Mbunge ana kazi nne:
1. Kutunga sheria.
2. Kushiriki katika shughuli kamati za Bunge.
3. Kupitisha/kutopitisha bajeti ya nchi
4. Kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wake -
hii ya nne (4) mdio kipimo cha ubora wa mbunge kwa sababu ni yeye mwenyewe alijipima akaona anaweza kuzitekeleza hizo ahadi ndio maana akazitoa kwa wapiga kura. Siwezi kumlaumu mbunge kwa kushindwa kuzuia bajeti kupitishwa ila nitamlaumu mbunge asiyetekeleza ahadi alizotoa kwa hiari yake.
Mkuu hiyo ya nne si kwa mujibu wa katiba, ni kwa mujibu wa muono wako. Hayo matatu ya kwanza yametajwa kabisa na katiba kama majukumu ya msingi ya mbunge kwa mujibu wa katiba.
Umeacha jukumu kubwa sana la mbunge, nalo ni uwakilishi (representational). Hili ni pamoja na kupeleka matatizo ya wananchi na kuishinikiza serikali iyatatue. Na ninaamini hili ndilo unaloliita ahadi kwa wananchi.
Kwa kuwa mbunge hapaswi kutatua matatizo ya wananchi kwa fedha zake, bali anapaswa kuikumbusha serikali majukumu yake, kama alivyotumwa na wananchi wake. Serikali ikiwa sikivu na ikiwa na rssilimali za kutosha itatekeleza. Serikali isipokuwa sikivu si kosa la mbunge. Serikali ya CCM ina tabia ya kukomoa wabunge wa upinzani. Siku hizi watu wanaona na wanaelewa tatizo li wapi. (Rejea hoja ya tatizo la maji ubungo).
Katika hili la uwakilishi, ni pamoja na kufanya mikutano na wananchi kuwasikiliza na kuwapa mrejesho. Haya Mnyika anayafanya vizuri sana. Labda kama unafahamu mbunge anayefanya vizuri zaidi mtaje. Website ya Mnyika (
mnyika.blogspot.com) imejaa nyaraka kwa wapiga kura wake akiainisha juhudi zake katika uwakilishi. Nani mwingine anafanya hilo.
Ni kazi ya Bunge katika mfumo wa kidemokrasia kuhakikisha kuwa matendo ya serikali iliyopo yanakidhi matakwa ya jamii wanayoiwakilisha, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono hoja nzuri na kupinga zile zinazoonekana kukinzana na maslahi ya jumla ya kitaifa. Hapa tena Mnyika anang'ara
Jukumu jingine la msingi sana la mbunge ni la kisera. Bunge ni ni chombo cha kutathmini mwenendo wa jumla wa kisera wa serikali na kutathmini mabadiliko yanayofaa. Hapa pia mchango wa Mnyika ni mkubwa sana.