Mheshimiwa Mnyika, we ni rafiki yangu, tumesoma wote Tambaza. kama rafiki ninapenda uwe na mafanikio zaidi ya haya, lakini pia kusema ukweli ni muhimu bila kuingiza siasa, ukweli ni kuwa hukuwa umechaguliwa kujiunga form five kwenda shule yoyote ya serikali, na hii inatokana na makosa, yaliyofnywa na Maua Seminary wenyewe kwa kutokupeleka, form zako wizarani... hivyo Tambaza uliingia kama second selection, maana ulichelewa kureport pia, hiyo pia iliwakuta mabinti kadhaa kutoka kwa shule hizo, kama kifungilo na nyingine. Ukweli unabaki kuwa mazingira ya Tambaza sio mazuri kwa mtu aliyezoea kutafuniwa kama huko Maua, kuweza kupenya kiurahisi, ndo maana wengi wa waliotoka shule kama hizo za kifungilo, seminary waliambulia div 4 au three, wachache sana walipata two, sina uhakika kama mnyika alipata div II, kama ulivyoeleza, hata hivyo nakuamini kuwa huenda ulipata marks hizo, though i knew kuwa ulipata division three.
Ukweli mwingine ni kuwa ilikuwa shida sana kwa mwanaume kwa wakati ule mwenye div III, au hata two ya mwisho kuwa admitted mlimani kwa government sponsorship maana criteria ilikuwa Ni a minimum of C na D, yaani at least points 5.5 kwa maana G.S ni points 0.5, hivyo nina Imani kuwa Mnyika hakuwa anaqualify kujiunga UDSM, halafu pia course ambazo walikuwa wakichukua watu wenye marks za chini mainly walikuwa FASS (PSPA na Socilogy), hivyo basi ukawa umepata wadhamini ambao, kama sikosei yalikuwa mashirika ya kidini, na katika course hiyo ya jioni ya BBA ulikuwa na Marafiki wengine wawili kutoka Tambaza, na ulikuwa ukiishi Mabibo.
Hata hivyo katika harakati za wewe kujiunga na kuendelea na masuala yako ya chuo bado ulikuwa Mwana CCM, hadi baada ya Muda ulipojiunga CHADEMA, na hatimaye kugombea Ubunge.
Ni ukweli usiopingika kuwa uamuzi wako wa kutokuendela na masomo ulikuwa zaidi juu ya masuala ya kisiasa na si kwasababu ya mizengwe, maana kuna watu wengi ambao walishawahi kufukuzwa vyuo na wengine kudisco kabisa lakini sasa wana PhD.
Ombi langu kwa wanasiasa si kila jambo linahitaji kuendeshwa kisiasa, tujipe Muda tujadili maendeleo ya Taifa, Maana kama leo tutasema tunaacha kusoma kwa ajili ya siasa kesho watoto wetu watasema wanaacha kusoma kwasababu wanataka kucheza soka, mwingine kuwa mwimbaji, na kwasababu hana Muda kwasababu soko litamtupa mkono then hataki hata kusomea huo Muziki ambao ndo anaona unalipa. Kwasababu kwa ulimwengu wa Leo it is not only about Experience but also, Qualification matter. Kama kuna tatizo kwa Accredited institutions kutoa competency based education and training hilo ni tatizo jingine lakini halitoi umuhimu wa QUALIFICATIONS. I stand to be corrected. No personal conflicts