hiyo mingine haina uwezo huo.

3. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni Kwaajili ya Wakristo Wakatoliki, tena waliojiandaa yaani wamejitakasa kwa toba na matendo mema, ili hali Mikate hiyo mingine inaliwa na yeyote bila kujali dini yake wala hali yake Kiroho.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Yote ni fake, Sema ya bulldozer ni fake zaidi maana yanauzwa waziwazi.
Kwa bulldozer maji sio lazima ununue hata ya nyumbani na mafuta ya nyumbani hujalazimishwa kununua ni kuwa na imani tu.

kwahiyo mkuu maji ya chimbwe yatibiwe yawe na ubora wafanyakazi walipwe mabobo yatengenezwe , usafiri umeme, label halafu upewe bure.

Yeye atakuwa analima wapi hizo hela.
 
kwa bulldozer maji sio lazima ununue ata ya nyumbani na mafuta ya nyumbani hujalazimishwa kununua ni kuwa na imani tuu.

kwaiyoo mkuu maji ya chimbwe yatibiwe yawe na ubora wafanyakazi walipwe mabobo yatengenezwe , usafiri umeme, label alafu upewe bure. yeye atakuwa analima wapi hizoo hela.
Kwahiyo Bulldozer anatatua changamoto ya uhaba wa maji nchini?

Yule ni Mganga mvaa suit!!!
 
Nimecheka sana,Kwa hiyo kwa Mungu tutakuwa tunakula mkate wa uzima na damu ya Yesu?
 
Kuombewa katoliki na kuombewa kawe Nini tofaut ukipata jibu umepata majibu
 
Back
Top Bottom