Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Hongera kumbe tuna share interest sehemu nyingi ikiwa ni pamoja na kufanya mtiani wa fm 4 uliofutwa pamoja, kusoma ktk mazingira magumu pamoja lakini bado nakuomba uweke wazi elimu yako ya chuo kikuu, uligraduate kweli? Weka ushahidi unaoeleweka ili ku clear beyond resonable dought.

Hivi wewe ndo unajiita una digrii mbona mgumu sana kuelewa..inaelekea ulikuwa unakamatwa sana wewe..Kashakwamvia hajakana kuwa hajamaliza chuo sasa unachotaka ni nini?mbona mmezoea kudanganya basi mnatak wote wawe waongo?
 
Tuwekee ushahidi wa elimu yako usitupe historia ya kazi zako. Hata mimi ni mwanaharakati tena kwa taarifa yako yale maandamano ya mwaka 2004 ud nililala polisi pale mabatini makumbusho.
Bro, mbona unang'ang'ania hii hoja ya kipumbavu! Unatata JJ aeleza nini tena kuhusu elimu yake? Kwa maelezo haya ya ndugu Mnyika, bado tu hujamwelewa? Watu wengine mkoje? Umetumwa nini hapa JF? Ww kuwa mwanaharakati au kulala polisi yana umuhimu gani hapa? Kuna yeyote hapa Jf aliyetaka kujua kuwa ww unafanya nini? Really you are hocus pocus!
 
Intruders are uphere! You leave issues n discuss sijui niite nn? We are too low this days! Zero minds shouldnt dictate
 
Mkuu hiyo ya nne si kwa mujibu wa katiba, ni kwa mujibu wa muono wako. Hayo matatu ya kwanza yametajwa kabisa na katiba kama majukumu ya msingi ya mbunge kwa mujibu wa katiba.

Umeacha jukumu kubwa sana la mbunge, nalo ni uwakilishi (representational). Hili ni pamoja na kupeleka matatizo ya wananchi na kuishinikiza serikali iyatatue. Na ninaamini hili ndilo unaloliita ahadi kwa wananchi.

Kwa kuwa mbunge hapaswi kutatua matatizo ya wananchi kwa fedha zake, bali anapaswa kuikumbusha serikali majukumu yake, kama alivyotumwa na wananchi wake. Serikali ikiwa sikivu na ikiwa na rssilimali za kutosha itatekeleza. Serikali isipokuwa sikivu si kosa la mbunge. Serikali ya CCM ina tabia ya kukomoa wabunge wa upinzani. Siku hizi watu wanaona na wanaelewa tatizo li wapi. (Rejea hoja ya tatizo la maji ubungo).

Katika hili la uwakilishi, ni pamoja na kufanya mikutano na wananchi kuwasikiliza na kuwapa mrejesho. Haya Mnyika anayafanya vizuri sana. Labda kama unafahamu mbunge anayefanya vizuri zaidi mtaje. Website ya Mnyika (mnyika.blogspot.com) imejaa nyaraka kwa wapiga kura wake akiainisha juhudi zake katika uwakilishi. Nani mwingine anafanya hilo.

Ni kazi ya Bunge katika mfumo wa kidemokrasia kuhakikisha kuwa matendo ya serikali iliyopo yanakidhi matakwa ya jamii wanayoiwakilisha, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono hoja nzuri na kupinga zile zinazoonekana kukinzana na maslahi ya jumla ya kitaifa. Hapa tena Mnyika anang'ara

Jukumu jingine la msingi sana la mbunge ni la kisera. Bunge ni ni chombo cha kutathmini mwenendo wa jumla wa kisera wa serikali na kutathmini mabadiliko yanayofaa. Hapa pia mchango wa Mnyika ni mkubwa sana.

Hapo Mkuu unacheza na maneno tu. Hiyo representation ni kutekeleza ahadi alizotoa na anafanya hivyo kama mwakilishi wa wananchi. Kumbuka kuwa wabunge huchaguliwa kutokana na kile wanachosema wakati wa kampeni.
Pili anapotoa ahadi hawezi kusema hajatekeleza kwa sababu ya serikali. Kumbuka jamii zetu zina uwezo mkubwa ambao kiongozi akiwa mzuri anaweza kuuorganise uwezo wa jamii wakafanya jambo kubwa. Swali ambalo unatakiwa kujiuliza ni je, wakati mbunge anatoa ahadi fulani alikuwa naive kiasi kwamba hakujua kuwa kuna vikwazo? Na kama alijua kuwa kuna vikwazo lakini akaona atoe ahadi inakuwaje leo aseme sio jukumu lake?
Vilevile jiulize, je, katika kampeni za uchaguzi unaokuja atatoa ahadi nyingine? na atategemea watu wachukulie ahadi zake serious?

Kumbuka kuwa hata yule mtu anayemkataa mbunge aliye madarakani hamkatai kwa sababu yeye eti amevaa shati la rangi fulani, humkataa kwa sababu maneno yake na vitendo haviendani. Ahadi zake atekelezi. matumaini anayowapa wananchi yanaenda in vain.

Unaposema mbunge ni machachari jiulize:
Kuna sheria gani amefanikisha itungwe ili kusaidia watu wake?
Kuna kipengele gani cha bajeti amefanikisha kiboreshwe ili kuwafaa watu wake?
Kuna jinsi gani watu wake walikuwa hawapati huduma wanayostahili amehakikisha kuwa wanaipata?

Nakukumbusha tu kuwa almost doest count. Kama mbunge alikuwa almost there katika kutatua lakini mpaka mwisho tatizo bado lipo hapo anakuwa hajawafaa watu wake.
TEKELEZENI AHADI ZENU...
 
Niko Ubungo, Mnyika is the best MP we have ever had!

Ukipenda tu bet niko tayari. Mnyika 2015 anashinda kwa margin kubwa zaidi ya kura kwa kuwa kukubalika kwake kumeongezeka tangu achaguliwe!

By the way wewe kuna mbunge yeyote wa upinzani ambaye umewahi kumkubali? Kuna mbunge yeyote wa CCM umewahi kumkosoa?
 
John Mnyika,

Si ungesema tu kuwa ni kweli umesoma mpaka kidato cha sita na umejaribu mara kadhaa kujiunga na chuo kikuu lakini hujafanikiwa kumaliza.

Pumba nyingi mchele kidogo. Ngonjera zote za nini? naona unamatatizo zaidi ya huo "mtanziko" uliousisitiza huko juu. Nakuuliza hivi? umeshawahi kuonana na daktari wa magonjwa ya uchizi "psychiatrist"? kama bado, nakusihi uonane nae haraka sana, unaonesha una matizo makubwa zaidi ya "mtanziko".

Zomba na wapuuzi wenzako wote pamoja na ualimu wako wote mmesha sikia kwamba kijana kamaliza six na hajafeli popote .Sasa imesha wasaidia kuwapatia watanzania maisha bora mliyo waahidi ? JJ ni kwamba hata yule ---- wenu wa class gani sijui hagusi kazi yake matusi tu naona sasa katulia .
 
Niko Ubungo, Mnyika is the best MP we have ever had!

Ukipenda tu bet niko tayari. Mnyika 2015 anashinda kwa margin kubwa zaidi ya kura kwa kuwa kukubalika kwake kumeongezeka tangu achaguliwe!

Huu ndio ukweli.

Sikukatalii. Kukubalika na kutekeleza ahadi ni vitu viwili tofauti though.
Tumeona mara nyingi sana viongozi wanakubalika kwa kiwango cha juu na ukiwauliza watu sababu hawana. Unakumbuka 2005?
 
Kwa uwezo wa kujenga hoja school dropout kama Mnyika amewashinda hawa jamaa wenye degree za India mara mia mbili.John Mnyika ana uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja na amedhihirisha kwamba cheti sio kila kitu.Hii inanikumbusha jamaa zangu tulio graduate pamoja pale UD na Masterz ya Mzumbe wanayo lakini hata uwezo wa kuandika sentensi moja iliyonyooka hawana, Iwe ya Kiingereza au hata ya Kiswahili
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa.

Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tamba safi s
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa.

Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.

Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.

Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.

Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita.

Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno.
Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.

Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo.

Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi.

Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree).

Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo.
Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.

Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.

Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.

Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.

Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.

Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu.

Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu.
Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi.

Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.

Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.

Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu.

Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani.
Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita).

Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa.
Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?

JJ

Kamanda rudi shule 2015 hatuwezi kukupa Uwaziri kwa sababu ya A zako za Maua lazima uwe na elimu ya kutosha hili ni muhimu believe me.
 
Sikukatalii. Kukubalika na kutekeleza ahadi ni vitu viwili tofauti though.
Tumeona mara nyingi sana viongozi wanakubalika kwa kiwango cha juu na ukiwauliza watu sababu hawana. Unakumbuka 2005?
Sababu wanayo.

Ni uwakilishi uliotukuka. Anafanya nao vikao, anawasikiliza, anawasemea bungeni, anafuatilia na utekelezaji, na anarudi kueleza mafanikio, matatizo na changamoto.

Muda wowote ukitembelea tovuti yake unaona wazi wazi ni nini anafanya na nini anapanga kufanya. Tembelea http://mnyika.blogspot.de/

Na anavyoandamwa na kujaribu kukwamishwa na CCM ndivyo anavyozidi kupendwa.

Niambie mbunge gani wa CCM anawakilisha wananchi namna hiyo?

Najua humpendi kabisa Mnyika. Licha ya hivyo huwezi kuondoa ukweli.
 
Matokeo ya O-level ni udhibitisho tosha kuwa JJ ni genious. Nepi na Rz1 nenden mkabishane na watu kama akina Lusinde. JJ ni level nyingine,atawatesa sana
 
Mnyika wewe ni zaidi ya profesa mi nimekiutunukia phd kwani uwezo wako ni zaidi ya wanaojiita maprofesa
 
Huyu ana Dagree na Cheti anacho lakini Tanzania "muungano wa nchi Mbili Tanganyika na Zimbabwe" Kuna tofauti kubwa kati ya elimu (cheti) na kuelimika.

Salutation

Honourable
First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name:Mulugo
Constituent: Songwe
Political Party: CCM
Office Location: P.O. Box 9121, Dar Es Salaam
Office Phone: +255 754 315 922/+255 784 315 922
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: [email protected]
Member Status: Current Member
Date of Birth 27 January 1972

[TD="width: 42%, align: center"]

Member picture
1645.jpg

[/TD]

[TD="width: 20%"] Member Type: [/TD]
[TD="width: 38%"]Constituency Member[/TD]
Open University of Tanzania
Songea Boys' High School
Mbeya Secondary School
Rukwa Primary School, Chunga

[TH="colspan: 5, align: left"] EDUCATION [/TH]

[TH="width: 35%"] School Name/Location [/TH]
[TH="width: 27%"] Course/Degree/Award [/TH]
[TH="width: 15%, align: center"] Start Date [/TH]
[TH="width: 13%, align: center"] End Date [/TH]
[TH="width: 10%, align: center"] Level [/TH]

[TD="align: center"]BA (Economics Education )[/TD]
[TD="align: center"]2002[/TD]
[TD="align: center"]2008[/TD]
[TD="align: center"]GRADUATE[/TD]

[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1994[/TD]
[TD="align: center"]1996[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]

[TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]1993[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY[/TD]

[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1982[/TD]
[TD="align: center"]1989[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
EMPLOYMENT HISTORY
 
OK..
Kumbe Mnyika ni form six leaver?safi sana,
Haya tunasubiri kuona na za kwenu kina NAPE,
Ila mnyika fanya urudi school kiongozi..
 
Hapo Mkuu unacheza na maneno tu. Hiyo representation ni kutekeleza ahadi alizotoa na anafanya hivyo kama mwakilishi wa wananchi. Kumbuka kuwa wabunge huchaguliwa kutokana na kile wanachosema wakati wa kampeni.
Pili anapotoa ahadi hawezi kusema hajatekeleza kwa sababu ya serikali. Kumbuka jamii zetu zina uwezo mkubwa ambao kiongozi akiwa mzuri anaweza kuuorganise uwezo wa jamii wakafanya jambo kubwa. Swali ambalo unatakiwa kujiuliza ni je, wakati mbunge anatoa ahadi fulani alikuwa naive kiasi kwamba hakujua kuwa kuna vikwazo? Na kama alijua kuwa kuna vikwazo lakini akaona atoe ahadi inakuwaje leo aseme sio jukumu lake?
Vilevile jiulize, je, katika kampeni za uchaguzi unaokuja atatoa ahadi nyingine? na atategemea watu wachukulie ahadi zake serious?

Kumbuka kuwa hata yule mtu anayemkataa mbunge aliye madarakani hamkatai kwa sababu yeye eti amevaa shati la rangi fulani, humkataa kwa sababu maneno yake na vitendo haviendani. Ahadi zake atekelezi. matumaini anayowapa wananchi yanaenda in vain.

Unaposema mbunge ni machachari jiulize:
Kuna sheria gani amefanikisha itungwe ili kusaidia watu wake?
Kuna kipengele gani cha bajeti amefanikisha kiboreshwe ili kuwafaa watu wake?
Kuna jinsi gani watu wake walikuwa hawapati huduma wanayostahili amehakikisha kuwa wanaipata?

Nakukumbusha tu kuwa almost doest count. Kama mbunge alikuwa almost there katika kutatua lakini mpaka mwisho tatizo bado lipo hapo anakuwa hajawafaa watu wake.
TEKELEZENI AHADI ZENU...
Ahadi za sasa zinatekelezwa chini ya ilani ya ccm.... Umesoma uochandika ukakielewa

ccm ndio wenye hatamu na hakuna kinachoendelea ndio maana hatuendelei, labda wachache wanaofaifika kutokana na ndugu zao kuwa wanasiasa na wafaidika wa mfumo ccm kama wewe

Tuna catalogue ya ahadi, 99% ni zenu mkuu
 
Sikukatalii. Kukubalika na kutekeleza ahadi ni vitu viwili tofauti though.
Tumeona mara nyingi sana viongozi wanakubalika kwa kiwango cha juu na ukiwauliza watu sababu hawana. Unakumbuka 2005?
Kwili mkuu, ahadi za serikali ya ccm lazima zitekelezwe
 
Back
Top Bottom