Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
- Thread starter
-
- #41
Mimi mwenyewe ninamchukulia serious sana. Nimeshangaa sana kwanini asifuate utaratibu. Zipo namna nzuri tu za kuwaita viongozi wa vyama vya siasa. Lakini siyo kihuni tu. Huwezi ukamwita kiongozi wa siasa kwa kumtumia sms.Sema jamaa huwa namtake kama mwanahabari serious sana na mwenye weledi mkubwa , Kama ni kweli kafanya hivyo basi atakuwa anajivunjia heshima kwa watu waliokuwa tunamuamini na kumuheshimu
Mtamteka?Odemba, tutamuonya kupotosha umma.
Ccm wangeshiriki, ningeshangaa Sana, kwamba, wenye akili wapo ccm!?!Chama cha Mapinduzi kinautaarifu umma kuhusu mdahalo wa jana:
View attachment 3084263
View attachment 3084264
Mwalimu Pambalu yule chuma! We KKNOCKOUT MAPEMA SANA CCMCcm wangeshiriki, ningeshangaa Sana, kwamba, wenye akili wapo ccm!?!
Ccm wanaishi kwa hila, na kulindwa na vyombo vya Dora, hawana regitimacy ya kuwa pale, sio katibu wao tu, hata samia hawezi kufanya mdahalo na John pambalu, achilia mbali Lisa, au mbowe,
Odemba afuate utaratibu aache uhuniCcm wangeshiriki, ningeshangaa Sana, kwamba, wenye akili wapo ccm!?!
Ccm wanaishi kwa hila, na kulindwa na vyombo vya Dora, hawana regitimacy ya kuwa pale, sio katibu wao tu, hata samia hawezi kufanya mdahalo na John pambalu, achilia mbali Lisa, au mbowe,
Ule mdahalo wa kishenzi.Kwa kweli sijajua.
Na hata hivyo sidhani kama ingekuwa sahihi kwa dr nchimbi kuhudhuria mjadala ule ambao mtu wa CCM akisimama anaanza kuzomewa ?
Mdahalo wenye audience wa aina hiyo ni sahihi kweli kwa watu wenye akili timamu kuhudhuria ?
Inabidi ukamatwe kwa kuchafua chama tawalaChama cha Majizi na Matekaji.
DENISS JOE MSACKY AGAINπ³π³π³π³π³ kipindi kile cha kesi ya ugaidi ya Lwakatare na kutekwa na kuumizwa kwa Dr UlimbokaChama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu kutoshiriki kwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenye mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Televisheni cha Star Tv, na kuratibiwa na Ndugu Edwin Odemba tarehe 31 Agosti, 2024.
CCM inautaarifu umma kuwa Katibu Mkuu hakukimbia wala hakudharau mdahalo huo. Balozi Nchimbi alifanya kila jitihada za mawasiliano na muaandaji na tunasikitishwa na jinsi alivyoupotosha umma.
Tarehe 10 Agosti 2024 mtangazaji wa Kituo cha Televisheni, Star Tv, Ndugu Edwin Odemba alimtafuta Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (sms) akimuomba Katibu Mkuu ashiriki mdahalo huo wa viongozi wa vyama vya siasa uliopangwa kufanyika Jumamosi, tarehe 31 Agosti 2024.
Katibu Mkuu alimjulisha kuwa masuala ya vyombo vya habari yanaratibiwa na Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla hivyo awasiliane naye na akampa namba ya simu ya mkononi ya Ndugu Makalla.
Kwa sababu ambazo Odemba anaweza kuzieleza mwenyewe, katika kipindi cha takriban wiki tatu, hakufanya mawasiliano au kumtafuta Ndugu Makalla kama alivyoelekezwa na kushauriwa na Katibu Mkuu Balozi Nchimbi.
Baada ya kuhisi kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inaweza kuwa ngumu kupatikana kutokana na majukumu yake ya kazi za chama, Ndugu Odemba alimtafuta tena Balozi Nchimbi akiomba amuandae mwakilishi huku matangazo ya mdahalo huo yakiendelea kumtaja Katibu Mkuu wa CCM kuwa ndiye atakayeshiriki. Badala yake Katibu Mkuu alimwelekeza Ndugu Odemba kutofanya lolote kabla ya kupata mawasiliano na Sekretarieti ya Chama.
Kimsingi Ndugu Odemba alitaka wananchi wadanganywe kuwa CCM kupitia kwa Katibu Mkuu ilikuwa imethibitisha kushiriki katika mdahalo huo jambo ambalo si sahihi.
Katika mazingira ya kustaajabisha tumeshangazwa na machozi ya Ndugu Odemba aliyotoa jana akielekeza lawama kwa CCM na kwa Katibu Mkuu wakati alijua bayana kwamba alikuwa hajapata uthibitisho wowote wa CCM kushiriki ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba yeye mwenyewe alishajua kwamba alikuwa akiendelea kutangaza kuhusu mdahalo huo kama "promo" pasipo kupata ridhaa ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM ndiye Mwenyekiti wa Sekretarieti na siku nzima ya jana ambayo ndiyo siku Odemba alipanga kufanyika kwa mdahalo huo, kulikuwa na vikao vya maandalizi ya Kamati Kuu Maalum ambayo inafanyika leo tarehe 01 Septemba 2024, jambo ambalo kwa namna yoyote Katibu Mkuu asingeweza kuwapo katika mdahalo huo hata kama angekuwa amethibitisha awali.
Kushiriki kwenye mdahalo kunahitaji mashauriano na maafikiano kati ya waandaji na waalikwa.
Tunaweza kutamka bayana na kwa uhakika kwamba Katibu Mkuu hakuwa ametoa uthibitisho wa kuhudhuria mdahalo huo. Hakukuwa na makubaliano yoyote rasmi ya yeye au mwakilishi wake kuhudhuria katika shughuli hiyo. Mwisho, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Nchimbi yupo tayari kwa midahalo, majadiliano na makongamano yanayolenga kujenga umoja wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa kadiri ya taratibu zilizopo na ratiba yake ya kazi inavyoruhusu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
View attachment 3084263
View attachment 3084264
Pia soma
- Kuelekea 2025 - Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa: Nchimbi kaingia mitini, wengine wagoma kushiriki!
Mbona unahaha ndugu yangu.DENISS JOE MSACKY AGAINπ³π³π³π³π³ kipindi kile cha kesi ya ugaidi ya Lwakatare na kutekwa na kuumizwa kwa Dr Ulimboka
Huu ufafanuzi wa CCM na taarifa zilizosambaa umenishtua sana! Kwanza, sijui kama wengine ilikuwa hivi yaani, unamwitaje Katibu Mkuu wa Chama kwa mssage fupi ashiriki mdahalo? Pili, huu mdahalo ulikuwa wa taasisi dhidi ya taasisi yaani StarTv na vyama vya siasa au na mtu (Odemba). Kama ni taasisi kwanini StarTv haikuepelka barua kwenye vyama husika? Jamaa kashindwa kuonyesha professionalism kabisa.πππBarua hizi zinaeleza kwamba Ndugu Edwin Odemba alitangaza kushiriki kwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kwenye mdahalo ulioratibiwa tarehe 31 Agosti, 2024, bila kuwa na uthibitisho wa kushiriki kutoka kwa Katibu Mkuu huyo. Katika barua hizo, inaonekana wazi kwamba Ndugu Odemba alikuwa anajua kuwa hakupata ridhaa wala uthibitisho wa kushiriki kwa Katibu Mkuu, lakini aliendelea kutumia jina lake kwa kutangaza ushiriki wake.
Kwa mujibu wa taarifa hizo:
Kwa hiyo, Ndugu Odemba anashutumiwa kwa kutoa taarifa za uongo kwa umma kuhusu ushiriki wa Katibu Mkuu kwenye mdahalo, wakati akijua wazi kuwa hakuwa na uthibitisho wa ushiriki huo. Hili linaweza kuchukuliwa kama udanganyifu kwa makusudi.
- Taarifa ya CCM: Inabainisha kuwa Katibu Mkuu hakutoa uthibitisho wa kushiriki kwenye mdahalo huo na kwamba aliendelea na majukumu yake mengine. Ndugu Odemba alishauriwa kuwasiliana na Ndugu Amos Gabriel Makalla, lakini hakufanya hivyo. Badala yake, aliendelea kutangaza kuhusu ushiriki wa Katibu Mkuu, jambo ambalo ni kinyume na ukweli.
- Taarifa ya Msaidizi wa Katibu Mkuu: Inaeleza kwamba ushiriki kwenye mdahalo unahitaji mashauriano na makubaliano kati ya waandaaji na waalikwa, ambayo hayakufanyika. Pia, barua hiyo inaeleza kwamba Katibu Mkuu alikuwa na vikao vya Kamati Kuu Maalum siku hiyo, hivyo asingeweza kushiriki hata kama angepata uthibitisho wa awali.
4o
You said:
View attachment 3084335View attachment 3084334