In any case Ujenzi huu ni wa gharama mno!! Kwa kweli kusema hapa nimetumia shillingi kadhaa hilo ni rahisi mno, especially kwenye ujenzi. Mnaweza mkajenga nyumba zinazofanana na kulingana na kuwa na vitu vinavyofanana kabisa; lakini mmoja akajenga kwa gharama mara kumi zaidi ya mwingine. Hakuna standards, isipokuwa kuna value for money!!
Tusiingie sana kwenye jargon ya ujenzi, tukubaliane kuwa hapo hakuna value for money. Benki kuu waliwagawia wajenzi fedha tu kwa kuwa zipo na hapa ndo linapokuja suala kubwa zaidi la INSTITUTIONALIZED CORRUPTION. Kwamba katika ujenzi huu kitu kinachoitwa kuangalia thamani halisi ya fedha na kitu tunachopata haikuwepo.
Katika nchi yoyote ile kwenye uso wa dunia hii Nyumba ya kuishi mtu mmoja yenye thamani ya Dola million moja ni nyumba ya gharama sana. Kwa Tanzania wakati tunalia umaskini na kuomba omba kila siku ni ajabu na kweli kuwa tunaweza kutumia fedha yetu wenyewe kumjengea nyumba mtu mwenye hadhi ya Gavana wa Benki kuu ya nchi yetu nyumba ya gharama kubwa kiasi hicho. Mtu ambaye kutokana na ukubwa wa mshahara wake na wingi wa marupurupu anayolipwa ana uwezo wa kujenga nyumba ya kwake na kukaa humo.
Wanaotetea uchafu huo mara nyingi wamejificha kwenye sheria zetu na taratibu zetu kuwa zinaruhusu hicho. Lakini wanaopinga wanaangalia hali halisi ya uwezo wetu na sera zetu. Jambo hili ni halali na ni busara kufanya hivyo? Inawezekana ni halali kufanya hivyo alivyofanya Gavana wa benki kuu, lakini si busara hata kidogo. Si busara kwa sababu hapa ndo inatakiwa tuoneshe kuwajibika!! Kumbe tunaomba omba halafu tunatapanya? eti tu kwa kuwa sheria na taratibu zetu zinaruhusu? Na hizi sheria na taratibu zetu wenye uwezo wa kuzibadilisha si ni hao hao wanaozitumia kuwabaka watanzania maskini? Kama wana busara kwa nini wasizibadilishe hizi sheria na taratibu zikaonesha responsibility kidogo? Au kwani sheria zote na taratibu lazima zitumike kama zilivyo wakati tunajua zilitungwa na kuwekwa wakati sera zetu ilikuwa tofauti. Hapa ni ukosefu wa kuwajibika kwa viongozi wetu!
Hawa watu wanaotaka kuishi kwenye nyumba za thamani ya Dola milion moja kwa nini wasiende kufanya biashara huko mitaani, wapate faida hadi wajenge majumba hayo? Kwa nini walio kwenye utumishi wa umma (naam Benki kuu ni utumishi wa umma) wasikubali kuishi maisha ya kawaida? Nasema tena na tena, HAYA NI MASALIA YA UJAMAA. Hakuna mabepari duniani wanaofanya hivyo. Kwa mabepari ukitaka maisha ya kitajiri, kafanye biashara zako. Katika ujamaa, uongozi wa umma ndo chanzo cha utajiri na maisha ya kitajiri.
Benno Ndullu, pamoja na kufanya kazi world bank, mentality yake ni Ujamaa. Na hapo ndo huwa nasema, bado tuna shida, tena kubwa. Viongozi wengi, hata huyo waziri wa sheria anayesema Tanzania ni nchi ya Kibepari, hajui maana ya ubepari.
Ubepari ni siasa makini sana ambayo haiwezi kuruhusu upuuzi huu wa viongozi kujifanya ndo kila kitu. Kwenye ubepari viongozi wamedhibitiwa vilivyo na hawawezi kufanya upuuzi kama huu ndo maana ubepari umeshinda!