Kuna utofauti mkubwa sana Bwaaa shekhe.
1. Maji ya Baraka hayauzwi ili hali yale ya upako yanauzwa.
2. Maji ya Baraka sio mali ya mtu, ili hali yale ya upako ni mali ya Mwamposa.
3. Maji ya Baraka yana nguvu ya Mungu, ili hali yale ya Upako hayana nguvu ya Mungu bali binadamu na ndio Maana yanauzwa.
Kuhusu Sakramenti na vimikate vingine.
1. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni mwili kweli na damu kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo, ili hali Mikate hiyo mingine ni Mikate tu kama Mikate.
2. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu inatupa Uzima wa Milele, Wakati Mikate hiyo mingine haina uwezo huo.
3. Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni Kwaajili ya Wakristo Wakatoliki, tena waliojiandaa yaani wamejitakasa kwa toba na matendo mema, ili hali Mikate hiyo mingine inaliwa na yeyote bila kujali dini yake wala hali yake Kiroho.
Sent from my V1901A using
JamiiForums mobile app