Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je hili ni tatizo la client ama contractor?
Hawajajibu chochote bali usanii tu!
Sisi watanzania na viongozi wetu wote ni wajinga na wapumbavu wakubwa.
ni break down nzuri na imekaa KITAALAMU!lakini kwanin irushwe leo?
HELA YA KAWAIDA SANA HIYO!hebu kasome specifications na requirements,EBO! why are you guys interested in figures?labda mngeshauri wabadilishe DESIGN
Na wapitie BQ ili kuona mtiririko mzima...
Du! Tanzania safari ndefu...sasa hamjaelewa nini? kwenye ripoti mumeambiwa hivi, mkaguzi wenu atafika na kukagua hayo mahesabu kama sheria inavyotaka.
Si msubiri hapo basi ndio mseme wapi kuna tatizo?
Hivi Ndulu amefika kampuni zimeshapewa tender mlitaka akatishe hizo tenda mwajua gharama yake?
Kuomba B.O.Q hakusaidii especially baada ya kuambiwa kwamba aliyepewa tenda ni yule mwenye bei ya chini!!! So BOQ itakusaidia nini? Tunajadili nini hapa? Mbona siwaelewi?
inawezekana tunajadili siasa!..ambayo naamini siiwezi.nisaidie kitu kimoja :
UNAPOSEMA PESA NI NYINGI UMEBASE KWENYE NIN?i mean una refer kitu gani?
I have no problems with that.
hata mimi sina tatizo na hiyo reports
So do I!
Swali zuri sana, majibu yake yako kwenye bei za makandasi walio-omba hiyo kazi.
Yaani majibu ya benki kuu ni aibu tupu!! Wao wanajibu kana kwamba sisi tunalalamika ujenzi haujafanyika kwa kufuata sheria.
HAPANA!! SISI TUNA HASIRA KUBWA KWENYE MATUMIZI YA PESA ZETU NDOGO KWENYE VITU AMBAVYO HAVITUSAIDII WANANCHI KWA UJUMLA.
Bungeni kila kukicha wabunge wakiuliza maswali, hospitali ya wilaya haina dawa, haina vitanda vya kulala wagonjwa, shule hazina madawati, barabara mbovu, Majibu ya mawaziri siku zote ni UWEZO MDOGO WA SERIKALI KIFEDHA NDIO SABABU HAKUNA VITANDA< MADAWATI BLAH BLAH
Lakini likija suala lakutumia mabilioni kwenye nyumba au kulipa posho za safari zisizokwisha na kununua mashangingi kwa kasi za ajabu, GHAFLA SERIKALI INA KUWA NA PESA.
Sasa issue hapa ni PRIORITY ya pesa zetu wananchi na nashangaa benki kuu wanajibu utadhani pesa ni zao na wanaona sifa namna walivyotumbua hizo 3 bilioni kwenye nyumba mbili tu.
Huyu Dk. Enos analipwa posho sababu anakaa kwenye nyumba yake binafsi, Kuna mtu anataka kuweka BET na mimi kuwa huyu analipwa mamilioni kila mwezi kwa kusihi kwenye nyumba ambayo serikali ilimuuzia kwenye ule ufisadi wa Mkapa kwa bei ya chee kabisa.
Yaani unamuuzia mtu nyumba kwa bei ndogo, halafu bado ni mwajiriwa wa serikali na serikali hiyo hiyo inamlipa tena posho kubwa kwa kuishi kwenye hiyo nyumba, Sasa justification ya kumuuzia ile nyumba in the first place ni ipi??
Sisi watanzania na viongozi wetu wote ni wajinga na wapumbavu wakubwa.
Hawa watu wanaotaka kuishi kwenye nyumba za thamani ya Dola milion moja kwa nini wasiende kufanya biashara huko mitaani, wapate faida hadi wajenge majumba hayo? Kwa nini walio kwenye utumishi wa umma (naam Benki kuu ni utumishi wa umma) wasikubali kuishi maisha ya kawaida? Nasema tena na tena, HAYA NI MASALIA YA UJAMAA. Hakuna mabepari duniani wanaofanya hivyo. Kwa mabepari ukitaka maisha ya kitajiri, kafanye biashara zako. Katika ujamaa, uongozi wa umma ndo chanzo cha utajiri na maisha ya kitajiri.
Maswali ya kujiuliza,
3. Kama Benki kuu inaazimia kuwa bei hizi ni sawa (si kwa sababu ya bajeti) kutokana na hali halisi ya sekta ya ujenzi na nyumba Tanzania, je Uchumi wa Tanzania na safari ya Watanzania kuwezakujitegemea na kujijengea nyumba bora itafanikiwa vipi ikiwa kila siku kuna mfumuko wa bei za viwanja, hakuna sheria madhubuti za ardhi, na gharama za vifaa vya ujenzi na wajenzi ni kubwa kuliko sehemu nyingi duniani na ukipima uwiano wa umahiri wa Sarafu yetu?
Kinachobakia ni kuchapana bakora kama Senegal tu au Kenya maana walianzia huko huko, watu wanaona sawa kusquander $1.2 Million wakati hamuoni haya TRA wanawashikia bango wazee wetu vijijini na kodi ya maendeleo hata dawa hamna katika hospitali ya kijiji. Unadhani yule mzee ukimwambia kuna watu wanatumia Bilioni 1 kujenga nyumba ya kulala ya mtu mmoja watakuelewa????
Tunashukuru Reverend kwa kurudi kundini, maana tulivyo kuwa tunakemea/kupinga toka mwanzo ni kutokana vitu hivi hivi unavyo viongelea.Maswali ya kujiuliza,
1. Kwa nini bado tuna utamaduni wa mashirika, taasisi na Serikali kujengea wafanyakazi nyumba? Kwa nini wasijihudumie wao wenyewe kwa kutumia mishahara yao?
2. Kwa nini Benki Kuu kama mdhibiti wa Uchumi wa Tanzania ilikubali kujengewa nyumba kwa gharama za juu kiasi hiki, ukizingatia kuwa sekta ya Ujenzi inajipangia bei zake kiholelea na hakuna udhibiti wa mfumuko wa bei za viwanja na malighafi (vifaa vya ujenzi) unaofanyiwa uratibu na Serikali?
3. Kama Benki kuu inaazimia kuwa bei hizi ni sawa (si kwa sababu ya bajeti) kutokana na hali halisi ya sekta ya ujenzi na nyumba Tanzania, je Uchumi wa Tanzania na safari ya Watanzania kuwezakujitegemea na kujijengea nyumba bora itafanikiwa vipi ikiwa kila siku kuna mfumuko wa bei za viwanja, hakuna sheria madhubuti za ardhi, na gharama za vifaa vya ujenzi na wajenzi ni kubwa kuliko sehemu nyingi duniani na ukipima uwiano wa umahiri wa Sarafu yetu?
Maswali ya kujiuliza,
2. Kwa nini Benki Kuu kama mdhibiti wa Uchumi wa Tanzania ilikubali kujengewa nyumba kwa gharama za juu kiasi hiki, ukizingatia kuwa sekta ya Ujenzi inajipangia bei zake kiholelea na hakuna udhibiti wa mfumuko wa bei za viwanja na malighafi (vifaa vya ujenzi) unaofanyiwa uratibu na Serikali?
Reverend,
Why do you want to swallow your own vomit? Few days ago, you adamantly defended BOT's decision to build those houses solely because it's not tax payers' money. Now, you want to turn around and accuse them of the same thing you did defend them before. This is simply the zenith of hypocrisy. ......Sorry Reverend, you can't have both ways.