kama unadhani kuna gharika ilitokea jiulize maswali haya.
1. maji yalitoka wapi na yalikwenda wapi baada ya gharika
2. wanyama walikuwa wanakula nini ndani ya safina
3. nani alianza kuwasambaza tena wanyama baada ya safina kwenda maeneo mbalimbali ya dunia
4. kuna wanyama ambao hawawezi ishi kabisa mashariki ya kati kama polar bears nuhu aliwezaje ishi nao
nitaongeza mengine badae
Ukitaka kujua uwezo wa watu kufikiri wewe soma tu mada kama hizi ndipo utaweza kushangaa sana....
Mtu anahoji jambo lililotokea miaka maelfu huko utadhani limetokea mwaka jana. hivi ni kweli hatujui kabisa kuwa kulikuwa na tofauti kubwa sana ya kimazingira na hali ya hewa kipindi kile na leo?
Hata hivyo,unapohoji na kujibu masuala ya ki-Biblia unapaswa ufikirie kwa namna ambayo siyo sawa na hii ambayo unaifikiria kwenye aisha ya kawaida kwasababu kuna mambo yaliyoko kwenye biblia ambayo hayawezekaniki kwa namna ya kawaida kwasababu mtendaji hafungwi na kanuni zinazokufunga wewe....
Sasa kama mtu anahoji namna wanyama wanaoishi kwenye mazingira fulani kuweza kuishi kwenye safina ambayo haina mazingira hayo huyo ni moja kwa moja anafungwa na kanuni ambazo aliyewafanya wanyama hao wakaishi kwenye safina hafungwi nazo....
Hilo ni sawa na kuhoji walichokuwa wanakula wanyama siku zote,yaani ni kichekesho kikubwa kabisa....
Hujui tu kuwa kuna mwanamama mmoja alitumia unga kidogo sana aliokuwa nao bila kuisha kwa siku mingi tu,jambo ambalo haliwezekaniki kwa akili zako za kawaida ambazo kwa kiwango kikubwa zimejengwa na mazingira na jamii yako na hivyo kuzifanya kuwa ziyo zako.....
Tunashindwa kuelewa hata mambo madogo kama haya,inasikitisha sana....