Majibu mabaya kwa mpenzi yasababisha mauaji: Mkasa wa kusikitishaA wa 'Mr. Blue'

Sajo

Platinum Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
4,540
Reaction score
8,256
Tarehe 29/04/2026 Mahakama Kuu ya Tanzania masjala ya Dar es Salaam imehitimisha kesi ya kusisimua na kusikitisha inayomhusisha Abdallah Miraji Mussa, maarufu kama "Mr. Blue", aliyepatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Ezenia Kamana. Kesi hiyo ilisajiliwa kama CRIMINAL SESSION CASE No. 5011 of 2025 kati ya JAMHURI dhidi ya ABDALLAH MIRAJI MUSSA @ MR. BLUE na ilisikilizwa na kutolewa hukumu na Mhe. Jaji Mbagwa. Ilidaiwa kuwa mshtakiwa na marehemu walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa miaka 4. Na mshtakiwa alikuwa na gari aina ya Porte lenye rangi ya blue, alilokua akilitumia kumtembelea Ezenia Tandika Maghorofani alikokuwa anaishi jambo lililopelekea mama wa Ezenia kumpa mshtakiwa jina la Mr. Blue

Chanzo cha Ugomvi: Majibu ya dharau kuhusu "Vijisenti"​

Simulizi hii ya maafa ilianza tarehe 19 Agosti 2024, pale mzozo wa kifedha ulipogeuka kuwa mauti. Siju hiyo Ezenia alikwenda Kariakoo kununua viti vya plastiki kwa ajili ya mgahawa wake. Mshtakiwa alifika Tandika na kumchukua kwenye gari lake la blue kisha safari ikaanza na wakaachana njiani. Baadae mshtakiwa alimpigia simu marehemu na kumwambia afike mitaa ya Maduka Mawili alipopaki gari akinsubiri. Kwa mujibu wa maelezo ya ungamo ya mshtakiwa, ugomvi ulianza baada ya Ezenia kumuomba kiasi cha Shilingi 100,000/= ombi ambalo mshtakiwa alidai hakuwa na uwezo wa kulitekeleza kwa wakati huo.

Mshtakiwa alipomkumbusha Ezenia kuhusu fedha alizompa hapo awali, kwamba alizitumiaje, marehemu Ezenia alijibu kwa dharau akisema kuwa fedha hizo ni "peanuts" (vijisenti) ambavyo havistahili hata kuzungumziwa, na kwamba angemrudishia. Jibu hilo lilimpa mshtakiwa hasira kali, ambapo alichukua kisu kilichokuwa chini ya kapeti ya gari lake na kumchoma Ezenia kikatili hadi kifo kilipomfika. Alimchoma kisu na hakukitoa mpaka Ezenia alipokufa.

Tukio la Kinyama na Jitihada za Kuficha Uhalifu​

Baada ya mauaji hayo yaliyotokea maeneo ya Chang’ombe Maduka Mawili, mshtakiwa hakumpeleka marehemu hospitalini. Badala yake, alipeleka mwili huo nyumbani kwake Sinza, ambapo aliuingiza kwenye chumba chake cha mazoezi na kuukata mwili vipande vipande na kuuweka kwenye mifuko ya sandarusi (sarufeti).

Ili kuficha ushahidi, mshtakiwa alitupa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ikiwemo Kunduchi, Silver Sand, Tegeta Block D na Ununio Kilimo Kwanza.

Hata hivyo, ushahidi wa kisayansi (DNA) uliofanyiwa kazi na Mkemia wa Serikali ulithibitisha kuwa damu iliyopatikana kwenye makali ya kisu na panga la mshtakiwa ilikuwa ya marehemu Ezenia. Aidha, mtoto wa kaka yake mshtakiwa alithibitisha kuwa mshtakiwa alimpa Tshs. 5,000/= na kumtuma kununua mifuko mitano ya sandarusi siku ya tukio, ambapo alinunua mifuko ya kijani na ndiyo hiyohiyo iliyokutwa na sehemu za mwili wa Ezenia.

Hukumu ya Kifo​

Licha ya mshtakiwa kujitetea kwa kudai kuwa alikiri kumuua Ezenia kwa kuwa aliteswa na polisi na kukana uhusiano wa kimapenzi na marehemu, Jaji A.A. Mbagwa aliridhika na ushahidi wa mazingira uliowasilishwa na upande wa Jamhuri na hasa ukizingatia kuwa mtuhumiwa alikuwa ndio mtu wa mwisho kuonekana na marehemu.

Mahakama ilibaini kuwa kitendo cha kumuua mtu kwa sababu ya majibu ya dharau ni kinyume cha kifungu na 196 na 197 cha Kanuni ya Adhabu toleo la mwaka 2022 na hakiondoi nia ovu (malice aforethought). Mnamo tarehe 29 Aprili 2026, Abdallah Miraji Mussa alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa hadi kufa, ikiwa ni fundisho kwa jamii dhidi ya vitendo vya kikatili vinavyotokana na migogoro ya mapenzi

Hukumu kamili soma hapa: Republic vs Abdallah Miraji Mussa@ Mr. Blue (Criminal Sessions Case No. 5011 of 2025) [2026] TZHC 1822 (29 April 2026)
 
kusikitisha inayomhusisha Abdallah Miraji Mussa, maarufu kama "Mr. Blue"
Mr. Blue, the celebrated Tanzanian Bongo Flava artist, is the stage name of Khery Sameer Rajab, born on April 14, 1987. Rising to prominence with his hit track "Mapozi," Mr. Blue has captivated audiences with his distinctive voice, artistic versatility, and enduring contributions to the music industry. Explore the complete collection of Mr. Blue's songs—stream, download, and experience

Imebidi niingie maktaba kwanza duu
 
We nawe! Sio Mr Blue mwanamziki, hiyo Mr blue mtuhumiwa alipewa aka tu kwasababu alikuwa anatumia gari ya blue
 
Shetani ananguvu sanaa

Sawa umeshaua sasa nguvu ya kumkata kata binaadamu mwenzako vipande vipande unaitoa wap? Ujasiri huo unautoa wap?

M/Mungu anihepushe inshaAllah
Ni balaa, ukiua sijui unakua umechanganyikiwa. Jamaa alikata vipande vipande na kutupa sehemu tofauti tofauti. Daktari aliviunga unga mpaka vikatengeneza umbo la binadamu, na DNA ikasaidia kuthibitisha.
 
Mr. Blue, the celebrated Tanzanian Bongo Flava artist, is the stage name of Khery Sameer Rajab, born on April 14, 1987. Rising to prominence with his hit track "Mapozi," Mr. Blue has captivated audiences with his distinctive voice, artistic versatility, and enduring contributions to the music industry. Explore the complete collection of Mr. Blue's songs—stream, download, and experience

Imebidi niingie maktaba kwanza duu
Mkuu, Mr. Blue wa hii kesi ni tofauti na Kabaisa.. huyu alipewa nickname na mama mkwe sababu jamaa alikuwa na gari la bluu
 
Huyu jaji feki nini? Yaani jaji anashindwa kutofautisha kati ya ‘Murder in the first degree) na ‘Murder in the second degree’?

Huyo hakupanga kufanya mauaji, bali alishtukizwa na mazingira, na adhabu yake sio kifo.

=========================

Murder in the first degree is the most serious form of homicide, defined as an intentional, willful, and premeditated killing with malice aforethought. It often includes killings committed during dangerous felonies (felony murder), such as robbery or kidnapping, and is characterized by planning or extreme indifference to life. [1, 2, 3]
Key Elements and Characteristics
  • Premeditation and Deliberation: The killer planned or thought about the murder before acting.
  • Specific Intent: The purpose was to cause the death of another person.
  • Felony Murder: A death occurring during the commission or attempted commission of a dangerous felony (e.g., arson, rape, robbery).
  • Special Circumstances: In many jurisdictions, this includes killing a police officer or public official. [1, 2, 3, 4]
Legal Context
  • Penalty: First-degree murder is a Class A felony, often resulting in life imprisonment without parole or, in some jurisdictions, the death penalty.
  • Distinction: Unlike second-degree murder, which may be a "spur of the moment" killing, first-degree requires evidence of planning or extreme cruelty.
  • Examples: Poisoning, lying in wait, or planning a murder for financial gain
 
Mr. Blue, the celebrated Tanzanian Bongo Flava artist, is the stage name of Khery Sameer Rajab, born on April 14, 1987. Rising to prominence with his hit track "Mapozi," Mr. Blue has captivated audiences with his distinctive voice, artistic versatility, and enduring contributions to the music industry. Explore the complete collection of Mr. Blue's songs—stream, download, and experience

Imebidi niingie maktaba kwanza duu

Sasa weye umefanya kituko gani hapa🤣

Ni kusoma hiyo naaaaah, hata kuchuchungulia udakue hata majina naaaaah huwezi

Ukaenda bila kusoma nawe huyooo . .. Ulifikiri utakuwa wa kwanza kufungua kikodi kwa kutaja jina eeeeh .. Jiongeze kwa manufaa yako...

inayomhusisha Abdallah Miraji Mussa, maarufu kama "Mr. Blue",
 
Wataalamu wa sheria tusaidieni hapa,

Hii ni Manslaughter au ni Murder?

Mtuhumiwa hakua amepanga hilo tukio la mauaji bali mauaji yalisababishwa na hasira ya majibu mabaya kutoka kwa huyo mpenzi wake,

Simtetei huyo muuaji wala sitetei alicho kifanya bali nataka kujua kuhusu sheria kati ya Manslaughter na Murder.
 
Kwa dunia ya leo, mapenzi yataondoka na wengi sana. Pengine jamaa hakutimiza hta mambo yake muhimu ya kimaisha ili tu amridhishe marehemu, mwisho wa siku unakuja kutolewa shit kwamba vile vilikua vijisenti tu, sawa ! yawezekana vilikua ni visijenti ila kwake vilikua na thamani, hutujui alirisk nini ili ampatie yeye.
 
Tarehe 29/04/2026 Mahakama Kuu ya Tanzania masjala ya Dar es Salaam imehitimisha kesi ya kusisimua na kusikitisha inayomhusisha Abdallah Miraji Mussa, maarufu kama "Mr. Blue", aliyepatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Ezenia Kamana. Kesi hiyo ilisajiliwa kama CRIMINAL SESSION CASE No. 5011 of 2025 kati ya JAMHURI dhidi ya ABDALLAH MIRAJI MUSSA @ MR. BLUE na ilisikilizwa na kutolewa hukumu na Mhe. Jaji Mbagwa. Ilidaiwa kuwa mshtakiwa na marehemu walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa miaka 4. Na mshtakiwa alikuwa na gari aina ya Porte lenye rangi ya blue, alilokua akilitumia kumtembelea Ezenia Tandika Maghorofani alikokuwa anaishi jambo lililopelekea mama wa Ezenia kumpa mshtakiwa jina la Mr. Blue

Chanzo cha Ugomvi: Majibu ya dharau kuhusu "Vijisenti"​

Simulizi hii ya maafa ilianza tarehe 19 Agosti 2024, pale mzozo wa kifedha ulipogeuka kuwa mauti. Siju hiyo Ezenia alikwenda Kariakoo kununua viti vya plastiki kwa ajili ya mgahawa wake. Mshtakiwa alifika Tandika na kumchukua kwenye gari lake la blue kisha safari ikaanza na wakaachana njiani. Baadae mshtakiwa alimpigia simu marehemu na kumwambia afike mitaa ya Maduka Mawili alipopaki gari akinsubiri. Kwa mujibu wa maelezo ya ungamo ya mshtakiwa, ugomvi ulianza baada ya Ezenia kumuomba kiasi cha Shilingi 100,000/= ombi ambalo mshtakiwa alidai hakuwa na uwezo wa kulitekeleza kwa wakati huo.

Mshtakiwa alipomkumbusha Ezenia kuhusu fedha alizompa hapo awali, kwamba alizitumiaje, marehemu Ezenia alijibu kwa dharau akisema kuwa fedha hizo ni "peanuts" (vijisenti) ambavyo havistahili hata kuzungumziwa, na kwamba angemrudishia. Jibu hilo lilimpa mshtakiwa hasira kali, ambapo alichukua kisu kilichokuwa chini ya kapeti ya gari lake na kumchoma Ezenia kikatili hadi kifo kilipomfika. Alimchoma kisu na hakukitoa mpaka Ezenia alipokufa.

Tukio la Kinyama na Jitihada za Kuficha Uhalifu​

Baada ya mauaji hayo yaliyotokea maeneo ya Chang’ombe Maduka Mawili, mshtakiwa hakumpeleka marehemu hospitalini. Badala yake, alipeleka mwili huo nyumbani kwake Sinza, ambapo aliuingiza kwenye chumba chake cha mazoezi na kuukata mwili vipande vipande na kuuweka kwenye mifuko ya sandarusi (sarufeti).

Ili kuficha ushahidi, mshtakiwa alitupa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ikiwemo Kunduchi, Silver Sand, Tegeta Block D na Ununio Kilimo Kwanza.

Hata hivyo, ushahidi wa kisayansi (DNA) uliofanyiwa kazi na Mkemia wa Serikali ulithibitisha kuwa damu iliyopatikana kwenye makali ya kisu na panga la mshtakiwa ilikuwa ya marehemu Ezenia. Aidha, mtoto wa kaka yake mshtakiwa alithibitisha kuwa mshtakiwa alimpa Tshs. 5,000/= na kumtuma kununua mifuko mitano ya sandarusi siku ya tukio, ambapo alinunua mifuko ya kijani na ndiyo hiyohiyo iliyokutwa na sehemu za mwili wa Ezenia.

Hukumu ya Kifo​

Licha ya mshtakiwa kujitetea kwa kudai kuwa alikiri kumuua Ezenia kwa kuwa aliteswa na polisi na kukana uhusiano wa kimapenzi na marehemu, Jaji A.A. Mbagwa aliridhika na ushahidi wa mazingira uliowasilishwa na upande wa Jamhuri na hasa ukizingatia kuwa mtuhumiwa alikuwa ndio mtu wa mwisho kuonekana na marehemu.

Mahakama ilibaini kuwa kitendo cha kumuua mtu kwa sababu ya majibu ya dharau ni kinyume cha kifungu na 196 na 197 cha Kanuni ya Adhabu toleo la mwaka 2022 na hakiondoi nia ovu (malice aforethought). Mnamo tarehe 29 Aprili 2026, Abdallah Miraji Mussa alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa hadi kufa, ikiwa ni fundisho kwa jamii dhidi ya vitendo vya kikatili vinavyotokana na migogoro ya mapenzi

Hukumu kamili soma hapa: Republic vs Abdallah Miraji Mussa@ Mr. Blue (Criminal Sessions Case No. 5011 of 2025) [2026] TZHC 1822 (29 April 2026)
Procedure zote alizozitumia inaonesha wazi jamaa ni muuaji mzoefi.
 
Sasa weye umefanya kituko gani hapa🤣

Ni kusoma hiyo naaaaah, hata kuchuchungulia udakue hata majina naaaaah huwezi

Ukaenda bila kusoma nawe huyooo . .. Ulifikiri utakuwa wa kwanza kufungua kikodi kwa kutaja jina eeeeh .. Jiongeze kwa manufaa yako...
Wanawake wapunguze tamaa na siyo kila mwanaume ni wa kumrukia na kumchezea feelings,kuna wengine pesa zao wakitoa haziliwi ovyoovyo

Ova
 
Tarehe 29/04/2026 Mahakama Kuu ya Tanzania masjala ya Dar es Salaam imehitimisha kesi ya kusisimua na kusikitisha inayomhusisha Abdallah Miraji Mussa, maarufu kama "Mr. Blue", aliyepatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Ezenia Kamana. Kesi hiyo ilisajiliwa kama CRIMINAL SESSION CASE No. 5011 of 2025 kati ya JAMHURI dhidi ya ABDALLAH MIRAJI MUSSA @ MR. BLUE na ilisikilizwa na kutolewa hukumu na Mhe. Jaji Mbagwa. Ilidaiwa kuwa mshtakiwa na marehemu walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa miaka 4. Na mshtakiwa alikuwa na gari aina ya Porte lenye rangi ya blue, alilokua akilitumia kumtembelea Ezenia Tandika Maghorofani alikokuwa anaishi jambo lililopelekea mama wa Ezenia kumpa mshtakiwa jina la Mr. Blue

Chanzo cha Ugomvi: Majibu ya dharau kuhusu "Vijisenti"​

Simulizi hii ya maafa ilianza tarehe 19 Agosti 2024, pale mzozo wa kifedha ulipogeuka kuwa mauti. Siju hiyo Ezenia alikwenda Kariakoo kununua viti vya plastiki kwa ajili ya mgahawa wake. Mshtakiwa alifika Tandika na kumchukua kwenye gari lake la blue kisha safari ikaanza na wakaachana njiani. Baadae mshtakiwa alimpigia simu marehemu na kumwambia afike mitaa ya Maduka Mawili alipopaki gari akinsubiri. Kwa mujibu wa maelezo ya ungamo ya mshtakiwa, ugomvi ulianza baada ya Ezenia kumuomba kiasi cha Shilingi 100,000/= ombi ambalo mshtakiwa alidai hakuwa na uwezo wa kulitekeleza kwa wakati huo.

Mshtakiwa alipomkumbusha Ezenia kuhusu fedha alizompa hapo awali, kwamba alizitumiaje, marehemu Ezenia alijibu kwa dharau akisema kuwa fedha hizo ni "peanuts" (vijisenti) ambavyo havistahili hata kuzungumziwa, na kwamba angemrudishia. Jibu hilo lilimpa mshtakiwa hasira kali, ambapo alichukua kisu kilichokuwa chini ya kapeti ya gari lake na kumchoma Ezenia kikatili hadi kifo kilipomfika. Alimchoma kisu na hakukitoa mpaka Ezenia alipokufa.

Tukio la Kinyama na Jitihada za Kuficha Uhalifu​

Baada ya mauaji hayo yaliyotokea maeneo ya Chang’ombe Maduka Mawili, mshtakiwa hakumpeleka marehemu hospitalini. Badala yake, alipeleka mwili huo nyumbani kwake Sinza, ambapo aliuingiza kwenye chumba chake cha mazoezi na kuukata mwili vipande vipande na kuuweka kwenye mifuko ya sandarusi (sarufeti).

Ili kuficha ushahidi, mshtakiwa alitupa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ikiwemo Kunduchi, Silver Sand, Tegeta Block D na Ununio Kilimo Kwanza.

Hata hivyo, ushahidi wa kisayansi (DNA) uliofanyiwa kazi na Mkemia wa Serikali ulithibitisha kuwa damu iliyopatikana kwenye makali ya kisu na panga la mshtakiwa ilikuwa ya marehemu Ezenia. Aidha, mtoto wa kaka yake mshtakiwa alithibitisha kuwa mshtakiwa alimpa Tshs. 5,000/= na kumtuma kununua mifuko mitano ya sandarusi siku ya tukio, ambapo alinunua mifuko ya kijani na ndiyo hiyohiyo iliyokutwa na sehemu za mwili wa Ezenia.

Hukumu ya Kifo​

Licha ya mshtakiwa kujitetea kwa kudai kuwa alikiri kumuua Ezenia kwa kuwa aliteswa na polisi na kukana uhusiano wa kimapenzi na marehemu, Jaji A.A. Mbagwa aliridhika na ushahidi wa mazingira uliowasilishwa na upande wa Jamhuri na hasa ukizingatia kuwa mtuhumiwa alikuwa ndio mtu wa mwisho kuonekana na marehemu.

Mahakama ilibaini kuwa kitendo cha kumuua mtu kwa sababu ya majibu ya dharau ni kinyume cha kifungu na 196 na 197 cha Kanuni ya Adhabu toleo la mwaka 2022 na hakiondoi nia ovu (malice aforethought). Mnamo tarehe 29 Aprili 2026, Abdallah Miraji Mussa alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa hadi kufa, ikiwa ni fundisho kwa jamii dhidi ya vitendo vya kikatili vinavyotokana na migogoro ya mapenzi

Hukumu kamili soma hapa: Republic vs Abdallah Miraji Mussa@ Mr. Blue (Criminal Sessions Case No. 5011 of 2025) [2026] TZHC 1822 (29 April 2026)
Majibu ya Baadhi ya wanawake ukiwa na moyo mwepesi unaweza ukaungana na Khamis magunia ya mkaa au Mr Blue LUPANGO.
 
Huyu jaji feki nini? Yaani jaji anashindwa kutofautisha kati ya ‘Murder in the first degree) na ‘Murder in the second degree’?

Huyo hakupanga kufanya mauaji, bali alishtukizwa na mazingira, na adhabu yake sio kifo.

=========================

Murder in the first degree is the most serious form of homicide, defined as an intentional, willful, and premeditated killing with malice aforethought. It often includes killings committed during dangerous felonies (felony murder), such as robbery or kidnapping, and is characterized by planning or extreme indifference to life. [1, 2, 3]
Key Elements and Characteristics
  • Premeditation and Deliberation: The killer planned or thought about the murder before acting.
  • Specific Intent: The purpose was to cause the death of another person.
  • Felony Murder: A death occurring during the commission or attempted commission of a dangerous felony (e.g., arson, rape, robbery).
  • Special Circumstances: In many jurisdictions, this includes killing a police officer or public official. [1, 2, 3, 4]
Legal Context
  • Penalty: First-degree murder is a Class A felony, often resulting in life imprisonment without parole or, in some jurisdictions, the death penalty.
  • Distinction: Unlike second-degree murder, which may be a "spur of the moment" killing, first-degree requires evidence of planning or extreme cruelty.
  • Examples: Poisoning, lying in wait, or planning a murder for financial gain
So jamaa akate rufaa? Ndugu wakili
 
Kwa dunia ya leo, mapenzi yataondoka na wengi sana. Pengine jamaa hakutimiza hta mambo yake muhimu ya kimaisha ili tu amridhishe marehemu, mwisho wa siku unakuja kutolewa shit kwamba vile vilikua vijisenti tu, sawa ! yawezekana vilikua ni visijenti ila kwake vilikua na thamani, hutujui alirisk nini ili ampatie yeye.
Ndio maana tume ya jaji chande ikapita na haya matukio
 
Back
Top Bottom