Aisee,
Mungu nijaalie nisiwe Mwanasiasa, wallah tena.....suala ni education background, sasa ngonjera zote za nini Mnyika?! Manake kila nikisoma, nashindwa kuelewa! Let me try to summarize:
1. Standard Seven ulibabua sana paper na kupangiwa Ilboru....lakini kwavile ulitaka kumtumikia bwana, ukaamua kwenda Maua Seminary....hapa nimekuelewa! Kwenye paper ya Form IV, ukakuntungua 9 A's ambazo zingekufanya upelekwe shule yoyote ile ya serikali(za Vipaji).
2. Kama ambavyo ulikataa mara ya kwanza kwenda shule ya vipaji, hivi sasa ukaenda Tambaza kwa sababu ulitaka kusoma huku ukiendelea na harakati ambazo ulizianza kabla. Hapa tena, ukababua paper ile mbaya! Aisee, Mnyika unatisha wangu!! Lakini pamoja na kubabua paper, unasema kwa mara nyingine "kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia" Hapa umeniacha! Mwenyewe unasema ulipangwa Ilboru shule ya vipaji, lakini ukakataa mwenyewe! Ukaenda Maua na kama kawaida yako, ukababua paper kwa kupata 9 A's na hivyo ungeweza kwenda shule yoyote ile! Hata hivyo, wewe mwenyewe tena, ili uweze kufanya yale ambayo umeyaanzisha, ukaamua kwenda Tambaza!! Sasa hiyo serikali ya CCM unayoilaumu kwamba kwa mara ya pili haikutambua vipaji na ukapaswa ujilipie mbona sikuelewi?! Mbona naona kuna mahali CD imeruka?! Maua ulikung'uta 9 A's ambazo zinakupa sifa na haki ya kwenda shule ya vipaji! Tambaza ulikung'uta A's ngapi kiasi cha serikali ya CCM kuendelea kutoona kipaji chako na kukuacha ujilipie?! Au unazungumzia hawakutambua kipaji chako baada ya kupiga hizo 9 A's?! Ulitakaje? Baada ya kupiga 9's ulipiwe ada, au? Hapa sijaelewa manake hususani pale unaposema KWA MARA YA PILI! Ina maana kwavile Std Seven ambayo ilikupa tiketi ya Ilboru ukaacha na kwenda Maua Seminary nayo inahusika....kwamba hata huko Maua ilibidiserikali wakulipie?!
Baada ya kupitia maelezo yako yenye mtiririko mbovu ambao naamini umeufanya kwa makusudi ili kuwachanganya watu, nashawishika kuamini kwamba education background yako imeishia hapa : "Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki."
Hata hivyo, hapo kabla umeandika:Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree).
With due respect sir, kama historia yako ndo inaishia hapo na unasema kwamba una elimu ya Chuo Kikuu, basi sina haja ya kutafuna maneno kwamba huo ni UDANGANYIFU WA HALI YA JUU! Narudia, kwa historia hii uliyoitoa hauna sifa za kujiita Una elimu ya Chuo Kikuu...! Sijaona popote ulipoandika kwamba ulirudi chuo kumalia ile miezi michache ambayo ilibaki na kwamba hata mitihani ya semister ya mwisho hukufanya! Na wala si sahihi hata kidogo hiyo ya kwako kuita eti ni Associate Degree....! Wewe unachotakiwa kuwa wazi ni kwamba ulisoma UDSM kwa miaka mitatu lakini kutokana nA pilika pilika za hapa na pale, hukumalizia masomo yako; PERIOD! Sema tu nakusifu umekuwa mjanja kwa kutosema wazi kwamba una degree au hauna degree huku maelezo yako ukitaka kuwafanya watu waamini kwamba una degree!