Majibu ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka mbele ya Baraza la Maadili

Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka alisomewa mshtaka manne katika Baraza la Maadili kutokana na malalamiko manne ya kukiuka maadili ya Viongozi wa Umma ambapo ameyakana yote

Kikao cha Baraza la Maadili liliketi chini ya Mwenyekiti wa Baraza, Jaji Mstaafu Rose Temba, upande wa mlalamikaji umewakilishwa na Mawakili wa Serikali, Emma Gellan na Hassan Mayunga ambapo hitimisho lilipatikana jana Oktoba 17, 2024.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Honoratus Ishengoma amesema “Baraza limesikiliza utetezi wake (Prof. Sedoyeka), Mwenyekiti amesema baada ya kusikiliza pande zote mbili, litafanya hitimisho na ushauri utapelekwa kunakohusika.”

Pia soma
~
Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote
~ Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yawasilisha malalamiko kuhusu Prof. Eliamini M. Sedoyeka

MAJIBU YA PROFESA HAYA HAPA
1. Tuhuma ya kuwa na ukaribu na Bw. Hakimu Ndatama na uhamisho wake kurudi IAA pindi mimi niliporejea kuwa Mkuu wa Chuo

Uhamisho wa Bw. Ndatama kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ulifuata taratibu zote za kisheria na kufuatia mahitaji ya kikazi, Chuo kiliandika kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba Bw. Ndatama arejeshwe. Hili la kuomba arejeshwe lilifanyika kabla hata ya mimi kurejea IAA kutokana na mahitaji ya kikazi.

2. Tuhuma kuhusu Uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama kuwa Mkuu wa Sehemu

Kuhusu tuhuma ya kutekeleza uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama na mgongano wa maslahi, napenda kueleza kuwa uteuzi huu ulikuwa na msingi mzuri unaozingatia uwezo na ufanisi wake katika utekelezaji wa
majukumu yake.

Nilizingatia sifa za Bw. Ndatama na uwezo wake wa kuchangia maendeleo ya IAA. Nikiwa na dhamira ya kulinda maslahi ya taasisi na kuhakikisha tunapata watu wenye uwezo wa kuchangia katika malengo yetu ya taasisi. Bw. Ndatama si ndugu yangu, si kabila langu, si dini yangu, si rafiki yangu na wala hakuna chochote kinachoniunganisha naye. Sina maslahi naye kwa namna yoyote ile.

3. Zabuni ya Viti na Meza vya Wanafunzi kwa Kampasi ya Babati

Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na. 7 ya mwaka 2013), inampa mamlaka Afisa Masuuli kukataa kuendelea na zabuni ama kurejesha zabuni kwenye Bodi ya Zabuni.

Vifungu hivyo vimefafanua kwamba atakapofanya hivyo ataeleza sababu na kupata idhini ya Bodi ya zabuni (Tender Board). Ninaweka wazi msimamo wangu kwamba nilifuata taratibu zote na sikuvunja sheria bali
nilikuwa nikitekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa Sheria.

Kama kiongozi mwaminifu kwa nchi yangu, nimekuwa makini kuhakikisha taasisi inapata bidhaa bora kwa njia za uwazi na kwa gharama nafuu kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Katika mazingira yote ya manunuzi ya umma, dhamira yangu kama Afisa Masuuli ni kuongeza wigo wa ushindani kwa lengo la kupata thamani halisi ya pesa za Umma (value for money). Hivyo nimekuwa na msimamo wa uwazi na kuzingatia taratibu zinazotakiwa, kwa lengo la kulinda maslahi ya
taifa na kuimarisha taasisi ili iweze kufikia malengo yake ya kutoa elimu bora kwa jamii.

4. Tuhuma kuhusu Uhamisho wa Ndani wa Mtumishi Bw. Robert Mwitango

Kwa ujumla uhamisho wa ndani wa watumishi hufanywa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kiutendaji wa taasisi.

Katika Mwaka wa 2023/2024 Idara ya Maktaba ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo zile ambazo kwa uhalisia wake zilihitaji msaada wa karibu wa kitengo cha Manunuzi ya Umma, kama Stock taking, Asset Verification” na Ununuzi mkubwa wa vitabu kwa mkupuo.

Nilipotathmini ukubwa wa majukumu hayo, unyeti wake na namna yanavyohitaji utaalamu wa manunuzi ya umma, niliamua mtumishi mmoja afanyiwe uhamisho wa ndani kutoka kitengo cha Manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
Wasomi wanalilia vyeo. Kwenye hivi vyuo kuna watu wanaoneana wivu sana na pia wanaopwndeleana sana. Ila mashitaka haya naona ni migogoro binafsi wa watu maofisini.
 
Vituhuma vidogo vidogo kama hivi kwa nini vinapewa publicity kubwa? Kuna jambo lipo nyuma ya pazia. Isije ikawa huyu Prof ana mpango wa kugombea nafasi ya kisiasa kwa hiyo anapata preemptive attacks.
Wanaopaswa kuivusha Tz kupitia taaluma zao wanawaza nafasi za kisiasa ili wakaimbe Mama mama mama.

Bora wapigwe speed governor tu.

NB: Hii komenti ni ya jumla haimhusu Prof Sedoyeka pekee
 
Ulitaka hukumu bila kusikilizwa upande wa mshatakiwa
Hapo kwa kijana wa manunuzi kumpeleka library...lazima atakuwa amedanganya tu ...akina MILARD AYO ndo fursa zenu hizi kwenda kumhoji kijana...haiwezekani serikali itoe pesa kumsomesha mtu manunuzi halafu aishie kufanya kazi library kwani hamna librarian???
 
Hili nalo ni tatizo, ila humu makazini watu wengi wanafanya majukumu ambayo hawajasomea.
 
Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamini Sedoyeka alisomewa mshtaka manne katika Baraza la Maadili kutokana na malalamiko manne ya kukiuka maadili ya Viongozi wa Umma ambapo ameyakana yote

Kikao cha Baraza la Maadili liliketi chini ya Mwenyekiti wa Baraza, Jaji Mstaafu Rose Temba, upande wa mlalamikaji umewakilishwa na Mawakili wa Serikali, Emma Gellan na Hassan Mayunga ambapo hitimisho lilipatikana jana Oktoba 17, 2024.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Honoratus Ishengoma amesema “Baraza limesikiliza utetezi wake (Prof. Sedoyeka), Mwenyekiti amesema baada ya kusikiliza pande zote mbili, litafanya hitimisho na ushauri utapelekwa kunakohusika.”

Pia soma
~
Prof. Eliamini Sedoyeka asomewa tuhuma nne kwenye Baraza la Maadili, azikana zote
~ Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yawasilisha malalamiko kuhusu Prof. Eliamini M. Sedoyeka

MAJIBU YA PROFESA HAYA HAPA
1. Tuhuma ya kuwa na ukaribu na Bw. Hakimu Ndatama na uhamisho wake kurudi IAA pindi mimi niliporejea kuwa Mkuu wa Chuo

Uhamisho wa Bw. Ndatama kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ulifuata taratibu zote za kisheria na kufuatia mahitaji ya kikazi, Chuo kiliandika kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba Bw. Ndatama arejeshwe. Hili la kuomba arejeshwe lilifanyika kabla hata ya mimi kurejea IAA kutokana na mahitaji ya kikazi.

2. Tuhuma kuhusu Uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama kuwa Mkuu wa Sehemu

Kuhusu tuhuma ya kutekeleza uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama na mgongano wa maslahi, napenda kueleza kuwa uteuzi huu ulikuwa na msingi mzuri unaozingatia uwezo na ufanisi wake katika utekelezaji wa
majukumu yake.

Nilizingatia sifa za Bw. Ndatama na uwezo wake wa kuchangia maendeleo ya IAA. Nikiwa na dhamira ya kulinda maslahi ya taasisi na kuhakikisha tunapata watu wenye uwezo wa kuchangia katika malengo yetu ya taasisi. Bw. Ndatama si ndugu yangu, si kabila langu, si dini yangu, si rafiki yangu na wala hakuna chochote kinachoniunganisha naye. Sina maslahi naye kwa namna yoyote ile.

3. Zabuni ya Viti na Meza vya Wanafunzi kwa Kampasi ya Babati

Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na. 7 ya mwaka 2013), inampa mamlaka Afisa Masuuli kukataa kuendelea na zabuni ama kurejesha zabuni kwenye Bodi ya Zabuni.

Vifungu hivyo vimefafanua kwamba atakapofanya hivyo ataeleza sababu na kupata idhini ya Bodi ya zabuni (Tender Board). Ninaweka wazi msimamo wangu kwamba nilifuata taratibu zote na sikuvunja sheria bali
nilikuwa nikitekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa Sheria.

Kama kiongozi mwaminifu kwa nchi yangu, nimekuwa makini kuhakikisha taasisi inapata bidhaa bora kwa njia za uwazi na kwa gharama nafuu kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Katika mazingira yote ya manunuzi ya umma, dhamira yangu kama Afisa Masuuli ni kuongeza wigo wa ushindani kwa lengo la kupata thamani halisi ya pesa za Umma (value for money). Hivyo nimekuwa na msimamo wa uwazi na kuzingatia taratibu zinazotakiwa, kwa lengo la kulinda maslahi ya
taifa na kuimarisha taasisi ili iweze kufikia malengo yake ya kutoa elimu bora kwa jamii.

4. Tuhuma kuhusu Uhamisho wa Ndani wa Mtumishi Bw. Robert Mwitango

Kwa ujumla uhamisho wa ndani wa watumishi hufanywa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kiutendaji wa taasisi.

Katika Mwaka wa 2023/2024 Idara ya Maktaba ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo zile ambazo kwa uhalisia wake zilihitaji msaada wa karibu wa kitengo cha Manunuzi ya Umma, kama Stock taking, Asset Verification” na Ununuzi mkubwa wa vitabu kwa mkupuo.

Nilipotathmini ukubwa wa majukumu hayo, unyeti wake na namna yanavyohitaji utaalamu wa manunuzi ya umma, niliamua mtumishi mmoja afanyiwe uhamisho wa ndani kutoka kitengo cha Manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
Ingawaje kwa kiasi fulani amejitahidi kujibu baadhi ya hoja kwa usahihi, lakini bado kuna baadhi ya hoja ambazo anapaswa azitolee ufafanuzi wa kina zaidi, hususani kuhusu suala hili la Uhamisho wa Ndani wa huyo Mtumishi mwenye taaluma ya manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
1. Kama lengo lilikuwa ni kuongeza ufanisi kwenye Idara hiyo ya Maktaba, Je, ni kwa nini Mtumishi huyo aliyehamishwa hakupewa na Maainisho ya Majukumu yake Mapya (Job Descriptions mpya) wakati alipohamishiwa huko Maktaba??
2. Kwa kuwa Mtumishi huyo hakupewa New Job Descriptions, maana yake ni kwamba Majukumu yake yale yale ya awali aliyopangiwa na Mwajiri wake ndiyo anapaswa kuendelea nayo akiwa huko kwenye Idara mpya ya Maktaba alikohamishiwa. Sasa; Je, kwa nini Mtumishi huyo apangiwe majukumu mengine Mapya kabisa kinyume na taaluma yake aliyosomea na kinyume kabisa na majukumu yake ya awali ambayo alipangiwa na ambayo pia ndio sababu za Msingi zilizopelekea Mtumishi huyo kuajiriwa na hiyo taasisi? So Where is the purpose of Professionalism and Job Specialization for the Job-seekers or Employees?? Je, kulikuwa na sababu gani ya kumuajiri Mtumishi mwenye sifa hizo za taaluma ya Manunuzi wakati kazi zake au majukumu yake atakayopangiwa hayaendani na uhitaji wa taaluma hiyo?? Jambo hili ni kitendo cha hatari Sana endapo kama utalifanyia tathmini ya kina Sana.
Yaani Kama vile Utawala wa Hospitali ya Muhimbili Leo hii kwa kutumia njia za holela waamue kuwabadilishia majukumu ya kazi baadhi ya Madereva na kuwapangia Majukumu Mapya ya kazi za Udaktari wa Tiba ya Binadamu na kisha kuwaruhusu Madereva hao waanze kuingia kwenye Vyumba vya Upasuaji Wagonjwa ili waweze kuwafanyia Upasuaji (Surgery) wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo!
Ridiculous!
 
Uko sawa kabisa... library waachiwe librarian na manunuzi waachiwe watu wa manunuzi...prof ana la kujibu hapa..
 
Katika kitu nimejifunza katika miaka ya gu ya kazi ni kujitahidi kucheza ndani ya STK za sehemu nilipo.

Kwanza nikipendelea mtu hua simuambii ili asije akashindwa kujizuia akatangaza, pili upendeleo wangu ulikua unatokea katika namna ambayo siachi gaps kwenye STK.
 
si prof kasema amempeleka huko maktaba kwa sababu maalum? uwe unaelewa na ww acha ushabiki
Sababu zipi hizo ambazo ni maalumu? Kuwakagua Wanafunzi wanaoingia na kutoka katika Chumba cha Maktaba au???

Ingawaje kwa kiasi fulani Profesa amejitahidi kujibu baadhi ya hoja kwa usahihi, lakini bado kuna baadhi ya hoja ambazo anapaswa azitolee ufafanuzi wa kina zaidi, hususani kuhusu suala hili la Uhamisho wa Ndani wa huyo Mtumishi mwenye taaluma ya manunuzi kwenda Idara ya Maktaba.
1. Kama lengo lilikuwa ni kuongeza ufanisi kwenye Idara hiyo ya Maktaba, Je, ni kwa nini Mtumishi huyo aliyehamishwa hakupewa na Maainisho ya Majukumu yake Mapya (Job Descriptions mpya) wakati alipohamishiwa huko Maktaba??
2. Kwa kuwa Mtumishi huyo hakupewa New Job Descriptions, maana yake ni kwamba Majukumu yake yale yale ya awali aliyopangiwa na Mwajiri wake ndiyo anapaswa kuendelea nayo akiwa huko kwenye Idara mpya ya Maktaba alikohamishiwa. Sasa; Je, kwa nini Mtumishi huyo apangiwe majukumu mengine Mapya kabisa kinyume na taaluma yake aliyosomea na kinyume kabisa na majukumu yake ya awali ambayo alipangiwa na ambayo pia ndio sababu za Msingi zilizopelekea Mtumishi huyo kuajiriwa na hiyo taasisi? So Where is the purpose of Professionalism and Job Specialization for the Job-seekers or Employees?? Je, kulikuwa na sababu gani ya kumuajiri Mtumishi mwenye sifa hizo za taaluma ya Manunuzi wakati kazi zake au majukumu yake atakayopangiwa hayaendani na uhitaji wa taaluma hiyo?? Jambo hili ni kitendo cha hatari Sana endapo kama utalifanyia tathmini ya kina Sana.

Mathalani, Yaani Kama vile Utawala wa Hospitali ya Muhimbili Leo hii kwa kutumia njia za holela waamue kuwabadilishia majukumu ya kazi baadhi ya Madereva na kuwapangia Majukumu Mapya ya kazi za Udaktari wa Tiba ya Binadamu na kisha kuwaruhusu Madereva hao waanze kuingia kwenye Vyumba vya Upasuaji Wagonjwa ili waweze kuwafanyia Upasuaji (Surgery) wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo!

Hoja hii Profesa Sedoyeka anapaswa aitolee Majibu ya kina kabisa yasiyoacha hata chembe ya mashaka.
 
Prof anaweza jaribu kuchomoka ila kuna sehemu unaona kabisa ana shida.

Afisa Daraja la kwanza unampeleka kua mapokezi Maktaba? Na siyo taaluma yake?

Afisa Daraja la pili anakua mkuu wa idara baada ya uhamisho ambao haujakamilika? Hapa kazi ipo
 
Hapo kwa kijana wa manunuzi kumpeleka library...lazima atakuwa amedanganya tu ...akina MILARD AYO ndo fursa zenu hizi kwenda kumhoji kijana...haiwezekani serikali itoe pesa kumsomesha mtu manunuzi halafu aishie kufanya kazi library kwani hamna librarian???
Tangu lini serikali inasomesha watu?
Walisomeshea enzi ya Nyerere tu
 
Mkuu wewe ungekuwa yule kijana wa manunuzi na ukapelekwa maktaba ..je ungekubali?usiwe unaongea kwa ushabiki jamaa ana hoja ya kujibu ..!!
Kweli hii hatari. Utolewe kwenye maokoto ukakae maktaba sio poa. Lazima pachimbike. Prof aelewe kwenye taasisi za serikali kuna watu wa vyeo vya chini wana nguvu kuliko hata makatibu wakuu na wanaogopeka kupitiliza. Wakati nikiwa mwanafunzi wa field wizara fulani nilishuhudia madingi fulani yanamdindia hadi waziri.
 
Mkuu wewe ungekuwa yule kijana wa manunuzi na ukapelekwa maktaba ..je ungekubali?usiwe unaongea kwa ushabiki jamaa ana hoja ya kujibu ..!!
Boss wako anaweza kukuhamisha na kukupangia kazi popote ndani ya taasisi kadri ya yeye anavyoona mahitaji. Tatizo vijana wa kisasa ni wajuaji sana. Kwa jibu la prof huyo kijana atajiteteaje? Yeye ni nani asihamishwe? Huko maktaba hakuna maofisa kama yeye? Au kaona hakuna 10% huko kaamua kudinda?

Sasa itakula kwake maana watu kama hao ni virusi ambao hakuna mtu atataka kufanya naye kazi. Loser atakuwa huyo mtumishi anayegoma kuhamishwa wala siyo huyo prof. Kingine cha kujiuliza huo uhamisho ni wa kudumu? Je amepangiwa kada mpya hadi aweweseke?
 
Back
Top Bottom