Majibu rasmi ya BoT juu ya nyumba ya Ndulu

Majibu rasmi ya BoT juu ya nyumba ya Ndulu

Kuomba B.O.Q hakusaidii especially baada ya kuambiwa kwamba aliyepewa tenda ni yule mwenye bei ya chini!!! So BOQ itakusaidia nini? Tunajadili nini hapa? Mbona siwaelewi?
inawezekana tunajadili siasa!..ambayo naamini siiwezi.nisaidie kitu kimoja :
UNAPOSEMA PESA NI NYINGI UMEBASE KWENYE NIN?i mean una refer kitu gani?
 
ni break down nzuri na imekaa KITAALAMU!lakini kwanin irushwe leo?

Imerushwa leo kwakuwa kuna gazeti moja limeendelea kutoa hizo habari. Ile ni taasisi nyeti lazima itoe maelezo maana watanzania hawataelewa.
I have no problems with that.
 
Imerushwa leo kwakuwa kuna gazeti moja limeendelea kutoa hizo habari. Ile ni taasisi nyeti lazima itoe maelezo maana watanzania hawataelewa.
I have no problems with that.
hata mimi sina tatizo na hiyo reports
 
Kula mle kuuliza tusiwaulize?

Lula wa Ndali-Mwananzela​
Disemba 30, 2009
BENKI Kuu wanataka kula tena; wanataka kula bila kuulizwa na yeyote; wanataka kula huku tukiwatazama. Si huku tunawatazama tu bali wanataka wale huku tukiwapigia makofi kwa jinsi gani wanakula vizuri.

Habari kuwa Benki Kuu imetumia zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu kujenga upya nyumba ya gavana wake ni habari za ulaji mwingine kwenye taasisi hiyo ulaji ambao walaji wake hawataki waulizwe!

Habari hizi zilizoripotiwa na gazeti moja la kila siku nchini zinadokeza kuwa Benki Kuu imetumia fedha hizo katika kumpatia Gavana wa Benki hiyo Profesa Benno Ndulu jumba la uhakika linaloendana na hadhi ya Gavana (wa Tanzania). Ingawa habari hizo zilidai kuwa fedha hizo zilitumika katika ukarabati siku chache baadaye gavana mwenyewe alijitokeza na kudai kuwa fedha hizo (au zaidi) hazikutumika katika ukarabati kama gazeti hilo lilivyodai bali zilitumika katika ujenzi mpya wa jumba la Gavana.

Ndullu alinukuliwa kudai kuwa "Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema" na hivyo kuhalalisha matumizi hayo ya fedha. Lakini zaidi alionekana kuchukizwa kwa kupatikana kwa habari hiyo akidai kuwa "Napenda taarifa sahihi ambazo hazipotoshi ukweli, kwa maana taarifa kama hizo zinaharibu kila kitu kizuri na kujengwa taswira mbaya kwa wananchi, kitu ambacho si sahihi. Pia si kweli kuhusu hizo gharama kwani hakuna tathmini kamili ambayo imekamilika hadi sasa".

Gavana Ndulu hakutaka kusema gharama halisi ya ujenzi wa jumba hilo ni kiasi gani na ni kwa nini ni kiasi hicho. Katika kufikiria suala hilo nimejikuta tena napigwa na bumbuazi la aibu; bumbuazi lililoniacha na maswali mengi kuliko majibu yake. Nilikuwa ninaamini kuwa mambo haya yalikuwa yanatokea wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa lakini sasa tunayashuhudia katika utawala wa Jakaya Kikwete na sitashangaa mwaka huu mmoja uliosalia tutaona mambo makubwa sana ya "ukarabati" hadi tunyofoe nywele zetu!

Ninajiuliza:
Profesa Ndulu amesema kuwa walichofanya si ukarabati bali ni ujenzi wa jumba jipya kabisa. Ningependa kujua kabla ya ujenzi wa jumba hilo eneo hilo lilikuwa na nyumba ya aina gani na kwa nini ililazimika kuvunjwa? Jibu hili ni muhimu kwani tusipoangalia wakuu wa taasisi mbalimbali watakapopewa majumba ya waliowatangulia nao watataka kujenga majumba mapya. Hivyo, ningependa kupewa jibu kwa nini Gavana wa BoT alihitaji jumba jipya?

Kwa vile jumba hili linadaiwa kugharibu zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu Gavana Ndulu anaweza kutupatia mchakato wa gharama za ujenzi wa jumba hili kiasi cha kuhalalisha matumizi makubwa ya fedha kiasi hicho?

Fedha zilizotumika zimetokana na mfuko gani? Swali hili ni muhimu kwani tangu habari hizi zimevuja kumekuwa na mjadala mkubwa wa fedha zilizotumika ni za walipa kodi au ni za Benki Kuu wenyewe na haziko katika usimamizi wa umma? Kama jawabu ni kuwa ni fedha za walipa kodi ni utaratibu gani ulitumiwa kuhalalisha hasa tukizingatia kuwa Gavana wa Benki Kuu ndiye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo? Na kama ni fedha za "benki kuu" kama baadhi ya watu wanavyoamini tunajuaje kuwa mchakato wa matumizi yake hauna mazingira ya kifisadi?

Kutokana na swali hilo hapo juu, hatuna budi kujiuliza kama Benki Kuu yetu ilivyo sasa haina tofauti na Benki Kuu ya Dk. Daudi Ballali? Mojawapo ya matatizo tuliyoyashuhudia wakati wa Gavana Ballali ni uwezo wa Gavana yule kuhalalisha malipo na matumizi makubwa ndani ya benki hiyo kwenda kwa makampuni hewa na hivyo kuwa sehemu ya ufisadi mkubwa.

Je, Gavana Ndulu kwa kuhalalisha matumizi haya anaweza kuelezea kuwa yanaendana na thamani kweli ya ujenzi wa jumba hilo na kwamba uchunguzi huru ukifanyika utahalalisha matumizi hayo?

Je, Gavana Ndulu yuko tayari kufungua vitabu vya Benki Kuu kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) au mkaguzi wa nje atakayeteuliwa na CAG kupitia mahesabu ya mapato na matumizi, hususan kwenye suala hili la ujenzi?
Katika kufanya hilo hapo juu, je, Gavana Ndulu anaweza kutuambia kuwa ujenzi huu wa hili jumba ulifanywa na kampuni gani iliyofanya hivyo kwa kushinda tenda gani iliyotangazwa lini na yenye vigezo gani?

Je, Benki Kuu inaweza kutuambia kuwa jumba hilo lililojengwa kwa fedha za Watanzania (ziwe zinazotokana na kodi yao au mtaji wao kwenye benki hiyo) lilitumia kiasi gani cha vifaa, ufundi, utaalamu, samani n.k kutoka ndani ya nchi yetu au ni yale yale ambapo hadi vitasa tunaagiza nje, mazuria nje, madirisha nje, makochi na vitambaa vya makochi kutoka nje?

Swali la mwisho ambalo ningependa kujua jibu lake ni kwa Gavana Ndulu kutuhalalishia kwa nini Gavana wa Tanzania akae kwenye jumba lenye gharama inayoshinda jumba la Gavana wa Benki Kuu ya Marekani, taifa kubwa zaidi lenye uchumi mkubwa na lenye matatizo ya kiuchumi ya kutosha tu?

Nina uhakika yapo maswali mengine lakini ningependa tuanze na haya. Napendekeza katika kuonyesha uongozi bora Waziri wa Fedha amwombe CAG kufanya ukaguzi wa haraka wa Benki Kuu hasa kwenye matumizi ya ujenzi na ukarabati wa majumba yao yote na kuona kama taratibu zimefuata na gharama inaendana na kile kilichofanyika au kudaiwa kufanyika (value for money).

Ndugu zangu Benki Kuu haina rekodi nzuri inapokuja kwenye masuala ya matumizi ya fedha zetu; imekuwa ni sehemu ya mtandao wa kifisadi na hadi hivi sasa hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kuisafisha isipokuwa kubadilisha mapambo tu ya utendaji wa Benki hiyo. Tusipoangalia fedha za Uchaguzi Mkuu kwa chama kimoja nchini zitapatikana tena kwa mtindo huu huu wa ulaghai.
Ninachosema ni kuwa mkila tutawauliza, kama hamtaki tuwaulize…
hs3.gif

Ningependa kuuliza kaswali kama kuna wajenzi humu ukumbini. Hivi leo nikitaka kujenga nyumba ya kisasa pale Tanzania, yenye vyumba vitano, sebule mbili, jiko ya kisasa, ikiwa na air conditioning na matenki ya maji safi itanigharimu kiasi gani? Achilia mbali bwawa la kuogelea kwa sababu tupo karibu na pwani nitaogelea pale Coco Beach. Tuseme viwanja Oyster Bay na Masaki havipatikani, basi kule Boko.
 
Swali zuri sana, majibu yake yako kwenye bei za makandasi walio-omba hiyo kazi.
 
Kula mle kuuliza tusiwaulize?

Lula wa Ndali-Mwananzela​
Disemba 30, 2009
BENKI Kuu wanataka kula tena; wanataka kula bila kuulizwa na yeyote; wanataka kula huku tukiwatazama. Si huku tunawatazama tu bali wanataka wale huku tukiwapigia makofi kwa jinsi gani wanakula vizuri............
Huyu mwandishi angesubiri kidogo tu, asingeandika utumbo wote huu!
 
Hivi kwa nini serikali yetu na umaskini wake bado inawagharamia watu ujenzi wa nyumba, magari n.k. eti nyumba za mashirika watu wanakaa bure, eti polisi naye anajengewa nyumba huu ni upuuzi kabisa. Angalieni wenzenu nchi za ulimwengu wa kwanza hakuna eti boss wa bank sijui polisi au meneja anaishi kwenye nyumba ya shirika. Hizi pesa zingetumika kujenga mashule na mahospitali. BOT turudishieni pesa zetu nyumba zipigwe mnada huu ni upuuzi. wauzieni hizo nyumba balozi mturudishie pesa yetu nanyi mje tubanane uswahilini.
 
Nifahamishe huo usanii kwenye hiyo Taarifa.

Tunakupa usanii huu hapa:
Kwanza gavana wa BOT ni kama CEO wa kampuni hana ulazima wa kupewa nyumba kwasababu ni kazi ya kuteuliwa na uteuzi hufanywa kwa mchakato. Tofautisha gavana na bank officer wa BOT yule ameajiriwa na gavana ameteuliwa nadhani umeshanifahamu vizuri. Najibu statement hii

"Gavana wa Benki Kuu pamoja na Manaibu wao wanastahili kupewa nyumba kwa mujibu wa mikataba yao ya kazi" BOT Act inasema kuwa Governor anateuliwa na rais but haitwambii anamteua kwakuwa mshkaji wake au ufanisi wake au la"

Pili katika Act ya 2006 inasema rais anafahamu mshahara na allowance ya bwana ndulu, navyofahamu mie mojawapo ni nyumba sijui rais alitaarifiwa hili kama trustee wetu au alimezea tu.

Tatu tuje katika mchakato mzima wa mikataba ya BOT inasema taarifa na nukuu
"Awali Benki Kuu ilikuwa na viongozi wakuu wawili, Gavana na Naibu wake mmoja. Baada ya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2006, Benki Kuu ina viongozi wakuu wanne; Gavana na Manaibu wake watatu. Kila mmoja wao, kwa mikataba iliyowekwa anastahili kupata nyumba ya kuishi" Swali ni nani anayedesign mikataba ya magavana na manaibu wake? Jibu utakuja kukuta ni board ambayo inakuwa approved by the Minister for Finance. Who is the chairman of the BOT board Benno Ndullu. Safi sana!!!!.

Vile vile huyo ndulu na nakuu katika Report inasema hivi,
"Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned)."
Nani aliyefanya maamuzi haya wakati huo ni Board ya BOT ambapo bwana Ndullu alikuwa ni mjumbe wetu adhimu ndani ya board hiyo. Sasa unadhani hata mjinga kama mnamtengenezea ulaji ataukataaaa!!!!Haihitaji kuwa na PhD kufahamu linaloendelea hapa Board ilikaaa wewe ukiwamo ndani kudiscuss ulaji wa mnene gavana unadhani wewe kama mjumbe utakataaa!!!

Vilevile nanukuu kutoka katika report hii adhimu,
"Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania"
mwisho wa kunukuu. Je swali nauliza nani mwenyekiti wa bodi ya zabuni BOT (au kiinglishi Central Tender Board) jibu unakuta ni Professor Ndulu.
Swali jengine Ndulu kateuliwa ugavana lini? 8 Jan 2008.

Mwenyekiti wa bodi Gavana, hoja ya kujengwa nyumba mpya alikuwa mjumbe, Tenda na yeye yumo kama si usanii ni kitu gani haswa. Wataalamu wa finance akina Professor Elton Gruber anakwambia "The Dog That did not Bark" ndio hiyo hata kama mbwa habweki but haimaanishi haumi.
 
Nashindwa kuweka post kwa sababu bado naona kuwa huu ni wizi tu na sijui ni nani alaumiwe; $1.2m ni nyingi sana kwa ujenzi wa nyumba hizo nilizoona sehemu mbalimbali. Tatizo la nchi yetu ni kuwa watu hangalia bei za nyumba huko Marekani na kuzitumia kupanga bei za hapa Tanzania!!
 
Tunakupa usanii huu hapa:
Kwanza gavana wa BOT ni kama CEO wa kampuni hana ulazima wa kupewa nyumba kwasababu ni kazi ya kuteuliwa na uteuzi hufanywa kwa mchakato. Tofautisha gavana na bank officer wa BOT yule ameajiriwa na gavana ameteuliwa nadhani umeshanifahamu vizuri.
Hapo juu nimekufahamu...
Pili katika Act ya 2006 inasema rais anafahamu mshahara na allowance ya bwana ndulu, navyofahamu mie mojawapo ni nyumba sijui rais alitaarifiwa hili kama trustee wetu au alimezea tu.

Tatu tuje katika mchakato mzima wa mikataba ya BOT inasema taarifa na nukuu
Swali ni nani anayedesign mikataba ya magavana na manaibu wake? Jibu utakuja kukuta ni board ambayo inakuwa approved by the Minister for Finance. Who is the chairman of the BOT board Benno Ndullu. Safi sana!!!!.

Vile vile huyo ndulu na nakuu katika Report inasema hivi,

Nani aliyefanya maamuzi haya wakati huo ni Board ya BOT ambapo bwana Ndullu alikuwa ni mjumbe wetu adhimu ndani ya board hiyo. Sasa unadhani hata mjinga kama mnamtengenezea ulaji ataukataaaa!!!!Haihitaji kuwa na PhD kufahamu linaloendelea hapa Board ilikaaa wewe ukiwamo ndani kudiscuss ulaji wa mnene gavana unadhani wewe kama mjumbe utakataaa!!!

Vilevile nanukuu kutoka katika report hii adhimu,
"Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania"
mwisho wa kunukuu. Je swali nauliza nani mwenyekiti wa bodi ya zabuni BOT (au kiinglishi Central Tender Board) jibu unakuta ni Professor Ndulu.
Swali jengine Ndulu kateuliwa ugavana lini? 8 Jan 2008.

Mwenyekiti wa bodi Gavana, hoja ya kujengwa nyumba mpya alikuwa mjumbe, Tenda na yeye yumo kama si usanii ni kitu gani haswa. Wataalamu wa finance akina Professor Elton Gruber anakwambia "The Dog That did not Bark" ndio hiyo hata kama mbwa habweki but haimaanishi haumi.

Nimekufahamu kuwa tatizo hapa ni Ndulu na sio gharama za ujenzi. Kama ndio hivyo basi sina swali lingine unless otherwise kama hukubaliani na gharama za ujenzi huo.
 
BoT Wachajaribu kuwaelewesha Watanzania ni kuwa kujenga Nyumba 2 kwa Mil 2.4 USD...ni sawa sawa kabisa..ni sawa na kununua soda kwa Shs 500.

BoT hapa inajaribu hata kuwashangaa Watanzania kwa nini wanalalamika, wakati hizi gharama hazina TATIZO lolote...ni Tshs Bilioni 2.4 tuuu.
 
Back
Top Bottom