Kitu ambacho nadhani unashindwa kukikubali ni kuwa, Kikwete kafanya mengi ya maana kwenye suala la umeme.
Alipochukua nchi kakumbana na mambo mengi sana, na kwa kibajeti chetu finyu afanye mangapi kwa pamoja? Katika priorities alizokuwa nazo, hili la umeme lipo na hajalisahau, utakumbuka kwamba, alipochukua urais nchi ilikuwa kizani. Akafanya haraka haraka iletwe mitambo ya emergency, matokeo tunayajua, na kwa bahati nzuri zikanyeesha mvua nzuri sana tukawa hatuna haja hata ya kuiwasha hiyo mitambo.
Ukame ule alioukuta Kikwete uliambatana na njaa kali sana, Kikwete akasema hafi mtu hapa. Akafanya kila njia na kweli hakufa mtu kwa njaa ile. Bahati nzuri sana mvua ile iliyojaza mabwawa ya hifadhi kwa ajili ya umeme, ilitusaidia kwa miaka minne mfululizo, na kina cha maji kilikuwa kizuri tu, sasa fedha inayohitajika sana sehemu zingine, ikaanza kutumika huko, kwenye mashule, mabarabara, ma university na mitambo ya umeme iliyokuwepo Ubungo ilionekana kuwa itatosha kabisa kama kuna tatizo.
Kilichotokea baada ya hapo ni wimbi la wawekezaji, wimbi la matumizi ya umeme yasio ya kawaida na umeme ukawa unahitajika na unaongezeka kwa 14% kila mwaka. Kikwete akaagiza mitambo kama mahitaji ya maongezeko, ghafla tumekumbwa na ukame, mitambo ambayo iliagizwa ku cover ongezeko la kawaida la kila mwaka ndio inatumika kujaziliz umeme ambao haufuliwi kwa ajili ya kupungua vina vya maji kwenye mabwawa. Hapo jamani ni nani wa kumlaumu? ingekuwa hajafanya kweli, mimi ningekuwa wa kwanza kumlaumu.
Kumbukeni kuna sababu ambazo zinakuwa nje ya uwezo wa yeyote awaye, lakini kizuri ni kwamba Kikweye hata kwa hilo hajasema hapana hapa ndio mwisho, kawekeza kwenye mkaa wa mawe, kawekeza kwenye upepo na sasa anahuisha umeme wa steigler.
Jee, ni madogo hayo?
Data zinaonesha average yake ya kuwekeza kwenye umeme kwa mwaka ni way above wote waliomtangulia. Wakati wenzake waliwekeza wastani wa 7.5MW kwa mwaka yeye anawekeza 50MW kwa mwaka, hilo nii kubwa sana na kasema itaongezeka kufikia uwiano wa 200MW kwa mwaka kabla ya kumaliza muda wake. Its a big achievement uki compare na wote waliopita. Na vilevile akabadilisha sheria ya monopoly kwenye umeme ili wafuaji binafi waweze kuwekeza na matokeo tunayaona.