Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

John Mnyika
Mh. Mbunge swali uliloulizwa na Nape jibu lake ni dogo sana; sidhani kama ulikuwa unahitaji kurasa nzima kulijibu; jibu lake lingekuwa hivi "elimu yangu ni kidato cha sita nilijiunga Mlimani kusomea BBA sikubahatika kumaliza"; nina uhakika hapo ungeeleweka zaidi; na inasikitisha sana kuona kijana kama wewe unajinyima haki yako ya kusoma kwa kigezo cha kuitumikia siasa na hili dai lako la kudai eti utarudi kusoma siku CCM ikitoka madarakani ni wazi umeamua kutokusoma kwa makusudi CCM haiondoki madarakani leo wala kesho; pamoja na kwamba unadai elimu haihusiani na kazi zako ni wazi umeamua kutupotosha kwa makusudi; elimu ya darasani ina umuhimu wake tena mkubwa sana; usiwadanganye vijana wa jimbo lako wakaacha kusoma kwa kutumia vigezo ambavyo havina msingi; ushauri wa bure wakati unaendelea na majukumu yako kama mbunge endelea na masomo; utaona ni jinsi inakusaidia kujenga hoja zako kisiasa.

Chama
Gongo la mboto DSM

kweli kama ndiyo tunatofautiana katika kuelewa kiasi hiki basi nchi hii tutakuwa maskini mpaka mwisho.
 
Hakuna hoja yoyote iliyojengwa na John Mnyika alichofanya ni kutafuta sympath; inashangaza sana mbona vijana wenzake kina Tundu Lissu; Zitto wamemaliza vyuo na wanaendelea na mapambano kama wanavyodai; hata mtu wangu wa deals Lema amemaliza elimu yake; sasa sielewi anachokiongea John Mnyika hata hao akina Mugabe pamoja na kuwa walikuwa wanapigana vita vya msituni kutafuta uhuru Southern Rhodesia bado walijizatiti kwenye elimu pamoja na walikuwa kwenye mazingira magumu bado walisoma na kuhitimu; ni vyema sana kama mh. John Mnyika angekuja na jibu honest; sio tu kwetu hata kwake yeye mwenyewe.

Chama
Gongo la mboto DSM
CC Ritz, Precise pangolin
Mkuu chama hakuna haja ya kusoma mavitu mengi wakati huyatumii hatutaki Mnyika aende tena darasani kwani Elimu aliyo nayo inawazidi hata maprofessor wezi wa CCM mimi namfananisha Mnyika na Steven Job
 
Last edited by a moderator:
Ukweli siku zote unamuweka mtu HURU. Asante sana Mnyika. Haya sasa njoo nape utueleze kati ya Mnyika na wewe nani ana akili zaidi. Mimi naona Mnyika kaelimika ila Nape unaweza kuwa na elimu ya madarasa
Nape elimu ya madarasa wapi.Naye Nape atuambie form fourr aliapta division ngapi.Maaana elimu ipo kwenye kidato cha nne huku juu form six au vyuoni hamna kitu. Maana mtu ukimaliza form four ukafaulu vizuri ukienda vyuo vya wenzetu ambavyo vipo kibiashara zaidi na haviangalii ubora wa elimu unaweza kurudi na PHD
 
CCM kweli hamnazo bado mnafikiri Tanzania ya leo ni ya 1990 iliyokua ya wazee wenye ufinyu wa mawazo na mawazo ya kizee yanayodharau vijana! huu ni wakati wa vijana na ni wa mabadiliko kweli 2015-CCM-OUT!!
 
afterall nchi hii kwa muda mrefu imekuwa ikujengwa na wasiosoma na kubomolewa na wasomi!

Mkuu ulichosema ni ukweli mtu kwani ccm imejaa madr. wangapi? Na kama wangetumia elimu yao kulijenga taifa tungekuwa wapi sasa? Ila kwavile wameamua kutumia elimu yao ktk kuiba basi ndivyo ilivyo ktk usemi wako
 
Mkuu chama hakuna haja ya kusoma mavitu mengi wakati huyatumii hatutaki Mnyika aende tena darasani kwani Elimu aliyo nayo inawazidi hata maprofessor wezi wa CCM mimi namfananisha Mnyika na Steven Job

Mkuu Precise pangolin
Badala ya kunihuzunisha imebidi nicheke sana unamfananisha John Mnyika na Steve Job ni matusi makubwa sana ambayo kama nitayaweka hadharani nitakula ban ya mwaka; kama Chadema hamtaki John Mnyika asome mtakuwa ni watu wa ajabu sana nadhani ipo haja ya daktari wa timu Kitila Mkumbo kuingilia suala hili
Kwa kuongezea tu leo nimsikiliza yule ustaadh wako Ilunga nakuomba siku nyingine usiwatusi waislamu; yule ni mwehu tu hata Quran sina uhakika kama anaijua kuvaa kanzu na barghashia sio ushehe.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Kujibizana na Nape ni kupoteza muda,kwanini ashihoji elimu ya pr.maji marefu au De sanga? Hii yote inaonyesha jinsi baadhi ya viongozi wa ccm walivyo kosa hoja!
Ni kweli mkuu akina Nepi wana uwezo mdogo sana wa kufikiri!! Ni wahusika wa Didas MASABURI alivyosema!? Hawana hata uwezo wa kujieleza kama alivyofanya Kamanda Mnyika hapa!!!!!!
 
Kujibizana na Nape ni kupoteza muda,kwanini ashihoji elimu ya pr.maji marefu au De sanga? Hii yote inaonyesha jinsi baadhi ya viongozi wa ccm walivyo kosa hoja!

Ama elimu ya lukuvi iliyochakachuliwa tangia msingi?
 
kweli kama ndiyo tunatofautiana katika kuelewa kiasi hiki basi nchi hii tutakuwa maskini mpaka mwisho.

Kwa mawazo yenu yanapotaka kutupeleka tunaweza kuwa masikini lakini kwa kuwa tupo makini hilo hamtaliweza!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
haaaa tena huyo deo sanga mbunge wa sisiem kaishia darasa la pili!!!!! kauli za ridhiwani zinalenga kuwadanganya wasiojua,mimi naona ni kelele tu
 
Kukosa hoja kwa nape na mwenzake akidhani kubishania elimu ya mtu ni hoja sasa mnabaki midomo wazi, pia nimefurahi mnyika alivyowaambia kwanini wasitumie elimu yao kutafuta matokeo yake ktk mitandao? na elimu ya Mnyika inahusiana na je na kushindwa kwa jk kushindwa kufanya shida ya maji kuwa historia Dar? Big up mnyika na kazi kwenu nepi na irizi kuweka cv zenu zilizojazana na F kibao
 
Kwanza nikupongeze kwa dhati kwa kazi njema unayofanya si kwa chama chetu pekee (CHADEMA) wala kwa Jimbo lako la Ubungo lakini pia kwa Taifa hili kwa ujumla.

Nikupe shime kwamba huna haja ya kuhangaika na kina Ridhwani au Nape kwani lengo lao ni kama ulivosema kuwa wanalenga kuwahamisha watu kwenye ajenda baada ya kuona serikali yao haina uwezo wa kutoa majibu kwa HOJA yako ya msingi.

Nikuombe uvute soksi bila kuchoka hadi hapo ukombozi kamili wa Mtanzania utakapopatikana kutia uchaguzi mkuu 2015 kwa CHADEMMA kutwaa nchi. Ombi la mwisho ni kuwa wewe kama mwanasiasa kijana jaribu kufanya kazi karibu na BAVICHA ili kuhakikisha hali ya hewa inatulia na tunafikia malengo ya kuwakomboa watanzania.

(Mwanachama wa CHASO Tawi la Muslimu University of Morogoro BAED 3 year na Mwl Rugambwa Sec. Bukoba). Viva Mnyika onces again.
 
Mnyika, kanda yetu ufunguzi lini? Achana na mazuzu, wanakupotezea muda. Kama hata Nape amesoma nani atashindwa. Kwa M4C halafu elimu ya uhakika. Hebu angalia leo matokeo ya form 4.
 
Back
Top Bottom