Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Acha urongo mleta mada mbeya ina uzuri gani sasa labda uniambie ule uzuri wa asili wa kijiografia kama milima,ukijani, na vinginevyo lakini sio kiujenzi
 
Nje ya nchi mbali, hajawahi kuvuka nje ya wilaya yake huyo

Ni kweli Tanzani hakuna jiji zuri hata moja bali kuna baadhi ya sehemu/mitaa nzuri/mizuri.

Kigenzo cha kuwa na jiji zuri inatakiwa jiji lote lipimwe ,wajenge miundombinu ya sehemu zote,kusiwe na slums wala mapori,huduma zote za kijamii zipatikane,jiji zuri foleni kama zote,hakuna subway hata moja!
 
Acha urongo mleta mada mbeya ina uzuri gani sasa labda uniambie ule uzuri wa asili wa kijiografia kama milima,ukijani, na vinginevyo lakini sio kiujenzi
Kwa iyo wakazi wake wanakaa kwenye mashimo Kama panya au kwenye vichuguu?
 
Kama Mbeya ni pazuri basi TAnzania hakuna miji mizuri. Mbeya! Pyuuuuuu!
Mbeya ni nzuri kuliko hivyo Vimiji vyenu uchwara,ukipewa picha ya ziwa ngozi au mlima loleza au miteremko ya barabara ya mlima kawetele unaweza Shani uko uswisi au Himalaya nk

Shida yenu hata hamjawahi tembea Tzn hii.

Kwanza Mwanza na Dom kuna uzuri gani hapo
 
Kwa hiyo kumbe kwenye majiji tu ndiyo pazuri?Nikieleza kwamba fedha/uchumi wa mikoa mingine unatumika vibaya/ambezlement ili kuyaremba tu hayo majiji mtabisha?Mimi kama mkulima wa mihogo nasikitika sana.
Lima tu mihogo hakuna namna ndo ushambiwa kuzuri uko
 
Mwanza iwe Na 3. Arusha ipande Na. 2, tenda haki!!
 
Sure, kwa uzuri wa kimandhari hakuna hapo mji wa kuufikia mji wetu wa Mbeya.
 
Tanzania Hakuna jiji zuri hata moja.

Tembeeni hata hapo Harare Zimbabwe uone Kama hutakuja kuufuta huu Uzi.

Eti mbeya ni Jiji, Dodoma ni jiji.[emoji3]
Ukisema ivo
Atakuja mtu kukutajia mji zaidi ya huo Harare
 
Shida inakuja pale wanapoweka mahaba na kusifia mikoa wanayotoka

Ni kuwaacha tu
Hilo ndio tatizo mkuu..

Shida kubwa ya Tanzania Ni mipango miji , nchi nzima ni takataka. Tuko zero. Nilikuwa naisikia Mwanza na sifa kila siku.

Siku nimefika niliingiwa na simanzi kuwa hi nchi haina watu wa City Plan? ... Mji uko hovyo. Kwenye makazi ya watu ni slams tupu. Milimani kwenye Good View kumejengwa vijumba jumba.

TANZANIA miji haitofautian Hakuna mji wa kumcheka mwingine yote ni sawa. Na tatizo kubwa Ni mipango miji. Haijulikani wapi Ni makazi ya watu na wapi Ni sehemu za biashara . Kwenye makazi watu pengine hakuna hata Barabara za mitaani na Kama zipo ni nyembamba hata Gari 2 hazipishani.

Kwenye makazi ya watu watu wameweka mafrem kila nyumba. Jamani tutembeeni hata hapo Malabo tuone majiji yanavyokuwa. Mji umepangwa Hadi unatamani ingemuwa bongo.


Tanzania kwakweli raia wake Wana hela na wanajenga ile mbaya ila wanaangushwa na serikali yao haipangi miji. Ndio maana unakuta mtu ana mjemgo wa maana katikati ya slam. Au ana jengo la maana sehemu haina hata mfumo wa majitaka.
 
Uzuri?Katika yepi?Majengo mazuri,watu wazuri,maisha maziri,hali ya hewa nzuri,uchumi mzuri "unaoshikika" ,rasilimali nzuri au kipi hasa unajikita?Au ndiyo Wanyaturu wanavyosema ..."the beauty is in the eyes"...?
Hata mimi nilitaka kumuuliza swali kama hili.
Anaposema uzuri anamaanisha nini? Mimi binafsi nimefika kwenye miji yote hiyo aliyoitaja na sijaona "uzuri" wowote wa hii miji.
Miji yote hii imepangwa vibaya, nyumba zimejengwa kiholela, uchafu umetapakaa kila mahali, miundo mbinu mibovu yaani kwa kifupi tu hakuna mji unovutia hapa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…