hapo kwenye red nadhani dogo Riz1 ulishapata jibu kuwa Mh. Mnyika amepimana ubavu na mzee wako siku nyingi hivyo wewe kujilinganisha naye ni mchicha/mbuyu!Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo.
Unalinganisha mlenda na pilau
Mnyika alifaulu aka-opt out, hawa watoto wamefeli, hawana choice
Wewe binafsi umekeshas sana, na ukafaulu, sasa uko bize unapiga domo maana kule kwingine si ulikua unaharibu sana??
usilinganishe pro-poor na poor
au a voluntary choice of a polician na forced choice yako ya kushindwa kufanya kazi uliyoipigia kitabu
Nyamtoroka ukichukulia serikali ya baba yake Ridhiwani kikwete mwaka huu haijatoa hata A saba tu! Hakuna devision one ya point saba mwaka huu! Waliosoma na Nape na Ridhiwani tuambieni walipata nini kidato cha nne!kijana kapata A tisa , huo ni uthibitisho tosha wa uwezo wake , achana na degree za mjomba za profesa jaji aliyekuwa mkuu wa kitivo
MIMI SI MWANA UBUNGO ILA,Mnyika atabaki kuwa mnyika tu.Ni tofauti kabisa na Vipaza sauti kama NAPE,MWIGULU,LUSINDE,SHIGELLA na WATOTO WA wengine wa WAKUBWA.
Mnyika ni hazina ya Taifa hili kwa siku zajazo bila kujali chama gani atakuwa anakiwakilisha.Huwezi kuona maendeleo kama huna macho na ndo maana huwezi kuwa huru kwa sababu bado wewe ni mtumwa.
Badilikeni ,tembeeni,jifunzeni,angalieni histroria ya UBUNGO,SEMENI baada ya kuona KISHA Kataeni kuwa watumwa..
Mkuu naona umempa Nape unafuu wa ukilaza compared to Riz! Kwa mlinganyo huu Rizone ni kilaza 5x (mara tano) ya Nape. All in all they are all brainwash, kamwe hawana hadhi ya kumchimba genius Mnyika.Wasiwasi wangu ni kwamba serikali ya CCM kupitia kwa mwanasheria mkuu itakuja na marekebisho ya sheria ya uchaguzi itakayotaka mgombea yeyote wa ubunge (except viti maalum) sharti awe na shahada ya chuo kikuu lengo ikiwa moja tu; kukomboa jimbo la ubungo kutoka CDM. Henda ndiyo maana hawa perpets (Nape na Riz) wa CCM wameanza kulifanya jambo hili kuwa agenda, ni kuwaandaa wananchi kisaikolojia juu ya kusudio lao la kufanya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi!!!!!
Mnyika ametumia porojo kukimbia kutoa taarifa zifuatazo kwa makusudi:
1. Matokeo yake ya A level hajayataja. Ya o level ametaja m¨paka idadi ya As alizopata, alipofika A level ameweka porojo. Ukweli ni kwamba A level alipata div 3.
2. Chuo hajamaliza. Kuhudhuria chuo si kuwa msomi wa chuo. Kusoma chuo ni kukamilisha mahitaji ya mitihani ya kozi yako ili uthibitishe umepata taaluma iliyokusudiwa. He is a collage drop out.
3. Hakuwa na sifa za kuchaguliwa kwenye program ya full time, hivyo akaingia program ya wazee ya jioni. Hili hajalisema kwa makusudi.
4. Baada ya kushindwa Ubunge mwaka 2005 alikuwa na miaka mitano mpaka 2010. Muda wote huu ameshindwa kumalizia kozi ya BBA!!!
5. Tangu aliposhindwa shule mpaka sasa ni miaka nane (8), bado ameshindwa kumalizia shule.
6. Sasa hivi ameenroll kwenye chuo fulani, ambacho katika majibu yake haya hajakizungumzia. Sababu ya kutokukizungumzia anajua yeye. Hata hivyo tangu ameenroll mpaka sasa hata module moja hajaweza kumaliza!!!
Jiulize kama mtoto wako akiamua kuacha shule na elimu ya form six ili ajikite kwenye siasa utamruhusu?
Ina maana gani kuacha shule kwa sababu ya siasa halafu unachoishia kufanya ni kulalamika kuwa CCM imeshindwa kutekeleza ahadi uloizotoa wewe kwa watu wako? as if CCM ilikwambia ukatoe hizo ahadi.
HAYA NI MAJIBU YA RIDHIWANI KIKWETE BAADA YA KUSOMA MNYIKA ALICHOANDIKA
Ridhiwani Kikwete
NIMEKUELEWA MBUNGE WANGU MNYIKA
Nimeisoma vizuri taarifa ya bwana Mnyika na nimeielewa. Nimeona sababu za msingi kwa nini hakumaliza shule na majibu juu ya hoja ambayo aliisimamisha bwana Nape Nnauye.
Ni jambo zuri ambalo amelifanya maana tumefunguka na kujua ukweli. Lakini naomba radhi kama sikueleweka vizuri. Nilichofanya mie ni kumuita ukumbini ili atutoe wasiwasi hasa mimi kama nilivyojielewa kuwa nilikuwa naye chuoni na ninaheshimu sana uwezo wake wa ufahamu.
Mwisho nimuhakikishie, ni jukumu la CCM kuhakikisha kuwa maji yanapatikana Jimboni Ubungo na tutayaleta. Kubwa zaidi akumbuke ilani yetu ni ya miaka mitano na maji yatafika pale kabla ya 2015. La msingi aendelee kuisukuma serikali na kumkumbusha waziri maghembe juu ya utekelezaji wa ya maneno yake mazuri na sio mbwembwe za kufurahisha baraza.
Mwisho, nikupongeze mnyika kwa kuja hadharani na kutoa wingu. Ni imani bwana Nape na wasomaji wengine tumekuelewa.
Shukrani. Hatuchafuani, tunasaidia kuwekana sawa . Huu ndiyo uwazi kwa vitendo.hongera muheshimiwa mbunge wangu.