Majibu ya hoja za uzi kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani nitajibu humu

Majibu ya hoja za uzi kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani nitajibu humu

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Habari za muda huu wana Jf, nimeona na kusoma comments zote za uzi wa Retired wenye kichwa cha habari " Kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani?

Nilichogundua watu wamekosa umakini kwa kiwango kikubwa watu wengi wanajadili bila facts na porojo nyingi sasa nimejipanga kujibu baadhi ya hoja nilizoziona haziko sahihi na za upotoshaji wa kiwango kikubwa katika uzi ule humu maana imezidi mno kuna watu wamefikia kusema eti wali kwa mama Ntilie unapata kwa Tsh 500/= .

Mimi ni mkazi wa Dar kwa kuzaliwa na kusoma Dar kuanzia awali mpaka form Six, ndugu na marafiki zangu wengi wametapakaa sehemu mbalimbali za jiji la Dar hali hiyo imenifanya nitembelee na kuishi sehemu nyingi mbalimbali za jiji la Dar kuanzia wanapopoita ushuani mpaka uswahilini hivyo niko well informed na jiji la Dar kama mtani wangu GENTAMYCINE Temeke ,Yombo yote vituka kiwalani na Buza hapo ndio maskani kabisa bila kusahau Mbagala, Chamazi na mbande, Upanga, Tandale nk

Kwa vile naelekea msibani sasa maeneo ya Yombo nina ahidi mida ya usiku panopo majaaliwa nitaleta uchambuzi na kujipu hoja za upotoshaji katika uzi ule maana kuna watu wameletwa Dar na magari ya ng'ombe wametembea maeneo mawili lakini kwenye ID fake wao wajuaji wa kila kitu sasa naomba tukutane katika uzi huu baadae kwa hoja na ushahidi bila blah blah.
IMG_20220910_114241.jpg


IMG_20220910_114328.jpg


#UziUtaeendelea
 
Habari za muda huu wana Jf ,nimeona na kusoma comments zote za uzi wa Retired wenye kichwa cha habari " kwa nini ardhi ya mbagala hauna thamani ?


#UziUtaeendelea
Ninachojua kuna Watu wana Maisha mazuri wanaishi huko Mbagala Kunakodharaulika kuliko hata Waishio Oysterbay, Masaki, Msasani, Mikocheni, Upanga, Kijitonyama, Mbezi Beach, Goba, Sala Sala, Kigamboni, Tegeta na Mbweni.
 
Bila kusahau #security wise ya eneo matter,Nina ndugu yangu amejenga mbagala,amehama na kununua Boko Kwa hela nyingi Kwa maswala ya usalama wake na familia.
-kama nataka kabwakabwa nenda mbagala.
 
Ninachojua kuna Watu wana Maisha mazuri wanaishi huko Mbagala Kunakodharaulika kuliko hata Waishio Oysterbay, Masaki, Mikocheni, Upanga, Kijitonyama, Mbezi Beach, Tegeta na Mbweni.
Kweli kabisa na nashangaa kuna watu wanasema Yombo na kusahau sehemu ambayo inakaliwa na watu wengi kutoka mkoa wako pendwa Mara ambayo ni Kivule ina miundombinu mibovu sana..
 
Wengi wao ni wale waliotoka mikoani na magari ya ng'ombe wametembea sehemu mbili tatu au usikute hajawahi kufika Mbagala kabisa wanakuja kuleta ujuaji wa kijinga.

Wengine walikuwa wanalala pamoja na mifugo sasa sijui wanatoa wapi guts za kuisema vibaya Mbagala.
Mbagala ya miaka 90 sio hii ya sasa.
 
Mbona umeweka picha za yombo vituka..


Yombo vituka ardhi yake imepimwa na serikali sehemu kubwa.

Ni viwanja vichache viko kienyeji enyeji
Nimeweka kwa sababu nimesema najibu hoja za uzi ule Nikimaanisha mpaka comments sasa kwenye uzi haikusemwa mbagala pekee yake watu wamesagia kunguni kuwa Temeke nzima ukijumlisha Yombo na Buza ni sehemu za hovyo na kuzisifia Goba ,kimara na Madale sasa nimekuja kuwaprove wrong.
 
kuna namna tu ukisema unaishi mbagala hadhi yako inashukaa sanaa huo ndio ukwelii japo sio kweli kuwa mbagala wanaishi watu wenye uwezo wa chini hapana. Kuna mzee alikuwa anaishi kule lakini akahama akajenga mbezi na sababu kubwa eti sababu ni MBAGALA
 
Nimekumbuka uzi wa KidukuLilo kwenye kikao chake na matajiri USA akaonyesha picha za mijengo yake Masaki , Ostabei na Posta na kuwaambia nchini kwao huko ndiko kuna wanakaa matajiri rafiki zake walihuzunika mno na kulia kuwa Tanzania kuna maisha magumu mno.

Sasa unakuta Jf mtu yupo kimara sijui ,Goba nk kuna maji shida ,usafiri shida anajiona yupo NewYork inasikitisha sana..
 
Nimekumbuka uzi wa KidukuLilo kwenye kikao chake na matajiri USA akaonyesha picha za mijengo yake Masaki , Ostabei na Posta na kuwaambia nchini kwao huko ndiko kuna wanakaa matajiri rafiki zake walihuzunika mno na kulia kuwa Tanzania kuna maisha magumu mno.

Sasa unakuta Jf mtu yupo kimara sijui ,Goba nk kuna maji shida ,usafiri shida anajiona yupo NewYork inasikitisha sana..
Sasa wewe ulikua unaamini stori za kiduku haha
 
Back
Top Bottom