Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

hapo kwenye red nadhani dogo Riz1 ulishapata jibu kuwa Mh. Mnyika amepimana ubavu na mzee wako siku nyingi hivyo wewe kujilinganisha naye ni mchicha/mbuyu!

Sikumjua vizuri Mh. mnyika lakini siku zote nimekuwa impressed na kazi zake, inaelekea ana akili hata kabla ya kuingia darasani na ndio maana akiingia darasani mtazamo wake unakuwa tofauti maana madarasa mengi yamejaa watu wanotafuta vyeti na wanaotafuta ujuzi/elimu ni wachache sana.
Embu chukulia mfano mdogo, pale UDSM wanafunzi walivyo na jeuri alafu akatokea mwanafunzi wa evening programmes na kusimama Nkrumah then akawashawishi juu ya kitu chochote sio jambo dogo. Na hili Riz1 mwenyewe anakiri kuwa alikuwa akimuona japo yeye hasemi alikuwa anasimamia wapi wakati huo. Hii ni wazi kuwa Mh. Mnyika alikuwa zaidi ya mwanafunzi pale chuo kama alivyo zaidi ya Mbunge pale bungeni japokuwa kuna mamia ya wabunge.

Baada ya kusoma maelezo yake (japo nilijua baadhi) nashawishika kuamini kuwa aina ya elimu, misukosuko, matatizo na mafanikio ya Mh. Mnyika yanahakisi (reflect) Mtanzania halisi asiyekuwa na 'godfather' kama hawa wanaomchimba

 
Honger kamanda, maelezo yamejitosheleza, CCM haikudai chochote, waache hao wanafanya kazi kwa fadhila!
 
kama hadi nape ana elimu ya chuo,basi elimu imeshuka kwa kiwango cha kutisha..
kwa zengwe la ccm,mnyika akijiunga na chuo chochote hapa tanzania lazima wamfelishe
 
Kina Nape na Degree zao utadhani hata STD seven hawajapita..
 
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka huu hayana devision one ya point saba! Hilo linapaswa kuwa fundisho kwa Nape Nnauye na Ridhiwani Kikwete!
 
Maelezo yako yanaeleweka vizuri sana, hakuna dalili yeyote ya uongo kwani tumeshawazoea waongo jinsi wanavyopenda kuchanganya lugha wakati wa kujibu maswali ili tu kuuficha ukweli. TANZANIA INAHITAJI VIONGOZI WA AINA HII.
 
Mimi binafsi ni form four Graduate, Mnyika ni asset ya Chadema na naomba wanaChadem mlijue hili, nimesoma maelezo yake wala hayahitaji nyongeza, kwanza naomba kuhoji Uprofesa wa Juma Kapuya una tija gani?
chama matokeo ya form forrm 60% wamefeli, unapata wapi uhalali wa kuhoji uwezo wa Mnyika aliyepiga Division 1 form four? kazi ya CCM iliyobaki ni kuuwa mapadri tu hapo ndipo mna umahiri.

 
MIMI SI MWANA UBUNGO ILA,Mnyika atabaki kuwa mnyika tu.Ni tofauti kabisa na Vipaza sauti kama NAPE,MWIGULU,LUSINDE,SHIGELLA na WATOTO WA wengine wa WAKUBWA.
Mnyika ni hazina ya Taifa hili kwa siku zajazo bila kujali chama gani atakuwa anakiwakilisha.Huwezi kuona maendeleo kama huna macho na ndo maana huwezi kuwa huru kwa sababu bado wewe ni mtumwa.

Badilikeni ,tembeeni,jifunzeni,angalieni histroria ya UBUNGO,SEMENI baada ya kuona KISHA Kataeni kuwa watumwa..
 

Janjaweed umepiga ikulu...umemaliza! ZeMarcopolo tunamjua bana, na sababu zake za kushindwa utabibu, sasa ana 'fani' mpya, kupiga domo!
 
kijana kapata A tisa , huo ni uthibitisho tosha wa uwezo wake , achana na degree za mjomba za profesa jaji aliyekuwa mkuu wa kitivo
Nyamtoroka ukichukulia serikali ya baba yake Ridhiwani kikwete mwaka huu haijatoa hata A saba tu! Hakuna devision one ya point saba mwaka huu! Waliosoma na Nape na Ridhiwani tuambieni walipata nini kidato cha nne!
 
Last edited by a moderator:
Nakupongeza sana Mh. Mnyika hakika umetugusa wengi tuliosoma kwa shida kwenye nchi hii, nakushauri upatapo nafasi ukamalizie masomo yako kwani kati wa marais wanaokuja wewe ni mmoja wao, una mbali Mh, Nape hakufiikii hata theluthi moja kwenye kujenga hoja na kuzitetea
 

Nimependa kauli ya Mnyika kuwa NITARUDI KUSOMA CCM IKIONDOKA MADARAKANI maana elimu haina mwisho! Hii ni kauli ya mzalendo hata Nyerere hakuwa na PhD. Lakini anakumbukwa hadi leo!
 
[h=5]HAYA NI MAJIBU YA RIDHIWANI KIKWETE BAADA YA KUSOMA MNYIKA ALICHOANDIKA

Ridhiwani Kikwete


[/h][h=5]NIMEKUELEWA MBUNGE WANGU MNYIKA

Nimeisoma vizuri taarifa ya bwana Mnyika na nimeielewa. Nimeona sababu za msingi kwa nini hakumaliza shule na majibu juu ya hoja ambayo aliisimamisha bwana Nape Nnauye.

Ni jambo zuri ambalo amelifanya maana tumefunguka na kujua ukweli. Lakini naomba radhi kama sikueleweka vizuri. Nilichofanya mie ni kumuita ukumbini ili atutoe wasiwasi hasa mimi kama nilivyojielewa kuwa nilikuwa naye chuoni na ninaheshimu sana uwezo wake wa ufahamu.

Mwisho nimuhakikishie, ni jukumu la CCM kuhakikisha kuwa maji yanapatikana Jimboni Ubungo na tutayaleta. Kubwa zaidi akumbuke ilani yetu ni ya miaka mitano na maji yatafika pale kabla ya 2015. La msingi aendelee kuisukuma serikali na kumkumbusha waziri maghembe juu ya utekelezaji wa ya maneno yake mazuri na sio mbwembwe za kufurahisha baraza.

Mwisho, nikupongeze mnyika kwa kuja hadharani na kutoa wingu. Ni imani bwana Nape na wasomaji wengine tumekuelewa.

Shukrani. Hatuchafuani, tunasaidia kuwekana sawa . Huu ndiyo uwazi kwa vitendo.hongera muheshimiwa mbunge wangu.


[/h]
 

Ikiwa hivyo CCM ndio watakuwa waathirika wakubwa. Wabunge wasio na shule ni wengi kwao na tu watakachofanikiwa ni kumfanya Mnyika apumzike kwa miaka 5 tu afanye degree yake na masters as well arudi tena kwa kishindo,kwani wewe kwa jinsi tu alivyojieleza hapa na jinsi anavyowajambisha bungeni mpaka wanazuia hoja una mashaka na kichwa yake?
 



kumbe mulikuwa mnajua? Mlikuwa mnahoji ya nin? Ok, elimu yake ndo km ivo, tatizo la maji lini kumalizika?
 
Namkubali mnyika kuliko yeyote pale chadema
 
Nimempa Mwanangu wa kiume ausome huu ufafanuzi wa Mnyika!nikamwambia nikifa mapema,huyu ndo awe role model wako!yupo hapo sababu hana "Godfather"....angelikuwa na Godfather ktk system Mnyika angekuwa mbali sana!!Nikajiuliza mimi nikifa leo,je mwanangu anaweza kupambana peke yake kiasi hiki?
 
 
Modern commercial institute imetoa offer ya degree kwa Mh Mnyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…