Maji ya ziwa Viktoria yavamia makazi Lamadi, kaya 400 hazina pa kwenda

Maji ya ziwa Viktoria yavamia makazi Lamadi, kaya 400 hazina pa kwenda

hapo ni makazi ndio yalivamia maji ya ziwa victoria.
Nature always run it course the tide is rising wit the moon,
It only take a spark to put a fyah to da fume,
What is hidden in the dark shall be revealed so very soon,
Tell Pharoah free the prisoners from the dungeon an the doom,
Majanga yanapunguza Kasi ya "kuupiga mwingi"!!
 
Ikiwa kaya Moja Ina wastani wa watu watano, kaya 400 , ni sawa na nyumba 80.

Msaada wa haraka unahitajika.
 
Water current
Pana mchoro au ukomo/ mipaka wa maji na ardhi ambao tunaweza kuhesabu zinapoanzia hizo MITA 1-60?

Yaani mipaka/ ukomo wa maji ya ziwa ni upi?

Maana unaweza kuhesabu 60 m Leo, baada ya wiki, maji yataongezeka MITA 2, hizo MITA 60 vipi hapo?
 
Kumbuka ni mita 60 kutokea pale ambapo maji ya mvua za Elnino yaliishia.
Sasa hapajawahi kufanyika jitiada za kuweka alama kuonyesha kuwa, hapa ndipo ukomo wa mvua za er nino.

Serikali Huwa Ina kawaida ya kukwepa kuwajibika Kwa kusema wananchi wamevamia.

Usiuingie huo mkumbo.

Anyway, tufanye sasa wananchi wamevamia, ubinadamu ni upi sasa, Hawana makazi na AFYA zao ziko hatarini KAZI ya Serikali ni ipi hapo?
 
Pana mchoro au ukomo/ mipaka wa maji na ardhi ambao tunaweza kuhesabu zinapoanzia hizo MITA 1-60?

Yaani mipaka/ ukomo wa maji ya ziwa ni upi?

Maana unaweza kuhesabu 60 m Leo, baada ya wiki, maji yataongezeka MITA 2, hizo MITA 60 vipi hapo?
Elimu kama hizi kwa dunia ya sasa inatakiwa zianzie shuleni. Harafu watu wanaimbiwa tu mita 60 bila kutofautishiwa mazingira. Kuna wakati mtu anaweza jenga umbali wa mita 5 tu kutoka ufukweni asivamiwe na maji ila mtu akajenga mita 200 kutoka ufukwe ukavamiwa na maji. Hiyo inatokana na ukubwa wa mwinuko kutoka usawa wa maji. Kwa mazingira ya lamadi ziwa likiongezeka kina kwa fut 1 tu mamia ya watu wanayakimbia makazi yao wakati maeneo mengine hata maji yakiongezeka kina kwa mita 3 watu hawana hata habari nayo
 
Hatari man! Omba isikupate hii unaweza kudata akili aisee...
Bora mto linaweza kuwa tukio la siku tu lakini ziwa inawezakuwa ndo maisha. Katika takwimu zinaonyesha kwamba ziwa victoria linakuwa kila kunapokucha
 
Salaam,shalom,

Mvua kubwa zilizonyesha nchini zimeanza kuleta madhara makubwa Kwa nyumba na makazi ya watu waishio kandokando mwa ziwa Hilo.

Imeripotiwa kuwa, kaya zaidi ya 400 hazina makazi wilayani Busega, Lamadi kutokana na maji ya ziwa kuongezeka na kufunika ardhi MITA Hadi SITA kuja juu hivyo kusababisha pasiwepo uwezekano wa kukanyaga ardhi KAVU bila kutumia mtumbwi.

Chakula, mazao pia yameharibiwa, Serikali ndio sisi, tutafute namna Bora ya kusaidia ndugu zetu.

Source: Global Online tv.

Karibuni 🙏.
Kwani sheria inasemaje juu ya uvamizi wa maji?
 
Kwani sheria inasemaje juu ya uvamizi wa maji?
Sheria inasema shughuli za kibinadamu zianzie umbali wa mita 60 kutoka mwisho wa maji na mwanzo wa ardhi. Lakini maji yanapoongezeka madhara yake yanatofautiana kulingana na mazingira. Kuna watu walikuwa mita 200 kutoka maji yalipokuwa mwaka 2006 na yamewavamia ila kuna wengine walikuwa mita 30 kutoka maji yalipokuwa mwaka 2006 na hayajawafanya chochote. Hiyo inatokana na kiwango cha mwinuko kutoka usawa wa ziwa
 
Kumbe ni hivyo tu!!!
 
Mi sijui kama kuna wilaya ya lamadi huku tanzania.

Kuhusu maji kuvamia nyumba na mashamba hilo siwezi liongelea maana binadamu wa siku hizi ni wabishi sana. Kwa ukame uliotokea kuanzia miaka ya 2005 mpaka 2018 ukanda wa guba ya spiki maji yalikuwa yakiacha eneo lake na kuwa nchi kavu. Hiyo ilifanya watu wengi kujimilikisha hayo maeneo kwa shughuri zao. Hata hivyo selikali ilikuwa ikiimbia watu waache umbali wa mita 60 kutoka ufukweni lakini watu hawakuelewa. Kuna ongezeko la maji sikatai ila nikwa asilimia ndogo sana ikilinganishwa na mwaka 1999 baada ya mvua za elimino. Kama watu wangetii ule utaratibu wa mita 60 kutoka fukwe ya mwaka 2000 hakuna ambaye angezurika na maji ya miaka hii. Pia watu wa ukanda wa kuanzia nyakasenge huku mwanza mpaka Lukungu huko lamadi hiyo huwa ni ghuba na huwa ni maji mafupi pia huwa hakuna mwinuko mkubwa kutoka ufukweni kwenda nchi kavu. Hivo ziwa likiongezeka kina cha mita 2 tu basi litakuwa limekula zaidi ya mita 50 kwenda nchi kavu
Asante kwa ufafanuzi. Ukweli ni kuwa watu wamevamia Ziwa Victoria
 
Chukulia mfano wa ziwa victoria la baada ya mvua za mwaka 1998 kisha toka mita 60 kutoka ufukwe wa miaka hiyo uone kama kuna mtu angevamiwa na maji. Hat
Wangeacha mita 60 baada ya 1998 hakuna ambaye angevamiwa leo hii. Huo mwaka nilikuwa mdogo MZA mjini nilishuhudia maji karibu na makazi ya watu, lakini miaka ya 2010 nilishangaa kuona yale maeno ambayo yalikuwa na maji kuna wageni wamenunua viwanja na wamejenga nyumba za gharama, nilijua ipo siku kitanuka tu!
 
Yes na asilimia kubwa ya nyumba zilizoharibiwa hazina hata miaka 20 huko. Nyingi wamezijenga kwenye ukame wa mwaka 2006+ mpaka 2019. Hao ndo wanaongoza kuipigia kelele watu selikali
 
Back
Top Bottom