Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Maji ya baraka ya (RC) vs maji ya upako ya (Mwamposa)

Mtume Meshach wa UKWELI ministry, Amiel Katelela, Mwakasege, Mch Misholi, Mch Maghembe, Askofu Gwajima, Mch Gamanywa , nk nk.

Pia usisubiri kutajiwa, wapo wengi, Muulize Roho mtakatifu atathibitisha.
Unatumia kigezo kipi?
 
Kuhani na Mwalimu Musa Mwacha...

Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu...

Vifaa vyake vinaitwa vitakatifu au vya kiroho...

Kuna maji, mafuta nk...

Tuanze na maji, yapo ya aina nyingi...

Maji ya mfuniko mweupe ndio maji yanayofichua vilivyosirini ila ukiamini kwa jina la YESU utapata majibu...
 
Kuhani na Mwalimu Musa Mwacha...

Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu...

Vifaa vyake vinaitwa vitakatifu au vya kiroho...

Kuna maji, mafuta nk...

Tuanze na maji, yapo ya aina nyingi...

Maji ya mfuniko mweupe ndio maji yanayofichua vilivyosirini ila ukiamini kwa jina la YESU utapata majibu...
😂 Donatila Kulingana na biblia, huo wadhifa wa mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni Yesu Kristo je, Kuhani Musa anakaimu au vipi?
 
[emoji23] Donatila Kulingana na biblia, huo wadhifa wa mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni Yesu Kristo je, Kuhani Musa anakaimu au vipi?
YESU ni Kuhani Mkuu...

Sipendi kuwasema wapakwa mafuta wa Bwana, ila kifupi tu Kuhani Musa ni mtumishi anayetumiwa na Bwana...

Namshukuru Mungu hata mimi kwa kupitia mafundisho ya neno la Mungu kwa Kuhani Musa nimekuwa na nguvu za Rohoni...

Ninaouwezo wa kujua kuwa mtumishi huyu ni wa Bwana kwa kupitia Roho Mtakatifu..

Na mambo yajayo...

Bwana YESU atukuzwe
 
Maji ya baraka unayanunua kwa sadaka, zaka unazotoa. Biashara ni ile ile sawa na Mwamposa.
 
Nyie mnaofananisha uganga wa buldoza na kanisa katoloki ni kama kufananisha kifo na usingizi
 
Ndugu wanajamii, kuna utofauti upi wa kiimani Kati ya maji ya "baraka " na maji "ya upako"?

Je tofauti pekee ni, yale mengine kuuzwa? Au kuna tofauti zingine za ziada. Je, mkate wa Bwana na keki ya upako Vina tofauti gani?

Nashawishika kuamini kuwa bulldozer ana"copy" vitu upande wa "kanisa katoliki" na kuvi"modifai".Je kuna uhusiano upi hapo juu?

Nawakaribisha wajuzi wa mambo watudadavulie!
Wanao tumia ndio wanajua nguvu ya hayo maji na keki za upako

tofauti ipo
 
Kuna utofauti mkubwa sana Bwaaa shekhe,
1.Maji ya Baraka hayauzwi ili hali yale ya upako yanauzwa.
2.Maji ya Baraka sio mali ya mtu,ili hali yale ya upako ni mali ya Mwamposa.
3.Maji ya Baraka yana nguvu ya Mungu,ili hali yale ya Upako hayana nguvu ya Mungu bali binadamu na ndio Maana yanauzwa.

Kuhusu Sakramenti na vimikate vingine
1.Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni mwili kweli na damu kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo,ili hali Mikate hiyo mingine ni Mikate tu km Mikate.
2.Sakramenti ya Ekaristi Takatifu inatupa Uzima wa Milele,Wakati Mikate hiyo mingine haina uwezo huo.
3.Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni Kwaajili ya Wakristo Wakatoliki,tena waliojiandaa yaani wamejitakasa kwa toba,na matendo mema,ili hali Mikate hiyo mingine inaliwa na yeyote bila kujali dini yake wala hali yake Kiroho.


Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
Mi ni mkristo ila nimecheka jinsi ambavyo hukuzingatia mafundisho ya kipaimara.Eti damu kweli na mwili kweli!!!! Mwenyewe Aliumega Mkate akawapa akisema.....fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
Ule ni mfano wa kukumbuka.Tungekuwa tunakula mwili wake wa ukweli tangu enzi hizo si huo mwili ungekuwa umeisha? Kha!
 
Back
Top Bottom