Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma


Nimeipanda sana hii, na hata alivyojibu Ridhiwan anaonekana ni mtu makini sana siyo kama wenzake.
 
nikusaidie kidogo, Mh. mbunge hataki majibizano yasiyo na msingi hivyo kaamua kuwaeka kila kitu ili msiendelee kuuliza maswali, atakae uliza tena hapo basi huyo ni mbulula.
 
Mmh, bado napata shida kujua kama huyu dogo kweli hana Degree, ndio maana hata Ridhiwani hapo juu naye ameandika kwa style ya kuona aibu hivi, ukweli kwa jinsi ambavyo Mnyika anavyo jua kujenga hoja na kupangilia maneno na hotuba zake (ushahidi ni huu waraka) huwezi amini eti hana Degree ukilinganisha na PHDs walizonazo watuwa magamba, iangalie ile PHD ya yule jamaa wa Wizara ya Elimu, nenda kwa yule wa maji, usimsahau yule mama aliyewahi kuwa Bar maid na kuzalishwa na wale wakimbizi wa ANC, mtazame vizuri naibu spika wa bunge na boss wake kisha malizia na mwanasheria mkuu wa serikali then walinganishe na Mnyika, unaweza baadae uka conclude vibaya kwamba kumbe elimu sio muhimu, well nadhani msomi ukiwa ccm sehemu fulani ya Ubongo inabidi uwe unaiacha Lumumba! Sorry to say so.
 
Kweli nimeamini wapo wa2 bado wanafikiri Elimu ni cheti. mbona vinauzwa kila mahali! elimu ni implemtation ya ulicho nacho. kwa taarifa 2 ya hoa jamaa ni kwamba ufahamu wa mnyika ni zaidi ya Ukoo wao wote. kumbe ndo mana wanaiba/nunua mithani ili waje kutuambia wameelimika eeeeeeeeeeeeeeeh! Hao ndio wanaosababisha elimu yetu iwe chini. kwa watu kama hao tutajiunga na Jumuiya ya Africa mashariki kweli? Hivi nape alipomaliza form four alipata hata A moja kweli hata ya kiswahili au hata ya Dini. Mnyika big up.
 
By Mnyika "Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne;
nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa. "


Mtu anayepata DIV ONE point 7 yenye A Tisa si wa kumwuuiza elimu yake. unaweza ukaumbuka bure. Watu wenye uwezo huu huwa wanafikiria mbali kuliko sisi wenye elimu ya kuunga unga madarasa na kozi. watu wenye upeo huu huwa hawafikirii kabisa kwamba kuwa na Degree ya Chuko kikuu ndiyo eti unaonekana msomi.

Mfano mzuri ni mwanzilishi wa Microsoft - Bill Gates. Aliacha masomo yake mwaka 1975 akiwa mwaka wa Pili pale Harvard University na kuanzisha kampuni yake ya Microsoft ili apate muda zaidi wa kujikita katika uandishi wa Program za Computer akiwa na Rafiki yake Paul Allen, haya ndiyo matunda yake kwamba mpaka sasa 98% ya dunia inatumia microsoft products.

Sasa huwezi kuibuka na ukahoji elimu yake utakuwa ni kishekesho; leo hii hoja anazotoa Mnyika, maandiko yake, utafiti wake unaonyesha kiwango cha udaktari wa falsafa;

Mbunge wangu chapa kazi, sijawahi kuwa na wasiwasi juu ya utendaji wako wa kazi. tupo pamoja 2015, hiki chama cha upinzani 2015 kimeshapoteza mwelekeo long time kitambo.
 
kama umeelewa basi vilevile kubali kwamba uamuzi waliotaka kuufanya spika na naibu wake ya kutokuonyesha bunge live haufai
 
Sawa ni pumba za JJ; zako ni pombe zilizolala utaishia uharo. Mtu mzima hovyo huna hata staha wala hekima ya nini cha kuzungumza hadharani? Yote haya sababu ya uccm

Wewe na muono wako nami nimempa ushauri huyo kijana, akipenda auchukuwe akipenda auache. Ni ushauri wa mtu mzima kwa kijana mdogo mwenye matatizo makubwa ambayo wewe na walio kama wewe kwa upofu wenu hamuyaoni.
 
Nape aje, tunamsubiri kwa hamu hapa! Amechimba kisima lazima aingie mwenyewe.
 
uwezo wa NEPI ni mdogo sana kulinganisha na JJ MNYIKA,nakumbuka LUKUVI alishawahi kusema ya kuwa katika WABUNGE anaowaheshimu sana kutokana na mtazamo wao na michango yao bungeni basi ni JJ MNYIKA.
 
Mnyika amezaliwa kizazi tofauti na kinachomhitaji ana mambo makubwa kuliko kwa hiki kizazi cha misukule. Just imagne mtu anaulizwa kwanini ahadi ya kuleta maji Dar Feb, 2013 haijatekelezwa anasema ilani ni ya miaka 5. Af sisi tunachecheka tu.

Umewaza kitu ambacho ni muhimu sana,ni kweli nchi nyingine zinazojua umuhimu wa watu Genius kama JJ
wangemtumia kwa manufaa ya nchi,lakini inasikitisha mijitu ndio kwanza inatafuta kumvunja moyo na kumkatisha
tamaa kwa juhudi zake kuwakomboa wananchi,jiulize tofauti kubwa ya kiufahamu kati ya Mnyika na Ridhwani
ameongelea suala la mtu ameahidi kuwa na maji safi kwa kipindi ambacho kimeshapita,mwenye ufahamu mdogo
anajibu sera zao ni mpaka 2015!!!!!stupid"!!!!!!
 
Kuna mmoja aliona umahiri wako kwenye kutoa hoja ndio akataka kujua kama na wewe ni DOKTA kama baba yake.
 
Big up Mh.Mnyika mwana BBA mwenzangu. Nakushauri ukamalizie sehemu ndogo iliyobaki, bila shaka umebakiza project work tu. Mimi pia elimu ya BBA imenisaidia sana kukuza uelewa wangu kwani nilisoma huku nikifanya kazi na nimetumia elimu hiyo kupa Masters hapo hapo mlimani.
 
Ehhh hapa umewakata maini wambea wote wa CCm big Kamanda!!!!!!
 
Ehhh hapa umewakata maini wambea wote wa CCm big up Kamanda!!!!!!
 
Nape alikuwa mzito darasani, alifeli la saba, akapelekwa sekondari ya kulipia, nako akafeli fomu 4, akambwelambwela mtaani asijue la kufanya, ndo baadae akaungaunga cetificate ya kigamboni kwenye chuo cha ccm, akaunganisha diploma japo alikuwa mzito mzito hivyo hivyo, lakini alibebwabebwa ili mradi mzigo uende. baadae kwa msaada wa ubalozi wa tanzania india wakati huo alijitaidi kumwunganishia chuo india,hii ni baada ya kutoswaga kwenye uongozi wa uvccm

Kwa riziwani, hakuna shida, dogo kapiga skul,offcourse namkumba dogo pale mkwawa sec.(complex and casino),ud, iyo elimu yake anayosema alienda kuongezea ulaya, mi sina taarifa nayo, labda mzee wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…