DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wote waongo hao na huyo vice president

Tunajua tatizo la saratani linasababishwa na kemikali za migodini zinazoelekezwa kwenye maji.
Unajua au unapiga ramli? Ni kemikali gani zinatumika migodini? Katika hizo kemikali ni zipi ambazo ni carcinogenic?
 
Tatizo unazungumzia nadharia na siyo uhalisia.

Muuzaji wa samaki akiwa na samaki wake, hawi na uhakika samaki wake atanunuliwa siku hiyo au keshokutwa, au hata baada ya siku kadhaa. Hivyo anamwekea dawa, au kumtunza kwenye barafu ili asiharibike, na ili asipate hasara.

Siyo kweli kuwa samaki wote wanapovuliwa, hununuliwa siku hiyo hiyo. Kuna mtu ninayemfahamu, ambaye alikuwa anafanya biashara ya kununua samaki toka kwa wavuvi na kupeleka kiwandani, kuna wakati alikuwa akikaa na samaki hata wiki zima, kabla ya samaki wake kununuliwa na kiwanda. Na hiyo ilikuwa inatokea pale ambapo wamepatikana samaki wengi maeneo mbalimbali.

Tusiwe wabishi. Yawezekana siyo maji ya maiti au dawa za kutunzia maiti, lakini kuna mbinu mbalimbali zinazotumika kuwafanya samaki wasiharibike kabla ya kumfikia mlaji, na nyingine siyo salama kabisa kiafya.
Na hapa ndo utafiti au uchunguzi wa kina unatakiwa kufanyika, huenda hayo maji ya maiti ni mbinu ya kishirikina kuwafanya hao samaki wasiharibike, ndo maana VP amesema kwa sababu yeye ana vyanzo vingi vya taarifa..
 
Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa zinadai, fedha hizo zilikuwa zikitolewa na Katibu wa mkuu wa mkoa, bwana Matia Levi.

Inaelezwa zaidi ya waandishi 20 walipokea mshiko huo ili habari hiyo isiandikwe, lakini waandishi walipokea na kutoa habari hiyo.

Hata hivyo Leo mchana, Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa hiyo na inaelezwa wamesikitishwa na kauli ya Makamu wa Rais.
Hawataki ukweli usemwe
Ndiyo maana hawakutimiza wajibu wao kuwakamata wahusika
 
Naomba kufunzwa hapa, maji ya kuoshea maiti ni maji gani na yamekaaje kaaje? Mimi nilidhani maiti anakoshewa maji haya haya ya kawaida tu!!!
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa Saratani wamekuwa wakitokea Kanda ya Ziwa jambo ambalo linapelekea Serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini Kanda ya Ziwa?

Jana nimeona Mh Makamu wa Rais akiwa hospitali ya Bugando ameeleza moja ya sababu inayopelekea takwimu za saratani kuwa juu Kanda ya Ziwa ni watu wanaotumia maji ya kuoshea maiti kuhifadhia samaki.

Nimeona niijulishe Serikali kwamba moja ya wateja wakubwa wa maji haya ni waganga wa kienyeji na maji haya yanauzwa kwenye maduka ya dawa asili.

Ili Serikali ifanikiwe kudhibiti usambaaji wa biashara hii nashauri wahakikishe masoko yote pamoja na mochwari ambapo ndipo yanapotoka wanadhibiti vinginevyo tatizo hili litaendelea.

Asante.
---

Kauli Makamu wa Rais kuhusu maji ya kuoshea maiti Kusababisha kansa

View attachment 2356409
Picha: Sehemu ya gazeti iliyoandika habari hii

Baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Phillip Mpango amesema ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani katika mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na baadhi ya watu kutumia maji ya yanayotumika kuoshea maiti pamoja na dawa aina ya Cloroform inayotumika kuhifadhi samaki.

DK. Mpango alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa saratani katika huspitali ya rufani ya kanda Bugando jijini Mwanza, jengo ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.6.

Baada ya kauli hiyo, inadaiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jana jioni ilianza kugawa fedha kwa waandishi wa habari kuzuia stori hiyo isitoke kwenye vyombo vya habari.

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa zinadai, fedha hizo zilikuwa zikitolewa na Katibu wa mkuu wa mkoa, bwana Matia Levi.

Inaelezwa zaidi ya waandishi 20 walipokea mshiko huo ili habari hiyo isiandikwe, lakini waandishi walipokea na kutoa habari hiyo.

Hata hivyo Leo mchana, Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa hiyo na inaelezwa wamesikitishwa na kauli ya Makamu wa Rais.
 
Kumbe ndo maana samaki wamenenepa sana kumbe ni virutubisho kutoka maiti.
 
Back
Top Bottom