Loftins
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 10,485
- 13,693
Wewe hata hujielewi.Hapo bado balaa la HILL WATER (sitangazii biashara) hajaingia rasmi huko Kaskazini, japo bado kwa Dar bado demand yake inakuwa kubwa sana mpaka sometimes yanakosekana baadhi ya sehemu, mfano LITA 1.5 NI adimu nayo huuzwa Tsh 600-700 hadi 1000 kwa sehemu zingine
KILIMANJARO acha apigwe tu, amebweteka sana pamoja na malalamiko ya watumiaji basi akajikuta ni PREMIUM sana sasa WATERCOM anayezalisha maji ya Afya acha ateke soko tu ni haki yake
Halafu mmegundua kitu siku hizi Maji ya kilimanjaro yanatangazwa Azam ambako kuna maji ya Uhai? Niliona hilo Tangazo kwenye channel za Azam Nikashtuka kwa sababu nimezoea kuliona ITV sanasana
KILIMANJARO Acha apumulie mipira tu, so far kwangu AFYA, HILL na Uhai ndio maji ya chaguo langu
Hiyo Hill water kupatikana kwake tu ni tatizo ndio aje amsumbue Kilimanjaro ambaye ni sehemu ya Cocacola?
Afya kanda ya kati na ziwa haitumiwi sana kama ilivyo Kili na maji mengine, Uhai kwa dodoma hapa yanauzwa 300 yes mia 3 hii sio bei ya jumla ni rejareja kwa wanaotembeza.
Nyanda za juu Afya amewashinda wengine wote na wana maji yao mfano Mkwawa na ya kutoka Njombe nimeyasahau jina ndio washindani wake