Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Hawakustahili hata hayo majibu mazuri kiasi kile, Nape na R1, Mnyika ni babu kubwa kwenu, nyinyi mnabebwa na nyadhifa za baba zenu kijana anapasua kwa uwezo wake, bisheni mpaka mfeee lakini ndo ukweli.
...mkuu hapo kwenye red ndipo penye point hasa!
January inasemekana aliiba mitihani ya form four Galanos - hajakanusha hadi leo. mwizi huyu aliwezaje kupenya hadi chuo kikuu marekani kama si MICHONGO YA BABAYAKE:
Nape form IV alipata div IV point 29 na form six yake ya ??BUTIMBA HIGH SCHOOL -lakini kaenda India kusoma degree.
Kati ya hawa hakuna anayeweza kujenga hoja ya viwango vya form six wetu MNYIKA -Hata Prof Maghembe mwenyewe alimkimbia.
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa.

Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.

Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.

Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.

Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita.

Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno. Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.

Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo.

Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi.

Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree).

Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo. Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.

Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.

Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.

Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.

Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.

Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu.

Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu. Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi.

Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.

Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.

Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu.

Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani. Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita).

Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa. Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?

JJ


JJ i greet you!
shukran kwa maelezo mazuri ila nina ushauri kidogo kwako! kwanza kabisa sidhani kama kuna mtu ana tatizo juu ya kipaji chako katika uongozi pamoja na misuko suko yoote uliyopitia cha msingi ukumbuke kila jambo lina sababu! maana yoote hayo yametokea ili uwe JJ tunaye kufahamu hivi sasa so ondoa kinyongo kwa woote walio kusulubu au kufanya maisha yako kuwa magumu wakati huo ndio dynamics zenyewe za maisha!

pili, pamoja na kipaji chako, najujua kwamba wajua ila sinabudi kukumbusha kwamba heshima ni muhimu sana kwa kiongozi wa calibre na umri wako, so waheshimu watu wote bila kujali itikadi, dini au jinsia. nasema hivyo sababu kila unapo taja serikali lazima useme, serikali ya CCM hamnaga serikali ya chama fulani kuna serikali ya TANZANIA! na hata CDM kama mtachukua nchi mwaka 2015 itakuwa serikali ya TANZANIA si serikali ya CDM! Mwalimu Nyerere aliisha twambia dhambi ya ubaguzi hainaga mwisho ni kama kula nyama ya mtu, ukiila utaendelea tu!

nne, katika CDM kuna kiongozi mmoja muungwana sana japo hatunaye tena nafikiri bado unamkumbuka marehemu RM (R.I.P) kwa cdm so far ni yeye tu ndiye role mode kwa uungwana wake so jaribu kujifunaza na kuendeleza mema yake

ni hayo tu JJ, I wish you all the best kwe mapambano!
 
Tanzania ni nchi ya pekee duniani ambako wenye akili wanabezwa na waliobebwa na mfumo mbaya wa kiuchumi na maisha. LEO NAPE na R1, HATA JANUARY MAKAMBA hawana uwezo kiakili wa mmuuliza JJ kuhusu shule yake.
 
Makamanda endeleeni kujiliwaza ila ukweli utabaki kama ulivyo kwa mimi niliyekwenda shule na ku graduate university Mnyika namregard kama ni mtu wa kidato cha sita tu; hizi hoja eti aliacha chuo kwa kupigania uhuru ambao Tanzania tulishaupata hazina mshiko hata kidogo; Robert Mugabe alikuwa mpigania uhuru wa kushika bunduki na alimaliza elimu ya chuo kikuu akiwa porini itakuwa Mnyika aliyeishi mjini? kama alishindwa kusoma na aseme vinginevyo na arudi shule amalize hiyo degree ya BBA hizi ngonjera zake atafute pa kuzipeleka!
CC Ritz
 
Last edited by a moderator:
Makamanda endeleeni kujiliwaza ila ukweli utabaki kama ulivyo kwa mimi niliyekwenda shule na ku graduate university Mnyika namregard kama ni mtu wa kidato cha sita tu; hizi hoja eti aliacha chuo kwa kupigania uhuru ambao Tanzania tulishaupata hazina mshiko hata kidogo; Robert Mugabe alikuwa mpigania uhuru wa kushika bunduki na alimaliza elimu ya chuo kikuu akiwa porini itakuwa Mnyika aliyeishi mjini? kama alishindwa kusoma na aseme vinginevyo na arudi shule amalize hiyo degree ya BBA hizi ngonjera zake atafute pa kuzipeleka!
CC Ritz

Mkuu hapa hakuna ngonjera Mnyika kaleza kila kitu kuhusu elimu yake. Wewe ndio unaleta ngonjera, soma vizuri habari yote. Inawezekana hukuisoma yote.
 
Last edited by a moderator:
Keep it up Mnyika, nilisikia tu vijana wakisema wewe kichani ni hatari na ulipata Dv. ya pt 7, japo ulipata Dv 2 form VI nimegundua ni kwa kuwa ulikuwa too busy na mambo ya kijamii. Hata hivyo bado ni Dv, Nzuri ya kwenda Chuo. Cha msingi, punguza majukumu, ninakutakia kila la heri maliza degree, pata masters faster hata kwa Open University kuna MCED ambayo wanasoma kwa semester 3 tu na kila moja ni wiki 2. Ukimaliza anza PhD, hii unasoma at your time. Kwa mantiki hii ninaomba sana Nape na Ridhiwan waweke CV yao short hapa kama ya kwako halafu tufanye comparison!!!! You are a talent, Mnyika!

Bwana Zogwale,naona uko obsessed na kitu kinachoitwa degree na Phd!
Nafikiri unareflect jamii ya kitanzania.Ndio maana wabunge wengi wana Phd fake,kama Nagu,Nchimbi,Makanga etc na akina Lukuvi eti wana digrii!!!!

Phd ya nini kwa Mnyika?Hosea ,Feleshi na Magufuli wana Phd za ukubwani toka UDSM ,angalia utumbo wanaofanya.

Kumbuka Bill Gate wa Microsoft ni drop out,na yule marehemu wa apple,Steve Jobs vilevile.
Cabinet ya sasa ina ma Phd wengi,lakini ni janga la taifa,incompetence ya hali ya juu.

Mnyika ni very intelligent guy,point 7 sio mchezo,wengi tuliosoma Form 4 tunajua ni nini.Nilikuwa na one ya point 14.Thubutu point 7

Mnyika na Slaa,hawa ni hazina katika taifa.Wanafuata liberation theology,kwamba umkomboe mtu kimawazo,kiuchumi,na kutoka ukoloni(mweusi) kwa better katika society.
 
I salute you Mnyika! Kuwa best student Dar nzima na kupata A tisa, only stiff-necked fools ndo watapinga!
Cc: chama
 
Last edited by a moderator:
Mkuu muda huu tu nimeisoma Short brief ya mnyika kuna thred alianzisha. Alipata Div pt 7 akiwa na A 9. Alichaguliwa kidato cha 6 mkoani ila akaamua kwenda Tambaza na hapo alianza harakati mbalimbali kwa hiyo muda mwingi alichanganya shule na masomo na akapata Dv 2 Form 6. Alienda Chuo kusoma BBA ila walimwekea vikwazo kwa sababu ya uanaharakati wake. Hivyo hakumaliza ila ana mpango wa kuendelea. Ni jembe hili. Kina Rizimoja na Nape waweke na zao tuchambue.


Nape alishawai kuweka hapa jamvini CV yake ya magumashi aliyoichakachua inayoonyesha amesoma Form 5 & 6 Butimba TTC... Wadau wakahoji tokea lini Butimba imekuwa Secondary School?... Maji yalipofika shingoni, Nape akatoka mbio...
 
Naomba kwa heshima na taadhima angalau wakili na mwanasheria ridhiwan kikwete naye atuambie amesimamia kesi ngapi na kushinda walau kesi moja tu tangu amehitimu sheria na hadi kutawazwa kuwa wakili.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ningependekeza kama hutakuwa umetetea kesi walau 5 kwa mwaka basi uwakili wako uwe pending...- maana kuna mawakili nchini kwetu ambao hawajawahi kutetea hata kesi moja toka watunukiwe huo uwakili kwa mbwembwe na vifijo viwanja vya karimjee.
 
ridhiwan kikwete, anachojua na kuiba hasa mgodi wa gold Buzwagi-Kahama
 
Last edited by a moderator:
Nadhani Ridhiwani ataanza kuwa wakili baada ya 2015 kwa sasa hivi yuko katika jitihada za kuiba kadri anavyoweza maana muda unaelekea ukingoni!
 
JJ i greet you!
shukran kwa maelezo mazuri ila nina ushauri kidogo kwako! kwanza kabisa sidhani kama kuna mtu ana tatizo juu ya kipaji chako katika uongozi pamoja na misuko suko yoote uliyopitia cha msingi ukumbuke kila jambo lina sababu! maana yoote hayo yametokea ili uwe JJ tunaye kufahamu hivi sasa so ondoa kinyongo kwa woote walio kusulubu au kufanya maisha yako kuwa magumu wakati huo ndio dynamics zenyewe za maisha!

pili, pamoja na kipaji chako, najujua kwamba wajua ila sinabudi kukumbusha kwamba heshima ni muhimu sana kwa kiongozi wa calibre na umri wako, so waheshimu watu wote bila kujali itikadi, dini au jinsia. nasema hivyo sababu kila unapo taja serikali lazima useme, serikali ya CCM hamnaga serikali ya chama fulani kuna serikali ya TANZANIA! na hata CDM kama mtachukua nchi mwaka 2015 itakuwa serikali ya TANZANIA si serikali ya CDM! Mwalimu Nyerere aliisha twambia dhambi ya ubaguzi hainaga mwisho ni kama kula nyama ya mtu, ukiila utaendelea tu!

nne, katika CDM kuna kiongozi mmoja muungwana sana japo hatunaye tena nafikiri bado unamkumbuka marehemu RM (R.I.P) kwa cdm so far ni yeye tu ndiye role mode kwa uungwana wake so jaribu kujifunaza na kuendeleza mema yake

ni hayo tu JJ, I wish you all the best kwe mapambano!


Mkuu ushauri wako, ulipaswa uwape viongozi wako wa CCM. Kwenye bunge mara kadhaa tumewasikia mawaziri wakitamka serekali ya CCM imefanya hiki ama kile, wabunge wa CCM nao wimbo ni huo huo, serekali ya ccm, na hasa wa viti maalum CCM. Hata viongozi wakuu wa nchi mara kwa mara hutamka serekali ya CCM kwenye hotuba zao. Sasa iweje leo umkosoe mheshimiwa Mnyika. Kweli nyani haoni_ _ _ _ _ _ _!!!
 
Nawe una cheti lakini haujaelimika hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuongoza na Kuwa na maDegreee.

Raisi wa Kwanza aliposema kuwa nchi kama nchi bado kuruusu wageni kuwekeza alikuwa na maana yake matokeo yake ni kama yanavyooneka leo kuwapa watu ambao kampeni zao mwanzo mwisho kusema vyama vyingine baada ya kueleza nini watafanya. elimu ina umuimu sana ata kama mtu amezaliwa kiongozi.......
 
Kwani kikwete elimu yake ni ya kiwango gani? Kama elimu ingekuwa ndio kigezo pekee cha uongozi hasa urais basi tanzania hakuna rais aliyewahi kuwa na sifa hizo! Hakuna rais professor hata mmoja wa Tanzania! Take it from me!
 
Back
Top Bottom